Ukiona gari zinatofautina engine kiasi hicho, most likely hiyo ya cc 1900 itakuwa ni ya Petrol na hiyo ya cc2700 itakuwa ni ya Diesel. Diesel ni ngumu kuwaka na haitoi moto mkali kama wa Petrol, so engine inabidi iwe kubwa ili kuweza kupata moto mkubwa wa kuzungusha engine.
Pia gari ya Diesel inaweza kuwa na engine kubwa isiyo na nguvu nyingi lakini ikawa na towing capacity kubwa, yani uwezo wa kubeba mizigo au kuvuta tela. Ndio maana gari ya diesel yenye engine kubwa unaweza ukaondokea gia namba mbili wakati gari ya petrol inakuhitaji uondokee na gear namba moja.
Gari ya Petrol inakula mafuta mengi kwa kuwa mafuta yote yanayoenda huchomwa. Nasikia gari ya diesel huwa inarudisha mafuta ili yaunguzwe raundi nyingine, sina uhakika na hili. Ngoja wataalam zaidi waje.