Kuna uhusiano mkubwa kati ya muonekano/unadhifu na Kupendelewa

Kuna uhusiano mkubwa kati ya muonekano/unadhifu na Kupendelewa

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Unadhifu wa kimavazi, kiakili na kimaneno (lugha) unauhusiano mkubwa sana na kupendelewa au kupewa kipaumbele kwenye jamii.

Watoto waliovaa vizuri na wasafi hata kwenye bus au hospitalini kila mtu anataka kuwa karibu nao.

Ukiwa katika safari za vijijini makonda na wapiga debe wanapata taabu kukutafutia siti nzuri. Kama ni kijana mtanashati basi mwenye gari bovu atajitahidi akuweke karibu na abilia wa kike msafimsafi.

Kama ni kwenye nyumba za sala, ukiwa mgeni ni rahisi kuwekwa kwenye meza za wakuu.

Ukiuliza kitu kila mtu anatamani akusaidie ukipate.

Umaridadi wa lugha na maneno ya maana utafanya usikilizwe na wakuu.

Kuna mdau wangu mmoja anasisitiza ukiwa na appointment na watu wa maana wenye influence jitahidi uvae vizuri maana hata kabla hujaongea watu wameshakushusha kwa muonekano wako.

Vijana msifikiri interview ndio sehemu ya kupendeza, kuna interview nyingine za kushtukiza ambazo unapimwa bila kujijua.

Ni hayo tu.

Mtumishi
Matunduizi.
 
Back
Top Bottom