HOJA Kuna uhusiano gani kati ya uanachama wa chama cha siasa na kugombea uongozi wa Serikali ya Wanafunzi?

HOJA Kuna uhusiano gani kati ya uanachama wa chama cha siasa na kugombea uongozi wa Serikali ya Wanafunzi?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Joined
Jun 3, 2026
Posts
1
Reaction score
1
Ninaomba suala hili lifanyiwe uchunguzi na mjadala mpana, kwa sababu linagusa haki za wanafunzi na uendeshaji wa uchaguzi wa Serikali za Wanafunzi katika vyuo vya Tanzania.

Kuna hali inayodaiwa kuwepo katika baadhi ya vyuo nchini ambapo mwanafunzi anapotaka kugombea nafasi za juu katika Serikali ya Wanafunzi, kama vile Rais au Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi, anatakiwa kuwa mwanachama wa CCM au kuwa na kadi ya CCM/UVCCM.

Swali langu ni: Kuna uhusiano gani kati ya uanachama wa chama cha siasa na kugombea uongozi wa Serikali ya Wanafunzi?

Serikali ya Wanafunzi ni chombo kinachowawakilisha wanafunzi wote wa chuo, wakiwemo wanafunzi wenye mitazamo na itikadi tofauti za kisiasa, pamoja na wale ambao hawajajiunga na chama chochote cha siasa. Kwa mantiki hiyo, inashangaza kuona kwamba mtu anaweza kuzuiwa au kukosa nafasi ya kugombea kwa sababu tu hana kadi ya chama fulani.

Jambo hili linakuwa na uzito zaidi pale ambapo wanafunzi wanaambiwa wazi au wanaelekezwa kwamba ili uwe na nafasi ya kushinda au kugombea nafasi fulani, ni lazima uwe mwanachama wa CCM/UVCCM.

Ikiwa kweli utaratibu huu upo, ningependa kujua:
  1. Ni sheria, kanuni au kifungu gani kinachomlazimisha mwanafunzi kuwa mwanachama wa CCM ili agombee uongozi wa Serikali ya Wanafunzi?
  2. Je, vyuo vinavyotumia utaratibu huu vina kanuni zilizoandikwa zinazoweka sharti hilo?
  3. Kama Serikali ya Wanafunzi inawakilisha wanafunzi wote, kwa nini nafasi za uongozi ziwe zinahusishwa na uanachama wa chama cha siasa?
  4. Mwanafunzi ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa anapata wapi haki yake ya kugombea na kuchaguliwa?
Na kama kweli vyuo vinataka uchaguzi wa Serikali za Wanafunzi uwe wa kisiasa kwa kuhusisha vyama, basi swali lingine ni: Kwa nini isiwe wazi kuwa ni ushindani wa vyama mbalimbali vya siasa, badala ya kutumia mfumo wa Serikali ya Wanafunzi ambao unapaswa kuwawakilisha wanafunzi wote?

Ninatoa mfano wa Centre for Foreign Relations (CFR/Kurasini), chuo nilichowahi kusoma, ambapo suala hili limekuwa changamoto kubwa kwa wanafunzi. Mimi ni mwanachama wa CHADEMA na siipendi CCM, sasa ninapotaka kuwatumikia wanafunzi wenzangu, kwa nini kigezo kiwe CCM? Ni upuuzi wa aina gani huu?

TAKUKURU wako wapi, wanalijua hili?
Suala hili halipaswi kuishia kwenye malalamiko ya wanafunzi. Kama kuna kanuni inayoruhusu jambo hili, wanafunzi wanastahili kuonyeshwa kanuni hiyo wazi. Na kama hakuna kanuni inayoweka sharti la uanachama wa chama fulani, basi ni muhimu mamlaka husika kuchunguza kwa nini sharti hilo linatumika.

Naomba JamiiForums na wadau wenye uelewa wa sheria na mifumo ya Serikali za Wanafunzi nchini Tanzania kusaidia kuweka jambo hili wazi.

Je, uanachama wa CCM/UVCCM ni sharti rasmi la kugombea nafasi za juu katika Serikali za Wanafunzi vyuoni Tanzania? Kama ndiyo, msingi wake wa kisheria ni upi?
 
Back
Top Bottom