Kuna uhusiano gani kati ya vazi la DERA(ke) na jezi(me) na Uswazi?

Dera inavaliwa sio uswazi tu, ni vazi rahisi kwa wanawake haswa tusopenda kufunga khanga. Unakuwa comfortable na shughuli zako, alafu dera nyingi ni cotton hivyo haisumbui na joto.
 
jezi haipauki haraka tofauti na mashati au tshirt kwa hio inasave kununua nguo kila wakati...mtu anakuvalia jezi chini track Siku imeisha....!!Uswazi hatu-complicate maisha..simpo yani na Siku inasonga!!
 
Niliwahi kumuuliza mdada mmoja hivi akanijibu, Dera ni rahisi kulivaa, unalitupia tu unaendelea na mambo yako
 
Wamevaa kujistiri
 
Ushuan ngumu sana kuona mtu kavaa dela
Kote wanavaa madera tofauti ni kuwa huku kwetu uswazi watu full time wako kibarazani au wanapuyanga mtaani ndio maana unaona madera mengi na huko ushuani kwenu watu muda mwingi wako magetini akitoka kaingia kwenye gari na dera lake.
 
Masikini wengi wanavaa hizo nguo kwa vile ni bei rahisi sana , hizo jezi wanazovaa hakuna original hata moja , zote famba ! kuvaa jezi ya simba au yanga kwa sehemu kubwa kunaakisi uwezo mdogo wa mtu kichwani .
Aisee....kuvaa jezi za simba na yanga kunaakisi nini? Haya maneno uyaseme humu humu JF.
 
Huko uzunguni kwenu hamvai jezi au madera? Misiba kibao si ya uzunguni wala uswahili wamama wanashona sare madera.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Nimejisikia kucheka tu, sijui kwanini[emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…