Kuna uhusiano gani wa CC za gari na ulaji mafuta?

Kuna uhusiano gani wa CC za gari na ulaji mafuta?

Ukiona gari zinatofautina engine kiasi hicho, most likely hiyo ya cc 1900 itakuwa ni ya Petrol na hiyo ya cc2700 itakuwa ni ya Diesel. Diesel ni ngumu kuwaka na haitoi moto mkali kama wa Petrol, so engine inabidi iwe kubwa ili kuweza kupata moto mkubwa wa kuzungusha engine.

Pia gari ya Diesel inaweza kuwa na engine kubwa isiyo na nguvu nyingi lakini ikawa na towing capacity kubwa, yani uwezo wa kubeba mizigo au kuvuta tela. Ndio maana gari ya diesel yenye engine kubwa unaweza ukaondokea gia namba mbili wakati gari ya petrol inakuhitaji uondokee na gear namba moja.

Gari ya Petrol inakula mafuta mengi kwa kuwa mafuta yote yanayoenda huchomwa. Nasikia gari ya diesel huwa inarudisha mafuta ili yaunguzwe raundi nyingine, sina uhakika na hili. Ngoja wataalam zaidi waje.
Gari ya diesel in return pipe ambayo hurudisha mafuta ya ziada ambayo hayakuingia kwenye combustion chamber lkn hili wataalam wanaweza wakaliweka vizuri zaidi
 
Mkuu ungefafanua technically kabisa ili tuelewe.
Hata mimi mwanzo nilikuwa sijui maana ya cc mpaka nilipokuja kusoma kwenye mtandao. Na baada ya kusoma sijaweza kurelate cc na ulaji wa mafta maana cc maana yake kumbe ni cubic centimetre na inapimwa kuanzia pale piston inapokuwa imecmama (dead) mpaka inapo rotate hadi mwisho.
Kwa mantiki hiyo ningependa mtu anielezee kuna uhusiano gani na utumiaji wa mafta
Labda gari ikiwa na cc kubwa kiwango cha mafuta kinachoingia kwenye cylinder ili kunguzwa ni kikubwa kuliko ya kile cha gari yeye cc ndogo. MF cc kubwa inachukua kijiko cha chakula cha mafuta kwa muunguzo mmoja kwa cylinder lkn cc ndogo inachukua nusu kijiko cha chai kwa muunguzo mmoja kwa cylinder, huo ni muono wangu wa kawaida tu.
 
huwez sema exactly engine ya cc 1000 itakuwa mafuta kiac gan kwa km flan ni mpaka injin iwekwe kwa gar ndo wafany test then watoe majib . mfano injin za toyota unakuta moja imetumika kwa magar kadhaa tofaut ambayo ni kimaumbo uzito pia application ya gar husika hvy utakuta fuel consumption ni tofaut wakat injin ni lile lile imetumika kwa magar mawil tofauti.
 
na co kwel kuwa gar ya cc 2000 ikifungwa turbo inafikia ya 2500 icyo na turbo inategemea na hyo turbo inaongeza asilimia ngap ya orijino power magar ya kawaida huwa turbo inaongeza 30_40% kwa injin some high perfomanc car zna turbo boosting up to 100% au zaid
 
Gari kuwa na cc kubwa au ndogo hakuna uhusiano na aina ya mafuta inayotumia moja kwa moja bali design ya mzigo ambao engine itakuwa inabeba. CC maana yake ni Cubic Centimeter yaani ni ukubwa au volume ya cylinders ambamo ndimo mchanganyiko wa mafuta na hewa huchomwa. sasa kama gari ina cc kubwa itakuwa inatumia mafuta mengi kwa sababu ya ukubwa wa cylinder. sasa cc inapatikanaje?

Kwenye gari kuna kitu kinaitwa
bore na stroke. ambapo bore ni kipenyo cha cylinder na stroke ni umbali ambao piston inatumia kusafiri juu hadi chini ya cylinder yaani kwa kitaalam Top dead center hadi bottom dead center. Sasa ili kupata cc ya engine ya gari yako unachukua volume ya one cylinder unazidisha na idadi ya cylinder yaani area of bore x stroke x number of cylinder kama gari yako ina piston 4 au 6 then unazidisha ila uhakikishe units ziko kwenye centimeter hapo utapata cc.

Kuhusu gari ya Petrol na Diese ni kweli diesel ni economical kwani hutumika kidogo kuliko petrol ingawa mfumo wa kisasa wa petrol engines umeboreshwa kufanana na ule wa diesel yaani kutumia nozzel ku inject mafuta kwenye cylinder tofauti na carburettor hapo zamani. Hii ni topic ndefu nitaanzisha uzi kuelezea kwa kirefu tofauti ya Diesel na Petrol Engines.
Nimesoma maelezo yako vizuri sana. Asante kwa ufafanuzi.

Naomba nijuze.. ivi mafuta ya Petrol yanayouzwa kwenye vituo vya kuuzia mafuta zinatofautiana??..

Mfano: baadhi ya vituo unakuta petrol hii ni "unleaded"

Kwenye kituo kingine utakuta Petrol ni "super"

Wengine utakuta ni " Premium"

Tofauti na Diesel huwa naona ni diesel tu.

Je hizi ni brand name tu au huwa zinatofautiana ubora.

Kama kuna utofauti wa ubora. Ipi ipo recomended, kwa uzoefu wako.

Thank you in advance.
 
Mkuu inawezekana mengine uliyoyasema ni sahihi lakini ili la kusema gari ikiwa na Cc kubwa ni ya diesel sio kweli. Kuna magari ya diesel yana cc 2,700 na wakati huo kuna magari ya petrol yana cc 4,700, mfano VX V8. Hapo sijui unasemaje.

Tiba
Yeah na kuna brevis pia 2500/3000cc ni petrol
 
Kama ni sensors za Fuel system na au ignition system kuna uhusiano mkubwa sana mkuu.
Mkuu kama sensors za fuel au ignition system zina tatizo utajuaje? Je mafundi wa mtaani wanaweza jua hili?kwasababu gari yangu imeongeza matumizi ya mafuta na fundi wangu naona kama imeshamshinda.
 
Nimesoma maelezo yako vizuri sana. Asante kwa ufafanuzi.

Naomba nijuze.. ivi mafuta ya Petrol yanayouzwa kwenye vituo vya kuuzia mafuta zinatofautiana??..

Mfano: baadhi ya vituo unakuta petrol hii ni "unleaded"

Kwenye kituo kingine utakuta Petrol ni "super"

Wengine utakuta ni " Premium"

Tofauti na Diesel huwa naona ni diesel tu.

Je hizi ni brand name tu au huwa zinatofautiana ubora.

Kama kuna utofauti wa ubora. Ipi ipo recomended, kwa uzoefu wako.

Thank you in advance.
Mkuu @prondo njoo utoe jibu hapa
 
Ni sawa na kulinganisha miili hasa vitambi, mwenye kubwa lazima ale sana kuliko mwembamba
 
CC ni cubic centimeters
Yaani total volume ambayo piston inasweep wakati inanyonya na kucompress mafuta
Kutoka BOTTOM DEAD CENTRE(BDC) Mpaka TOP DEAD CENTRE (TDC)
Yaani jumla ya ujazo (eneo la wazi) ya cylinder zote, ujazo ukiwa mkubwa inamaana volume ya mafuta pia yanayonyonywa SUNCTION itakuwa kubwa,
Nguvu ya engine inategemea UWINGI WA MAFUTA YANAYOKUWA COMPRESSED na CALORIFIC VALUE YA MAFUTA HUSIKA
kumbe
Power= total volume(fuel)*calorific value ya fuel
Hitimisho CC ikiwa kubwa engine inakula mafuta mengi,ila power ya engine haitegemei uwingi wa mafuta tu ,inategemea ni mafuta aina gani na yana calorific value ngap(ENERGY CONTENT)
 
Maelezo yako ni mazuri sana,sasa hebu fafanua pale unapokuta gari kama Ipsum new model cc2400 engine vvti inakuaje inakwenda almost sawa na gari ya cc 1500 yaani 1liter inagonga mpaka 13km.
Jibu ni rahisi
Kuna uwezekano mkubwa gari yenye Engine ndogo kula mafuta mengi ukilinganisha na yenye Engine kubwa na sababu ni hizi
1. Gari inakula mafuta mengi unapotembelea gia kubwa yaani Nr .1
2. Kwahiyo gari ndogo pahala unapotembelea gia Nr 1 au Nr 2 kwa gari yenye Engine kubwa unatembelea gia Nr 4 au tano.
3. Ngari yenye Engine ndogo inabidi wakati mwingi ukanyage mafuta mpaka mwisho wakati Engine kubwa ukikanyaga kidogo unapata mwendo unaouhitaji
4. Mambo mengine yanayochangia ulaji wa Mafuta Aina ya Matairi, Upepo katika matairi, Barabara (mzuri au mbovu)
Kasi ya Upepo, Kufungua kioo pia kunachagia ulaji wa Mafuta, Mkato wa gari (yaani gari yenye kioo cha Flat kama Defender itakula mafuta mengi kulikoni yenge round Glasses
Ziko Fakto nyingi
 
Ufafanuzi mzuri.
 
Ukiona gari zinatofautina engine kiasi hicho, most likely hiyo ya cc 1900 itakuwa ni ya Petrol na hiyo ya cc2700 itakuwa ni ya Diesel. Diesel ni ngumu kuwaka na haitoi moto mkali kama wa Petrol, so engine inabidi iwe kubwa ili kuweza kupata moto mkubwa wa kuzungusha engine.

Pia gari ya Diesel inaweza kuwa na engine kubwa isiyo na nguvu nyingi lakini ikawa na towing capacity kubwa, yani uwezo wa kubeba mizigo au kuvuta tela. Ndio maana gari ya diesel yenye engine kubwa unaweza ukaondokea gia namba mbili wakati gari ya petrol inakuhitaji uondokee na gear namba moja.

Gari ya Petrol inakula mafuta mengi kwa kuwa mafuta yote yanayoenda huchomwa. Nasikia gari ya diesel huwa inarudisha mafuta ili yaunguzwe raundi nyingine, sina uhakika na hili. Ngoja wataalam zaidi waje.
ni ukweli petrol ikichomwa inakuwa imechomwa ila diesel ikichomwa inarud tena
 
ni ukweli petrol ikichomwa inakuwa imechomwa ila diesel ikichomwa inarud tena
Petrol na diesel yote ni mafuta ila wakati wa uchomwaji baadhi hurudishwa kwenye tank na kwani sio mafuta yote uchomwa kwa wakati mmoja mengine hubakia na kurudishwa kwenye tank, mfano mzuri ni toyota spacio ambapo gari hii utumia petrol, ukifungua mfuniko wa tank wakati iko sailensa utaona baadhi ya mafuta yanachuruzika kutoka kwa ndani kidogo ambapo kuna pipe yakurudisha mafuta na kuelekea kwenye tank
 
Jibu ni rahisi
Kuna uwezekano mkubwa gari yenye Engine ndogo kula mafuta mengi ukilinganisha na yenye Engine kubwa na sababu ni hizi
1. Gari inakula mafuta mengi unapotembelea gia kubwa yaani Nr .1
2. Kwahiyo gari ndogo pahala unapotembelea gia Nr 1 au Nr 2 kwa gari yenye Engine kubwa unatembelea gia Nr 4 au tano.
3. Ngari yenye Engine ndogo inabidi wakati mwingi ukanyage mafuta mpaka mwisho wakati Engine kubwa ukikanyaga kidogo unapata mwendo unaouhitaji
4. Mambo mengine yanayochangia ulaji wa Mafuta Aina ya Matairi, Upepo katika matairi, Barabara (mzuri au mbovu)
Kasi ya Upepo, Kufungua kioo pia kunachagia ulaji wa Mafuta, Mkato wa gari (yaani gari yenye kioo cha Flat kama Defender itakula mafuta mengi kulikoni yenge round Glasses
Ziko Fakto nyingi
hapo kwenye red, inakuwaje?
 
hapo kwenye red, inakuwaje?
Aina ya Matairi nilikusudia Profile ya Pira wenyewe (Umekakwa na Kashata kubwa kama mpira wa Offroad au ya kwaida tu)
Hio inaongeza au Kupunguza Friction kwenye Barabara
Mipira vile vile iana Klass zake na Speed zake Kwa Mfano:
F-Index 80 km/h
G-Index 90 km/h
J-Index 100 km/h
K-Index 110 km/h
L-Index 120km/h
M-Index 130km/h
N-Index 140 km/h
P-Index 150 km/h
Q-Index 160km/h
R-Index 170 km/h
S-Index 180 km/h
T-Index
T- 190 km/h
U-Index 200 km/h
 
power to weight ratio ..engine doesnt have to work harder

yu may find a car like IST with five psg kuna saa inakula mafuta mengi kuliko rav4 ya cc 2000 ni kwa sababu ya hcho kitu power to weight ratio mliman injin ndogo inafanya kazi kubwa ku maintain spid flan hivo rpm inakuwa juu mafuta yanaeza kwenda mengi sana
 
Hizo gari zenye engine za kisasa zote km VVTI, D4-D, GDI n.k zina mfumo mzuri wa ulaji wa mafuta ambao ni electronic contlolled na hata kama ni petrol inatumia nozel na Petrol,air mixture inafanyika kwa ku optimize air ratio zaid kwenye combustion chamber tofauti na zile za zamani ambapo ilikuwa kwa Petrol mchanganyiko huo unafanyika ndani ya cylinder theni unakuwa ignited na spark plug.

nitatoa tofauti moja kuu ya Diesel na Petrol engines nayo ni Ignition point. kwa waliosoma Chemistry watakuwa wanajua hii kitu. sasa Deisel fuel ina low iginition point ndio maana engines zake huwa hewa inaingia kwenye cylinder then inakuwa compressed halafu inakuwa ignited na Diesel fuel moja kwa moja wakati Petrol Engine Petrol and air has to be mixed at a certain proportion then compressed before being ignited by the sparking plug. Hii inafanya Diesel kutumika kidogo kuliko Petrol

Sasa maboresho yaliyofanyika ni pamoja na kufanya mchanganyo uwe bora zaidi yaani premix kwa kuwa elecronic controlled with nozzels and sensors inside the manifold.

ndio maana kwa mafundi wetu tulionao wengi hawajajiendeleza na teknolojia hii ya kisasa badoa wako na zile za zamani gari hizi zinakuwa tabu kwao kutengeneza.
VVTI ni ya zaman kidogo mpya.ni hizi D4 au D4D kwa upande wa toyota GDI kwa mitsubishi na TDI kwa audi na bmw
 
Back
Top Bottom