Kuna uhusiano wa kuota ndoto mbaya ukilalia mgongo (Chali)?

Kuna uhusiano wa kuota ndoto mbaya ukilalia mgongo (Chali)?

Hili tatizo sijui ni langu tu ama tuko wengi. Nikilala chali ama kwa ubavu wa kushoto naota sana ndoto mbaya, nakabwa ama nalimishwa hata nisali kabla ya kulala ama niweke biblia kama hirizi chini ya pillow. Na hizi ndoto hata wakati wa mchana huwa mda mwingine zinakuja.

Je kuna uhusiano gani wa ndoto na posture ya kulala? na hii kitu inaitwa majinamizi ni vvitu gani?
BUBUji MziziMkavu

nenda kaombewe
 
Swala sio kulala na biblia au msaafu. Kumbuka hata hao wanaokukaba wanaenda kanisani au msikitini. Usalama wako upo katika kuwa na moyo Safi ili ulinzi wa Mungu uwe kwako, otherwise utakabwa hadi ujikute upo kuzimu
 
Hili tatizo sijui ni langu tu ama tuko wengi. Nikilala chali ama kwa ubavu wa kushoto naota sana ndoto mbaya, nakabwa ama nalimishwa hata nisali kabla ya kulala ama niweke biblia kama hirizi chini ya pillow. Na hizi ndoto hata wakati wa mchana huwa mda mwingine zinakuja.

Je kuna uhusiano gani wa ndoto na posture ya kulala? na hii kitu inaitwa majinamizi ni vvitu gani?
BUBUji MziziMkavu

Anza maombi.
 
Anza maombi.

Mnaosema kuhusu maombi yani mngejua naomba sanaaa huenda hata kuliko ninyi mnaoandika.

Wewe jaribu tu kulala chali leo usiku uone! I think kuna ishu ya brain positioning wkt wa kulala...am not sure
 
Nikaombewe na nani? Ukiugua malaria unaombewa? Shida nahisi itakuwa ni ishu ya position ya kichwa.

Ebu jaribu kulala chali leo usiku

sasa kama ishu ni position ya kichwa unaomba ushauri wa nini si ubadilishe position ya kichwa?mbona mi hata nikilala chali au hata nilale vipi sikabwi?
 
Ndoto za kutisha (nightmare).
Zinasababishwa na shibe (kushiba sana), na ulalaji mbaya (chali)...!

Hali hii usababishwa na kugusana kwa diaphragm na abdominal, na hii kupelekea uvutaji wa pumzi kuwa wa shida... Na meseji inayopokewa kwenye ubongo wako ni picha mbaya ya kutisha (kukabwa).

Unaweza kumuona mtu aliyelala akiangaika uku na kule, unachopaswa ni kumtikisa polepole na kumuita jina lake ili ahamke... Upaswi kumshtua kwa sauti mtu aliye kwenye hali hii, unaweza kumsababishia madhara mengine makubwa, kama vile mshtuko wa moyo.@
Jerrymsigwa

553432_425604320825811_1687825358_n.jpg

KUKABWA NA JINAMIZI NINI MAANAA YAKE?

Kukabwa na Jinamizi katika ndoto kama tunavyoita ni kitendo ambacho kinawatokea watu wengi sana.

Watu wengi hufikiri kwamba anayewakaba ni Jini lakini Tendo hilo kwa kitaalamu linajulikana kama “Mwili kupooza katika usingizi” (Sleeping Paralysis)

Tendo hilo huwa linakutokea katika muda wa sekunde 20 lakini wewe unayehusika utahisi kama dakika 5 au dakika 10.
Matukio hayo ya kijinamizi yanatofautiana na yanakutokea wakati ukiwa nusu usingizini na nusu macho.

Ukweli ni kwamba hayana madhara yoyote, ila yanakupa khofu kwa muda fulani.

Unapokabwa unakuwa na fahamu nusu. Unaweza kufungua macho, na utahisi kupiga kelele lakini watu hawakusikii, Mwili wako unakuwa hauwezi kufanya lolote na viungo vya mwili wako vinakuwa havifanyi kazi,

Inapokutokea unakuwa huwezi kunyanyua mguu wala mkono wala kichwa. Kwa ujumla unakuwa kama uliyepata

“ugonjwa wa Kupooza”.

Hali hii ya kukabwa inapotokea unaweza ukamuona mtu anayetisha akiingia ndani chumbani kwako, wengine wanaona kama wanatekwa nyara au kuchukuliwa, wengine wanahisi wanabakwa, wengine wanaona wakipigwa au kukimbizwa na matukio mbali mbali ya kutisha.

Kukabwa na Jinamizi kama tunavyoiita kunatokana na sababu nyingi, ya kwanza kabisa ni jinsi wewe mwenyewe ulivyolala, mara nyingi unapolala chali mambo hayo yanakutokea, au ukiwa na jambo linalokusumbua kimaisha ambalo huwezi kulitatua linaweza kukuletea kukabwa na Jinamizi.

Sababu nyingine ni mazingira unayoishi au eneo ulilopo kama kuna makelele, au chumba kisicho na hewa ya kutosha au kuwa na mawazo kuhusu jambo fulani, au kulala na njaa au ukiwa umelala umekasirika au ndoto unazoota.

Njia ya kwanza ya kupambana na tatizo hili ni kujaribu sana lisikutokee, unatakiwa ujaribu kujua kitu gani kinakusababashia wewe kupata matatizo hayo, mfano ukijua kwamba kila ukilala chali unakabwa basi badilisha ulalaji wako, lala upande au lalia tumbo.

Ikiwa unakabwa ukiwa umelala usiku sana, au umefanya kazi ngumu, Jaribu kubadili muda wako wa kulala au punguza kufanya kazi mpaka ukachoka.
Njia nyingine ni kuhakikisha unapata muda mrefu wa kulala na umepunzika kabla ya usingizi haujakuja.

NJIA ZA HARAKA ZA KUEPUKANA NA KUKABWA NA JINAMIZI

1.Ikikutokea hali hiyo jaribu kuvuta pumzi nyingi ndani kwa sababu pumzi peke yake ndio unayoweza kuidhibiti ukiwa umekabwa.

2.Jiepushe kulala chali.

3.Punguza mawazo mengi.

4.Lala katika muda mzuri na jaribu kupata muda mrefu wa usingizi masaa 8 mpaka 10.

5.Jaribu kuwa na muda maalum wa kulala ikiwa ni saa 3 basi iwe muda huo wakati wote.

6.Jaribu kula vizuri kabla hujalala.

7.Kumbuka kwamba pamoja ya kuwa hali hii inatisha lakini haina hatari yoyote.

8.Ukihisi unakabwa jaribu sana kujitingisha, hali ya kukabwa itakwisha.

9.Ukiona kama unataka kukabwa amka kaa chini kwa dakika 5 halafu lala tena. Usikose kunipa Feedback. Chanzo. MziziMkavu.
MziziMkavu nimependa utafit wako
 
Last edited by a moderator:
Biblia kama biblia haiwezi kuzuia nguvu za pepo wachafu ila imani ya biblia kwamba ni kitabu kitakatifu ndio inayowafukuza pepo na kutokukusumbua kabisa...Jamaa yangu umesema unatumia biblia kama hirizi kweeeeeeeeeeeli jamaa yangu unamfananisha mungu na shetani kwa kweli hutopata mafanikio....Ni bora kuwa baridi au moto na sio vuguvugu kwa kuwa mungu wetu ana wivu na hapendi kuchanganywa.....Sijui mstari gani ila ni barua ya mtume paulo kwa Wakorintho. Mwombe mungu akujengee imani ya kusadiki kwamba yeye ndie mlinzi wa maisha yako na amini utakuwa salama tangu sasa...vyote unavyoviona ni vitisho vya shetani vyenye lengo la kukunyima amani kama ulivyo sasa.
Mkuu Tamatheo Anachotakikana afuate ushauri wangu utamsaidia sio kuweka kitabu cha Biblia chini ya mto hakitoweza kufukuza ndoto za kukabwa.

MziziMkavu nimependa utafit wako
Mkuu Jerrymsigwa Umependa utafiti wangu basi hata kuniwekea (Like) Umeshindwa? Au ndio Big Deal kwako?
 
Hili tatizo sijui ni langu tu ama tuko wengi. Nikilala chali ama kwa ubavu wa kushoto naota sana ndoto mbaya, nakabwa ama nalimishwa hata nisali kabla ya kulala ama niweke biblia kama hirizi chini ya pillow. Na hizi ndoto hata wakati wa mchana huwa mda mwingine zinakuja.

Je kuna uhusiano gani wa ndoto na posture ya kulala? na hii kitu inaitwa majinamizi ni vvitu gani?
BUBUji MziziMkavu
nenda kaombewe unachezewa wewe!
 
Kijana iyo ni michezo ya waswahili tu,utahadithiwa sana ni-PM nikupe namba ya fundi akusaidie.
 
Mkuu Tamatheo Anachotakikana afuate ushauri wangu utamsaidia sio kuweka kitabu cha Biblia chini ya mto hakitoweza kufukuza ndoto za kukabwa.

Jamaa yangu Imani inajenga Saikolojia ya binadamu....wazo unalompa ni la kutumia nguvu za fikra za binadamu na wazo nililompa ni la kutumia ulimwengu wa roho...Hizi ni nguvu 2 zinazokinzana ila ukitaka kuwa ktk ulimwengu wa roho lazima uwe na Imani...Sijui kama umenielewa hadi hapa.
 
Wadau kwa wataalamu, ni kwanini watu wengi huoata ndoto mbaya wanapolala kwa mgongo/kichwa kuangalia juu.

Ukilala kwa mgongo, Kuna uwezekano mkubwa wa ulimi wako kurudi nyuma na kublock njia ya hewa. Hii inakifanya upumue kwa shida. Ubongo wako iko kama processor ya computer na inaendeshwa kwa oxygen kama nishati. Hewa ikipungua kwenye ubongo unaanza kupata maruweruwe. Pozi zuri la kulala Ni kwa Tumbo na shingo ikae upande Ili njia ya hewa iwe wazi. Ukilala chali ukaota ndoto nzuri ujue unakaribia kufa (sitanii hehehe google 'euphoria')

X-PASTER said:
Mara nyingi wanaopata ndoto za kutisha au kuhisi kukabwa wakiwa usingizini, ni matokeo ya mgandamizo wa nerves au wakati mwingine kunasababishwa na kushiba sana au kuvimbiwa.

Ulaji wa chakula kingi kabla ya kwenda kulala si mzuri, kwa sababu kunasababisha tumbo kukugasana na diaphragm, na hi upelekea mgandamizo kwenye mapafu na kusababisha kutoweza kupumua vizuri.

Hali hii inapotokea, ubongo unajaribu kutafuta au kutaka kujuwa nini tatizo ili kuweza kukupa taarifa au ufahamu wa kile kinachoendelea. Matokeo ni pale ubongo unaposhindwa kutafairi tatizo ndio ukuletea taarifa ambayo wewe unaiona kuwa kuna mtu au dubwana fulani linakukaba na ndoto zingine za kutisha.

Vilevile inaweza kuwa ni Paralysis, ambayo usababiswa kwa kuharibiwa kwa nervous system au mgandamizo mkubwa kwenye nervous wakati wa kulala, ushauri jaribu kutumia mto ambao si mgumu na kula chakula masaa mawili au matatu kabla ya kulala na chakula kiwe laini na usishibe sana kwa sababu itakusababishia mgandamizo kati ya tumbo na diaphragm na kupelekea kupata hayo mamtatizo.

Kabla ya kulala ni vema ukakoga maji ya uvuguvugu, hii usaidia nerves zako ku relax na kukupelekea kupata usingizi mzuri na unywaji wa maziwa ya moto kabla ya kulala, japo nusu saa kabla pia inasaidia kupata usingizi mzuri.

Ila kama tatizo ni kubwa ni bora kuonana na daktari ili kuweza kujuwa tatizo kwa undani zaidi.
 
Aisee hata mimi hua inanitokea sana tufahamishane wadau wenye utaalamu wa mambo hayo
 
Ukilala kwa mgongo, Kuna uwezekano mkubwa wa ulimi wako kurudi nyuma na kublock njia ya hewa. Hii inakifanya upumue kwa shida. Ubongo wako iko kama processor ya computer na inaendeshwa kwa oxygen kama nishati. Hewa ikipungua kwenye ubongo unaanza kupata maruweruwe. Pozi zuri la kulala Ni kwa Tumbo na shingo ikae upande Ili njia ya hewa iwe wazi. Ukilala chali ukaota ndoto nzuri ujue unakaribia kufa (sitanii hehehe google 'euphoria')
 
kwakweli hata mimi inanisumbua sana hata jana tu imenitokea kama jinamizi ndio wanaita, nikilala chali tu ninaota ndoto za kutisha.
 
Back
Top Bottom