Kuna uhusiano wa kuota ndoto mbaya ukilalia mgongo (Chali)?

Kuna uhusiano wa kuota ndoto mbaya ukilalia mgongo (Chali)?

Best position ya kulala inaitwa 'recovery position'. Hapo itakuokoa na mambo mengi sana aisee. Angalia picha (hii position inatumika kwenye kutoa huduma ya kwanza pia. Ukilala hivi hata kukoroma ni nadra sana)


Recovery Position.JPG
Dah... Basi mie nimezoea kulalia tumbo mpaka nahisi kero sometimes. Nisipolalia tumbo usingizi hauji, afu hata kama nikilala vipi mwisho wa siku nitajikuta nishageuka na kulalia tumbo. Kuna wakati nilidhani kulalia sana tumbo kuna athari kiafya kumbe sio kweli.. Asante kwa kunifungua
 
Mara nyingi wanaopata ndoto za kutisha au kuhisi kukabwa wakiwa usingizini, ni matokeo ya mgandamizo wa nerves au wakati mwingine kunasababishwa na kushiba sana au kuvimbiwa.

Ulaji wa chakula kingi kabla ya kwenda kulala si mzuri, kwa sababu kunasababisha tumbo kukugasana na diaphragm, na hi upelekea mgandamizo kwenye mapafu na kusababisha kutoweza kupumua vizuri.

Hali hii inapotokea, ubongo unajaribu kutafuta au kutaka kujuwa nini tatizo ili kuweza kukupa taarifa au ufahamu wa kile kinachoendelea. Matokeo ni pale ubongo unaposhindwa kutafairi tatizo ndio ukuletea taarifa ambayo wewe unaiona kuwa kuna mtu au dubwana fulani linakukaba na ndoto zingine za kutisha.

Vilevile inaweza kuwa ni Paralysis, ambayo usababiswa kwa kuharibiwa kwa nervous system au mgandamizo mkubwa kwenye nervous wakati wa kulala, ushauri jaribu kutumia mto ambao si mgumu na kula chakula masaa mawili au matatu kabla ya kulala na chakula kiwe laini na usishibe sana kwa sababu itakusababishia mgandamizo kati ya tumbo na diaphragm na kupelekea kupata hayo mamtatizo.

Kabla ya kulala ni vema ukakoga maji ya uvuguvugu, hii usaidia nerves zako ku relax na kukupelekea kupata usingizi mzuri na unywaji wa maziwa ya moto kabla ya kulala, japo nusu saa kabla pia inasaidia kupata usingizi mzuri.

Ila kama tatizo ni kubwa ni bora kuonana na daktari ili kuweza kujuwa tatizo kwa undani zaidi.

Reasonable Reason .

Nimependa maelezo yako . ! .

THANKS .
 
Labda kuna ukweli ndani yake, maana mimi kulala kwangu ni kulalia tumbo, na sikumbuki mara ya mwisho kuota ndoto mbaya ni lini, kwa kifupi ni muda sana toka niote ndoto mbaya! Pia cha kushangaza mimi siku hizi sioti kabisa, je ni tatizo au! Kwa mwenye maelezo kuhusu hili, Tafadhari.
 
Dah... Basi mie nimezoea kulalia tumbo mpaka nahisi kero sometimes. Nisipolalia tumbo usingizi hauji, afu hata kama nikilala vipi mwisho wa siku nitajikuta nishageuka na kulalia tumbo. Kuna wakati nilidhani kulalia sana tumbo kuna athari kiafya kumbe sio kweli.. Asante kwa kunifungua

Wewe ni kama mimi, siwezi lala chali na kupata usingizi.
 
Sidhani kama kuna ukweli wowote ndani yake!,Labda kama unalala chini ni Lazima tu utaota ndoto mbaya!
 
Kuna tatizo ninapolala kwa kuelekeza macho juu, huwa naandamwa na mauza uza na kuota ndoto za ajabu. Hili laweza kuwa tatizo?
 
Jinamizi (hali ya kukabwa ukiwa umelala usiku) husababishwa na nini? kuna uhusiano wowote na afya ya mwili?
 
Hili tatizo sijui ni langu tu ama tuko wengi. Nikilala chali ama kwa ubavu wa kushoto naota sana ndoto mbaya, nakabwa ama nalimishwa hata nisali kabla ya kulala ama niweke biblia kama hirizi chini ya pillow. Na hizi ndoto hata wakati wa mchana huwa mda mwingine zinakuja.

Je kuna uhusiano gani wa ndoto na posture ya kulala? na hii kitu inaitwa majinamizi ni vvitu gani?



===Majibu kutoka kwa WanaJF===






TWASHUKURU KWA MAELEZO YAKO KWA TUSIOFAHAM TUMEFAHAM SASA zile imani zakuwa nimelogwa sasa basi
 
Back
Top Bottom