Kuna uhusiano gani kati ya vazi la DERA(ke) na jezi(me) na Uswazi?

Kuna uhusiano gani kati ya vazi la DERA(ke) na jezi(me) na Uswazi?

Nilikuwa naapita mitaaa ya uzwazi ya hapa Jijini.. Manzese na Magomeni. Ukikutana na wanawake 10.. lazima tisa wamevaa vazi la dera.. Ukikutana na vijana 10 lazima 9 wamezaa tshirt za timu(simba,yanga, madrid,Arsenal, Manchester etc)
Bado najiuliza kuna uhusiano gani ya haya mavazi na uswahilini?
Joto nazani linafanya watu wavae nguo nyepesi kama hizo, hata mm nikiwa Dar miezi ya 11,12,01,02 napenda kuvaa pensi na jezi siku za wkend
 
Masikini wengi wanavaa hizo nguo kwa vile ni bei rahisi sana , hizo jezi wanazovaa hakuna original hata moja , zote famba ! kuvaa jezi ya simba au yanga kwa sehemu kubwa kunaakisi uwezo mdogo wa mtu kichwani .
Tatizo lako unazani maskini ndo wavaa jezi, Mimi wkend lazima nitupie Jezi ya Madrid OG dola 80, ninazo 3 za msimu huu, acha kukariri maisha hayako hivyo, hafu mm najamaa zangu wengi sana hata wakiwa makwao wanatupia jezi labda mtu kama anamtoko wa kwenda kusalimia ndugu au anaenda kazini au kwenye kikao
 
Materials za dera na jezi ni polyester aka "kauka nikuvae",haiitaji pasi,ndio maana zinapendwa uswazi.
BTW, they are very cheap as compared to nguo za cotton.
 
Ulitaka wavae nguo gani?
wanawake wenyewe wana mizigo balaa.acha wavae madera watustiri na mifadhaiko.
Dar RAHA.
 
Huku kwetu vijijini hatuvaagi madera bali tunafunga kanga na vitenge[emoji23]
Kweli kabisa.. lkn hata hapa mjini kabla ya madera ilikuwa ni mwendo wa kijifunga khanga na vitenge.. ila sasa imepungua sna
 
Kingine ni aina ya kazi wanazofanya. Uswazi wanafanya kazi siyo rasmi na wengi wamejiajiri. Wanavaa watakavyo/casual. Huko kwa mamiddle class utahitajika tu uwe na mashati/blauzi suruali au sketi nyingi sababu ya aina ya kazi.
 
Back
Top Bottom