Mara nyingi wanaopata ndoto za kutisha au kuhisi kukabwa wakiwa usingizini, ni matokeo ya mgandamizo wa nerves au wakati mwingine kunasababishwa na kushiba sana au kuvimbiwa.
Ulaji wa chakula kingi kabla ya kwenda kulala si mzuri, kwa sababu kunasababisha tumbo kukugasana na diaphragm, na hi upelekea mgandamizo kwenye mapafu na kusababisha kutoweza kupumua vizuri.
Hali hii inapotokea, ubongo unajaribu kutafuta au kutaka kujuwa nini tatizo ili kuweza kukupa taarifa au ufahamu wa kile kinachoendelea. Matokeo ni pale ubongo unaposhindwa kutafairi tatizo ndio ukuletea taarifa ambayo wewe unaiona kuwa kuna mtu au dubwana fulani linakukaba na ndoto zingine za kutisha.
Vilevile inaweza kuwa ni Paralysis, ambayo usababiswa kwa kuharibiwa kwa nervous system au mgandamizo mkubwa kwenye nervous wakati wa kulala, ushauri jaribu kutumia mto ambao si mgumu na kula chakula masaa mawili au matatu kabla ya kulala na chakula kiwe laini na usishibe sana kwa sababu itakusababishia mgandamizo kati ya tumbo na diaphragm na kupelekea kupata hayo mamtatizo.
Kabla ya kulala ni vema ukakoga maji ya uvuguvugu, hii usaidia nerves zako ku relax na kukupelekea kupata usingizi mzuri na unywaji wa maziwa ya moto kabla ya kulala, japo nusu saa kabla pia inasaidia kupata usingizi mzuri.
Ila kama tatizo ni kubwa ni bora kuonana na daktari ili kuweza kujuwa tatizo kwa undani zaidi.