Kuna ukweli kwamba Almasi haipasuki hata ikigongwa na nyundo?

Kuna ukweli kwamba Almasi haipasuki hata ikigongwa na nyundo?

Almasi ni moja ya vitu vigumu zaidi duniani, lakini haimaanishi kwamba haipasuki au haiharibiki kabisa ikigongwa.

Almasi ina ugumu wa kiwango cha 10 kwenye skeli ya Mohs, ambayo hupima ugumu wa madini.

Hii inamaanisha kwamba inaweza kukwaruza vitu vingine vyenye ugumu mdogo, kama kioo au chuma.

Lakini ugumu wa almasi ni juu ya uwezo wake wa kukabiliana na mikwaruzo, siyo ustahimilivu wa kupasuka.

Almasi ina tabia ya kupasuka kirahisi (brittle), ambayo inamaanisha kwamba kama ikigongwa kwa nguvu fulani, inaweza kuvunjika au kupasuka.

Kwa hiyo, kama almasi ingegongwa kwa nyundo katika mwelekeo fulani wa kijiometri, inaweza kupasuka kwa sababu ya tabia yake ya kuwa brittle, licha ya kuwa ngumu sana.

Kwa nini almasi ni maalum:
Almasi inapata ugumu wake kutokana na muundo wake wa kijiometri wa atomi za kaboni.

Atomi za kaboni kwenye almasi zimepangwa kwenye muundo wa kipekee (tetrahedral), ambapo kila atomi ya kaboni inaunganishwa na nne nyingine kwa nguvu za kovalenti.

Hii hufanya almasi kuwa na ushirikiano thabiti na mgumu wa kimuundo.

Je, almasi inaweza kutumika kwenye skrini za simu na TV?

Ingawa almasi ni ngumu sana na inaweza kustahimili mikwaruzo, haitumiki kwa wingi kwenye skrini za simu au TV kutokana na sababu mbalimbali:

1. Gharama: Almasi ni ghali sana kutengeneza au kutumia kwa matumizi makubwa kama skrini za simu au TV.

2. Kupasuka kirahisi (brittleness): Ingawa almasi ni ngumu, bado inaweza kupasuka kwa urahisi chini ya shinikizo au mshtuko, jambo ambalo sio nzuri kwa vifaa kama simu au TV ambazo zinahitaji kuwa na uwezo wa kustahimili kudondoka.

3. Teknolojia mbadala: Vifaa kama Gorilla Glass na sapphire hutumika kwenye skrini za vifaa kwa sababu ni vigumu dhidi ya mikwaruzo na zinatoa uwiano bora wa ugumu na kustahimili mshtuko.

Kwa hiyo, ingawa almasi ina sifa ya ugumu wa juu, haifai moja kwa moja kutumika kwenye skrini za vifaa vya elektroniki kutokana na tabia yake ya kupasuka kirahisi na gharama zake za juu.
Je ugumu wa madini(hardness) ndio thamani yake ilipo pia?kama Almas ina 10 je ukipata jiwe lenye ugumu kuanzia 5 kwenda juu lina thamani pia?
 
Je ugumu wa madini(hardness) ndio thamani yake ilipo pia?kama Almas ina 10 je ukipata jiwe lenye ugumu kuanzia 5 kwenda juu lina thamani pia?
Ugumu wa madini (hardness) sio kigezo pekee cha thamani ya madini. Ingawa almasi ina ugumu wa 10 kwenye skeli ya Mohs, thamani yake inatokana na mambo mengi zaidi kama uzuri, uadimu, ukubwa, na soko lake.

Madini mengine yenye ugumu wa 5 au zaidi yanaweza yasiwe na thamani kubwa kama almasi kwa sababu ya vigezo vingine kama mwonekano, rangi, au matumizi yake kwenye soko la vito au viwanda.

Kwa mfano, korunda (corundum) yenye ugumu wa 9 inaweza kuwa ya thamani kubwa ikiwa inajulikana zaidi kama yakuti au zumaridi(hii hata kwenye biblia imeandikwa kuwa ni madini yaliyoko hata mbinguni) . Mfano mwingine hapa ni madini ya rubi nayo yako kundi hili la korunda.

Hata Tanzanite ya hapa kwetu ina ugumu wa 6.5 hadi 7 kwenye skeli za mohs ila bei yake ni kubwa kuliko madini mengi ingawa haiifikii bei ya Almasi kwa sababu ya uadimu wake na matumizi yake

Lakini madini kama apatite yenye ugumu wa 5 yanaweza yasiwe na thamani kubwa kwa sababu hayana sifa nzuri kama vile mwanga au mwonekano unaovutia.

Kwaiyo naomba tuhitimishe hivi ingawa ugumu unachangia katika thamani, sifa nyingine kama uadimu wa madin, matumizi ya madini, na mwonekano wa kuvutia pia ni muhimu kuzingatia.
 
Mkuu asante kwa maelezo yaliyoshiba,kuna mawe fulani nitayapost humu nitakutag ili uone kama unaweza kuyatambua
 
Diamond sio ngumu kwa kuigonga ni ngumu kwa kuisugua. Hivyo kuna uwezekano wa nyundo kuishatter diamond ikigongwa vizuri kwenye its line of weakness. Ndiyo maana wanasema diamonds are hard but brittle.
Ni sawa mkuu kuvunyika itavunjika ila kwa mbinde na ukishaivunja angalia nyundo yako itakua imechimbika chimbika, kwakua chuma yenyewe ni ina malleable property.

Kuna hizi term mbili, sina uhakika kama kuna maneno ya kisiwa yakutofautisha maana zake.

Hardness na Toughness
Mkuu nyundo(chuma) kwa almasi ni kama sabuni ya kipande (jamaa) na kipande cha chupa),

Ukigonga nyundo kwa nguvu kunauwezekano almasi ikatitia ndani ya nyundo mithili ya chupa inavyotitia ndani ya sabuni.
Hardness,
Diamond hata glass inaangukia kwenye hardness lakini hauwezi ukaifinyanga itavunjika (brittle),

Toughness,
Chuma ni tough ponda unavyoponda haitavunyika ila itakua inapondeka tu hivyo unaweza ukaifinyanga (malleable).
 
Ni sawa mkuu kuvunyika itavunjika ila kwa mbinde na ukishaivunja angalia nyundo yako itakua imechimbika chimbika, kwakua chuma yenyewe ni ina malleable property.

Kuna hizi term mbili, sina uhakika kama kuna maneno ya kisiwa yakutofautisha maana zake.

Hardness na Toughness

Hardness,
Diamond hata glass inaangukia kwenye hardness lakini hauwezi ukaifinyanga itavunjika (brittle),

Toughness,
Chuma ni tough ponda unavyoponda haitavunyika ila itakua inapondeka tu hivyo unaweza ukaifinyanga (malleable).
Mkuu diamond ni hard actually ni the hardest natural element japo now kuna artificial elements ambazo ni hard kuliko diamond. ila diamond ni brittle inaweza kuvunjika hata kwa kugongwa na chuma. Ugumu wake uko kwenye kusuguliwa na ndio maana hutumika kudrill miamba kama tip ya drill kwa sababu ni ngumu kuishilia kwa kuisugua.
Unaweza kutazama video kadhaa za maelezo youtube ambapo diamond zinavunjwa kwa nyundo. Maana yake si kwamba si rahisi kuvunjika, ila hammer inaweza kuivunja hivyo kama inaweza kuivunja hasa ikiwa na tip.
 
Mkuu diamong ni hard actually ni the hardest natural element japo now kuna artificial elements ambazo ni hard kuliko diamond. ila diamond ni brittle inaweza kuvunjika hata kwa kugongwa na chuma. Ugumu wake uko kwenye kusuguliwa na ndio maana hutumika kudrill miamba kama dip ya drill kwa sababu ni ngumu kuishilia kwa kuisugua.
Unaweza kutazama video kadhaa za maelezo youtube ambapo diamond zinavunjwa kwa nyundo. Maana yake si kwamba ni rahisi kuvunjika, ila hammer inaweza kuivunja hivyo kama inaweza kuivunja hasa ikiwa na tip.
Hiyo ni fact mkuu nimekuelewa... Tupo pamoja hujaniacha.
 
Kha! Mungu atusaidie sisi kama taifa, atujalie kupambana na huu ugonjwa unaowakabili watoto wa 2000
Hello Great thinker wa JF,

Hivi ni kweli kwamba Almasi haipasuki hata ikigongwa na nyundo?
Kama ni kweli, Almasi ina kitu gani special mpaka isipasuke hata ikigongwa na nyundo?

Na vipi kuna uwezekano wa kutumia Almasi kwenye screens za simu, TVs n.k kuepuka kuharibika pindi zikidondoka?

View attachment 3131409
 
Uanaweza kumudu simu yenye kioo cha Almasi?

Kweli vitoto vya 2000 vimeingia JF.
Yaani kisimu chako kimevunjika kioo umewaza Simu iwe na kioo cha Almasi😂😂

Muache awe na mawazo huru. Pengine hajui kwamba, kuwa na vifaa vyenye almas vitakuwa na bei kubwa sana. Hakuna atakayenunua. Pia vitakuwa vinawindwa sana na vibaka.
😂
 
Back
Top Bottom