Kuna uhusiano wa kuota ndoto mbaya ukilalia mgongo (Chali)?

Jerrymsigwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
14,084
Reaction score
8,384
Hili tatizo sijui ni langu tu ama tuko wengi. Nikilala chali ama kwa ubavu wa kushoto naota sana ndoto mbaya, nakabwa ama nalimishwa hata nisali kabla ya kulala ama niweke biblia kama hirizi chini ya pillow. Na hizi ndoto hata wakati wa mchana huwa mda mwingine zinakuja.

Je kuna uhusiano gani wa ndoto na posture ya kulala? na hii kitu inaitwa majinamizi ni vvitu gani?

Kuna tatizo ninapolala kwa kuelekeza macho juu, huwa naandamwa na mauza uza na kuota ndoto za ajabu. Hili laweza kuwa tatizo?

===Majibu kutoka kwa WanaJF===



 
wengine wanasema ukila ugali usiku ndio unaota vby, mi naona sio sababu kabisa maana ukiwa na njaa ndio ndoto mbaya zaidi
 

Hebu jaribu kubadilisha!
Badala ya biblia weka quraan! Huenda mambo yakageuka! Kujaribu sio dhambi!
 
Last edited by a moderator:
wengine wanasema ukila ugali usiku ndio unaota vby, mi naona sio sababu kabisa maana ukiwa na njaa ndio ndoto mbaya zaidi

Yaani mwana wane hapo umenchekesha mno!
Babu yangu amekula ugali usiku mwaka wa 60 leo! Hata siku moja hajaota ndoto mbaya!
Hayo ni maneno ya wala chips.
 
Afya mgogoro tu. Unafanya mazoezi? Una uzito mkubwa? Punguza 10% tu ya uzito wako then utaona.

umewahi lala chale usiku mzima ndugu? ebu jaribu leo uone

niko sawa kabisa, urefu vs uzito viko sawa,mazoezi ni moderate I like cycling na ndio usafiri wangu kwenda na kurudi kazini
 
Yaani mwana wane hapo umenchekesha mno!
Babu yangu amekula ugali usiku mwaka wa 60 leo! Hata siku moja hajaota ndoto mbaya!
Hayo ni maneno ya wala chips.

Unacheka tatizo? nilisikia kwa yule jamaa anaitwa Ndodi, unamkumbuka? ila kwangu sijala ugali na bado mda mwingine naota ndoto mbaya
 
Hapana, sina tabia ya kulala chali. By the way hata mie afya yangu mgogoro, nna mwili wa kiswahili ni balaa!

Wasiwasi mwingine ni kwenye moyo. Umeshawahi kuchekiwa kama moyo wako uko sawa kabisa? Kama bado jaribu kucheki.
umewahi lala chale usiku mzima ndugu? ebu jaribu leo uone

niko sawa kabisa, urefu vs uzito viko sawa,mazoezi ni moderate I like cycling na ndio usafiri wangu kwenda na kurudi kazini
 
Dhana ya kula ugali usiku inaweza kuwa na maana ya kuwa usile ukashiba mno kabla ya kulala. Unajua unapokula, activity nyingi za mwili zinazimwa ili nguvu ikatumike kusaga misosi. Minimum energy inaachwa kuendesha ubongo ili upumue na kuendesha moyo. Sasa unaposhindilia na especially ukila late inaweza kuleta strain kwenye mgawanyiko. Unashauriwa kula a light meal kabla ya saa moja usiku.
Unacheka tatizo? nilisikia kwa yule jamaa anaitwa Ndodi, unamkumbuka? ila kwangu sijala ugali na bado mda mwingine naota ndoto mbaya
 
Ninayo ya kiswahili, hivi ya kiswahili ina nguvu sawa na ile original ya kiarabu?

Sina hakika! Lkn nadhani tafsiri sio sawa na maandiko ya asili!
Manake tafsiri inaweza kukosewa!
Mi nashauri ujaribu original.
Ni kujaribu tu! Huwezi jua huenda ndio ikakomesha!
 
Hapana, sina tabia ya kulala chali. By the way hata mie afya yangu mgogoro, nna mwili wa kiswahili ni balaa!

Wasiwasi mwingine ni kwenye moyo. Umeshawahi kuchekiwa kama moyo wako uko sawa kabisa? Kama bado jaribu kucheki.

Sasa we sister unataka mwenzako asilale kabisaaaa!
Moyo tena! Bora ungeanzia mbali kidogo!
 

100% nakubaliana nawe, thanks alot king'ast
 
Last edited by a moderator:
Unacheka tatizo? nilisikia kwa yule jamaa anaitwa Ndodi, unamkumbuka? ila kwangu sijala ugali na bado mda mwingine naota ndoto mbaya

Mkuu kulala chali kunahusiana pia na ndoto mbaya!
Ni chemical reactions inayotokana na blood flow kwenye ubongo!
Kwa hiyo mi nakushauri ulalie ubavu wa kulia na weka quraan chini ya mto! Na km unao ugali pia kula tu!
Halafu utanipa majibu!
 
Sina hakika! Lkn nadhani tafsiri sio sawa na maandiko ya asili!
Manake tafsiri inaweza kukosewa!
Mi nashauri ujaribu original.
Ni kujaribu tu! Huwezi jua huenda ndio ikakomesha!

Duh, kama hazina "integrity" sawa mbona mie nimenunua msikiti wa hapa pasiansi na nikaambiwa ni lugha tu? Haya asante ila sina hakika na utofauti wa hivyo vitabu
 


Ndoto za kutisha (nightmare).
Zinasababishwa na shibe (kushiba sana), na ulalaji mbaya (chali)...!

Hali hii usababishwa na kugusana kwa diaphragm na abdominal, na hii kupelekea uvutaji wa pumzi kuwa wa shida... Na meseji inayopokewa kwenye ubongo wako ni picha mbaya ya kutisha (kukabwa).

Unaweza kumuona mtu aliyelala akiangaika uku na kule, unachopaswa ni kumtikisa polepole na kumuita jina lake ili ahamke... Upaswi kumshtua kwa sauti mtu aliye kwenye hali hii, unaweza kumsababishia madhara mengine makubwa, kama vile mshtuko wa moyo.@
Jerrymsigwa


KUKABWA NA JINAMIZI NINI MAANAA YAKE?

Kukabwa na Jinamizi katika ndoto kama tunavyoita ni kitendo ambacho kinawatokea watu wengi sana.

Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama "Mwili kupooza katika usingizi" (Sleeping Paralysis)

Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10.
Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho.

Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa khofu kwa muda fulani.

Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi,

Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu wala mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa kama uliyepata

"ugonjwa wa Kupooza".

Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani chumbani kwako, wengine wanaona kama wanatekwa nyara au kuchukuliwa, wengine wanahisi wanabakwa, wengine wanaona wakipigwa au kukimbizwa na matukio mbali mbali ya kutisha.

Kukabwa na Jinamizi kama tunavyoiita kunatokana na sababu nyingi, ya kwanza kabisa ni jinsi wewe mwenyewe ulivyolala, mara nyingi unapolala chali mambo hayo yanakutokea, au ukiwa na jambo linalokusumbua kimaisha ambalo huwezi kulitatua linaweza kukuletea kukabwa na Jinamizi.

Sababu nyingine ni mazingira unayoishi au eneo ulilopo kama kuna makelele, au chumba kisicho na hewa ya kutosha au kuwa na mawazo kuhusu jambo fulani, au kulala na njaa au ukiwa umelala umekasirika au ndoto unazoota.

Njia ya kwanza ya kupambana na tatizo hili ni kujaribu sana lisikutokee, unatakiwa ujaribu kujua kitu gani kinakusababashia wewe kupata matatizo hayo, mfano ukijua kwamba kila ukilala chali unakabwa basi badilisha ulalaji wako, lala upande au lalia tumbo.

Ikiwa unakabwa ukiwa umelala usiku sana, au umefanya kazi ngumu, Jaribu kubadili muda wako wa kulala au punguza kufanya kazi mpaka ukachoka.
Njia nyingine ni kuhakikisha unapata muda mrefu wa kulala na umepunzika kabla ya usingizi haujakuja.


NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA NA JINAMIZI

1.Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndio unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.

2.Jiepushe kulala chali.

3.Punguza mawazo mengi.

4.Lala katika muda mzuri na jaribu kupata muda mrefu wa usingizi masaa 8 mpaka 10.

5.Jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni saa 3 basi iwe muda huo wakati wote.

6.Jaribu kula vizuri kabla hujalala.

7.Kumbuka kwamba pamoja ya kuwa hali hii inatisha lakini haina hatari yoyote.

8.Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha, hali ya kukabwa itakwisha.

9.Ukiona kama unataka kukabwa amka kaa chini kwa dakika 5 halafu lala tena. Usikose kunipa Feedback. Chanzo. MziziMkavu.
 
Punguza kuangalia MOVIES za mazombie,Vampire na nyingine za muundo huo!
 

Inategemea pia na shghuli unayo ifanya usiku! Kama ni heavy duty! Inabidi ule ushibe!
We hujaskia kale ka msemo kanako sema "kumridhisha mama watoto lazima ule ushibe"
Kwi kwi kwi kwi kwi!

Hasa kwa sisi wasukuma! Ile milo light inaweza kukutoa knock out!
 

Biblia kama biblia haiwezi kuzuia nguvu za pepo wachafu ila imani ya biblia kwamba ni kitabu kitakatifu ndio inayowafukuza pepo na kutokukusumbua kabisa...Jamaa yangu umesema unatumia biblia kama hirizi kweeeeeeeeeeeli jamaa yangu unamfananisha mungu na shetani kwa kweli hutopata mafanikio....Ni bora kuwa baridi au moto na sio vuguvugu kwa kuwa mungu wetu ana wivu na hapendi kuchanganywa.....Sijui mstari gani ila ni barua ya mtume paulo kwa Wakorintho. Mwombe mungu akujengee imani ya kusadiki kwamba yeye ndie mlinzi wa maisha yako na amini utakuwa salama tangu sasa...vyote unavyoviona ni vitisho vya shetani vyenye lengo la kukunyima amani kama ulivyo sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…