Kuna uhusiano gani kati ya vazi la DERA(ke) na jezi(me) na Uswazi?

Kuna uhusiano gani kati ya vazi la DERA(ke) na jezi(me) na Uswazi?

Dera inavaliwa sio uswazi tu, ni vazi rahisi kwa wanawake haswa tusopenda kufunga khanga. Unakuwa comfortable na shughuli zako, alafu dera nyingi ni cotton hivyo haisumbui na joto.
 
jezi haipauki haraka tofauti na mashati au tshirt kwa hio inasave kununua nguo kila wakati...mtu anakuvalia jezi chini track Siku imeisha....!!Uswazi hatu-complicate maisha..simpo yani na Siku inasonga!!
 
Niliwahi kumuuliza mdada mmoja hivi akanijibu, Dera ni rahisi kulivaa, unalitupia tu unaendelea na mambo yako
 
Nilikuwa naapita mitaaa ya uzwazi ya hapa Jijini.. Manzese na Magomeni. Ukikutana na wanawake 10.. lazima tisa wamevaa vazi la dera.. Ukikutana na vijana 10 lazima 9 wamezaa tshirt za timu(simba,yanga, madrid,Arsenal, Manchester etc)
Bado najiuliza kuna uhusiano gani ya haya mavazi na uswahilini?
Wamevaa kujistiri
 
Masikini wengi wanavaa hizo nguo kwa vile ni bei rahisi sana , hizo jezi wanazovaa hakuna original hata moja , zote famba ! kuvaa jezi ya simba au yanga kwa sehemu kubwa kunaakisi uwezo mdogo wa mtu kichwani .
Aisee....kuvaa jezi za simba na yanga kunaakisi nini? Haya maneno uyaseme humu humu JF.
 
Huko uzunguni kwenu hamvai jezi au madera? Misiba kibao si ya uzunguni wala uswahili wamama wanashona sare madera.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Nimejisikia kucheka tu, sijui kwanini[emoji4]
 
Back
Top Bottom