Kuna ukweli wowote katika aina hii ya utapeli?

Hakuna kitu kama hicho. Kuna thread iko hapa juzi tumejadali sana kuhusu hili. Wengine wanadai kuna dawa inafanya mtu anatenda mambo bila free will ila hayo yote ni uvumi. Kungekuwa na dawa za aina hiyo kwanza wangepigwa wenye fedha ndefu tu na wasingehaika na vitu kama simu za techno na fedha za kutoa kwa simu. Na zaidi, wanawake wazuri wangepona? Si wangekuwa wanachukuliwa kama utani tu?
hayajakukuta

dadangu alitoa cm, hela ya nauli, pochi na kadi ya ATM, na namba ya siri akawapa

ndani ya muda mchache wakaenda kutoa hela kwa wakala
 
Unadhani mimi nimepinga kuwa hakuna utapeli wa namna hiyo? Mimi nakubali kabisa upo na kuna watu wanatoa mpaka nyumba. Ninachopinga ni nadharia kuwa eti watu wanapumbazwa na dawa! Hakuna cha dawa. Huyo dada yako aliingizwa kingi kwa maneno ya kilaghai tu na yeye mawazo yake yote akawa ameyaweka kwenye kuchuma fedha au utajiri wa haraka. Unatakiwa kujua kuwa kuna watu wenye vipaji vya kutapeli na mtu kama hutafakari mara mbili ni rahisi sana kuingia kingi. Ingekuwa ni dawa inatumika hailaiki yote ya watanzania wanaotembea mitaani na ATM kadi zao wangesalimika? Kama unashindwa kukubali hebu tafakari hili: Ilikuwaje mtu kama Kibwetere adanganye watu wengi namna ile na wote wajiue kwa mpigo?
 
Ndiyo maana mara nyingi misaada ya ndugu huwa naikwepa sana.

Utapewa msaada utafuatiliwa matumizi yako hadi wazazi wako na watu wengine watapigiwa simu ili wajue tu umesaidiwa na ndugu fulani.

Anyway, mkuu hiyo aina ya utapeli upo.
 
Muhimu ni kuvuta ndum na kula noah a.k.a kitimoto! Uchawi hauendi kwa mentali!
Na pia utanzania wetu na roho nzuri zinatutesa sometimes,. Mafuta yamepanda bei na kila kitu pia af bado unapata mda wa kuanza kubembelezana street?
Mimi personally hua staki maneno mengi, ukinisimamisha nakuchana straight to the point kukuuliza unachotaka, kama ukianza story nakuacga nazo!
 
Mwanajeshi gani wewe intelijens huna eti sky soldier futa au badili Hilo jina
 
ilimtokea mtu wangu wa karibu pia, tofauti yeye aliombwa amuelekeze njia ya kwenda kituo cha watoto yatima. Baadae akamuomba ampeleke kabisa. Kukubali tu ikawa kosa akaanza kuambiwa karogwa na amelishwa nywele na wachawi, kukagua mdomoni kweli akazikuta nywele nyingi tu. To cut a story short, alipigwa simu mbili pamoja na handbag. Hao jamaa wapo, sure kabisa.
 
Unadhani mimi nimepinga kuwa hakuna utapeli wa namna hiyo? Mimi nakubali kabisa upo na kuna watu wanatoa mpaka nyumba. Ninachopinga ni nadharia kuwa eti watu wanapumbazwa na dawa! Hakuna cha dawa. Huyo dada yako aliingizwa kingi kwa maneno ya kilaghai tu na yeye mawazo yake yote akawa ameyaweka kwenye kuchuma fedha au utajiri wa haraka. Unatakiwa kujua kuwa kuna watu wenye vipaji vya kutapeli na mtu kama hutafakari mara mbili ni rahisi sana kuingia kingi. Ingekuwa ni dawa inatumika hailaiki yote ya watanzania wanaotembea mitaani na ATM kadi zao wangesalimika? Kama unashindwa kukubali hebu tafakari hili: Ilikuwaje mtu kama Kibwetere adanganye watu wengi namna ile na wote wajiue kwa mpigo?
Narudia kama jamaa hapo juu. Hayajakukuta na usiombe yakukute, maana utafika nyumban unawaambia "Me nlijikuta tu nmewapa simu na wallet" kuna matapeli wa kuitumia akili na kuna wale wanatumia Magic kama huna ushuhuda usipende kuongea hovyo.
 
Huyo jamaa ni mbishi mno, ana dunia yake flani na hawezi kamwe kukubaliana na wengine.
 
Kutapeliwa ni matokeo ya ujinga, tamaa na Kupenda mambo yaje kirahisi.

Moja ya udhaifu wangu ni kutopenda kusaidiwa hasa na watu nisiowaomba, yaani mtu from nowhere aje aniambie blah! Blah! Au anipigie Simu Kwa kweli mara nyingi ninawatapeli wao.

Trust no one hiyo ndio falsafa itakayokusaidia kwenye ulimwengu huu

Binafsi siwezi kutapeliwa,
 
ilimtokea mtu wangu wa karibu pia, tofauti yeye aliombwa amuelekeze njia ya kwenda kituo cha watoto yatima. Baadae akamuomba ampeleke kabisa. Kukubali tu ikawa kosa akaanza kuambiwa karogwa na amelishwa nywele na wachawi, kukagua mdomoni kweli akazikuta nywele nyingi tu. To cut a story short, alipigwa simu mbili pamoja na handbag. Hao jamaa wapo, sure kabisa.
Ilinitokea pia posta.. ety nimuelekeze kituo Cha watoto yatima na nlikua nakijua Kiko temeke nkamwambia panda gar za temeke.. ghafla jamaa mwingine huyo anauliza shida Nini kwan..? akaelekezwa na yule jamaa wa Kwanza tukaanza kubishana Sana me nawaambia hapo posta sjawai kuskia iko kituo jamaa wa pili anasema kipo kule mbele tumpeleke... Lol si nkajikuta nmeanza kwenda na Mimi jumla watatu.. kufika mbele Sana movement za watu zinazid kupungua ndo napata akili me nawasindikiza kituo gani wakat Ata skijui nkageuza chap... Aisee wangeniliza kila kitu siku ile.. walinilaumu nna roho mbaya spend kusaidia watu blah blah Ila nlipona.. so haya Mambo yapo sana
 
Narudia kama jamaa hapo juu. Hayajakukuta na usiombe yakukute, maana utafika nyumban unawaambia "Me nlijikuta tu nmewapa simu na wallet" kuna matapeli wa kuitumia akili na kuna wale wanatumia Magic kama huna ushuhuda usipende kuongea hovyo.
Haya... nipe ushuhuda wako. Najua kuna watu wengi wanaibiwa, na wakishaibiwa hukimbilia kusema ''nilijikuta nawapa kila kitu bila kujua'' kumbe siyo kweli. Walizidiwa maarifa tu wakawa wamehamishia akili na ufahamu wao wote kwenye ''kupata'' na mchezo ulipoisha ndiyo wakakumbuka.
 
Ilinitokea pia posta.. ety nimuelekeze kituo Cha watoto yatima na nlikua nakijua Kiko temeke nkamwambia panda gar za temeke.. ghafla jamaa mwingine huyo anauliza shida Nini kwan..? akaelekezwa na yule jamaa wa Kwanza tukaanza kubishana Sana me nawaambia hapo posta sjawai kuskia iko kituo jamaa wa pili anasema kipo kule mbele tumpeleke... Lol si nkajikuta nmeanza kwenda na Mimi jumla watatu.. kufika mbele Sana movement za watu zinazid kupungua ndo napata akili me nawasindikiza kituo gani wakat Ata skijui nkageuza chap... Aisee wangeniliza kila kitu siku ile.. walinilaumu nna roho mbaya spend kusaidia watu blah blah Ila nlipona.. so haya Mambo yapo sana
MUNGU alikuwa upande wako asee[emoji23]
 
Anaanzaga mmoja ama kukusalimia au kukuulizia kitu, halafu anatokea mtu mwingine, shtuka!

Anaweza akakuacha wewe halafu akamwambia huyo alieongezeka kuwa ana matatizo flani na akayatatua hapo hapo kwa namna na wewe unaona kbs na huyo jamaa akaondoka zake.

Halafu anaendelea kukuulizia kile alichokuwa anakuuliza na labda ni kitu kidogo mno kwako.
Kwa akili ya tamaa na matatizo watu walionayo ukikumbuka jamaa alivosaidiwa kirahisi unajikuta tu umeshakuwa mateka kisaikolojia.
 
Back
Top Bottom