Kuna ulimwengu usioonekana?

Kuna ulimwengu usioonekana?

Naendelea leo wakuu...lakini kabla sijaendelea naomba nisimulie kwa kilichotokea mpaka kupata ajali ambayo nusura initoe uhai
Niliamka nikiwa bukheri wa afya tayari kwa mishe zangu, mimi naishi Pwani lakini kuna mishe zangu nyingi ziko Dar.. Hivyo sometimes hujilawa mapema asubuhi ili kufika dar mapema
Siku husika nilikuwa na miadi saa nne hivi mitaa ya kurasini hivyo nikitoka saa moja nawahi kabisa
Nimeshajiandaa nachukua funguo ya kausafiri kangu nakutana na pancha.. Logistics za kubadili tairi zingenichukua si chini ya nususaa kulingana na mazingira niliyokuwa nayo
Kwa bahati njema wakati natafakari cha kufanya akapita jirani yangu na kunipa lift mpaka magomeni

Nikafika kwa wakati Kurasini na kufanya shughuli zangu mpaka saa kumi hivi nilipopata nafasi ya kuandika hii mada niliyokwisha iandaa siku moja kabla
Nikiwa nimeshaanza kuandika nikapata simu ya dharura na kunitaka nifike Mbezi kwa haraka! Nilikatisha kuandika nikapost nilipoishia ili nikimaliza ishu yangu Mbezi niendelee

Ishu ya pale Mbezi ikala muda wangu na nikatoka pale hoi, nikasema hapa siwezi kuendelea kuandika nimechoka acha nifike home nipumzike nitaendelea kuandika usiku

Mbezi nikakamata usafiri wa jumuiya na kunifikisha salama kituo ninachoshukia.. Hapo sasa ilikuwa ni kuchukua boda kunifikisha kilingeni kwangu

Nikampigia boda wangu lakini akasema yuko mbali hivyo nikamchukua aliyepo japo kwa kusita sana sana! Hapa nilipaswa kuisikiliza roho yangu lakini nikafanya ukaidi
Nikapanda akaondoa chombo ili tuvuke barabara, nilichosikia ilikuwa ni honi moja tu ya boda aliyekuwa kibati mbaya.. Sekunde iliyofuata ilikuwa ni bonge la sauti la mgongano

Nilipaishwa juu na kutua juu ya lami kwa kuburuzika kidogo.. Kilichofuata ilikuwa ni kelele za watu na maruweruwe.. Nilibakiza kidogo mno kupoteza fahamu
Nilisaidika kwa haraka kusogezwa pembezoni mwa barabara na kupata huduma ya kwanza na kuwahishwa hospital
Simu, saa na pochi vilisalimika kuna msamaria mwema alinihifadhia (ananifahamu) vingine vilimwagika, kuharibika na kupotea eneo la ajali

Nilifikishwa hospital na kupata matibabu.. Ilihofiwa nitakuwa nimevunjika mkono wa kulia kutokana na ulivyokuwa ukionekana lakini baada ya vipimo nikaonekana sina mvunjiko wowote bali majeraha ya kawaida kwenye mguu wa kulia kiuno cha kulia mkono na bega la kulia

Sikulazwa niliruhusiwa usiku huo huo no kati ma kilingeni nikiwa na pancha za kutosha ambazo sikuwa nazo asubuhi

Kuhusu eneo la ajali ni eneo ambalo ndani ya mwezi mmoja limeshaondoka na roho zisizopungua sita na ajali yangu ilikuwa ya nne ndani ya siku kumi huku zingine zikiuwa wawili, mmoja eneo la ajali na mwingine alifia hospital. Ajali ya tatu huyo alivunjika mguu na majeraha mengine! Ajali ya nne ni mimi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu ni mahiri mno kubisha kwamba hakuna mambo ya kimwili yenye kiroho yenye tafsiri za kimwili wala hakuna ulimwengu wa roho unaoona yajayo na kutupa taarifa kabla hayatokea kwa njia ya mafumbo

Mimi ni mzuri sana wa kusikiliza sauti za rohoni lakini kwa kupungukiwa na ukamilifu wa kibinadamu na kuzongwa na harakati za maisha nilipuuzia pengine zile alarms za kiroho tangu siku ilipoanza
Kwa aliyetangulia kutoka kabla yangu siku ile aliiona gari ikiwa sawa kabisa bila pancha yoyote, kwa maana ilikuwa na upepo wake wote usiku mzima! Hata nilipkuja kuifungua na kupeleka kwa fundi leo hiyo, haikuwa na pancha yoyote bali upepo uliisha tu wenyewe! Imejazwa upepo na iko sawa kabisa

Kuna matukio kama mane hivi yalitawala siku yangu nzima siku ile na hata hizo mishe zangu hazikuenda sawa kwa asilimia zote
Ndoto za jana yake usiku pia zilikuwa na ujumbe wake.. Kuota nimepaa na chombo chetu[emoji3] kisha kupigwa push na bati la kimbunga na kuangukia kwenye mawe..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna ulimwengu wa roho usioonekana lakini upo na unaishi yaani ni kama akili tunazo lakini hatuwezi kuzionrmesha kwenye uyabisi wake
Ni kati ya huu ulimwengu wa roho unaondesha dunia na ulimwengu huu wa nyama hapa katikati ndio kuna ulimwengu kijakazi unaounganisha na kutafsiri jumbe za ulimwengu wa roho kwenda kwenye ulimwengu wa mwili

Ni kama vile mchakato wa kutengeneza gongo
Kuna moto unaochemsha pipa lenye malighafi ya kutengeza gongo, kisha kuna mpira usiovuja ambao unabeba mvuke toka kwenye pipa linalochemka lililozibwa kisawasawa (sealed) na kuupeleka/kuupitisha ule mvuke kwenye kipozeo (condenser) na hatimaye kufikia kwenye kipokeo (receiver tank) ambacho si muhimu sana kiwe sealed

Hapo kwenye huo mchakato chochote kikienda kombo huwezi pata matokeo tarajiwa ambayo ni gongo safi nambari moja!
Vivyo hivyo kwenye ulimwengu wa roho hakupaswi kuwepo na uvujaji wowote wa taarifa husika mpaka ifike inapitakiwa salama.. Tofauti na hapo taarifa yoyote inayovuja katikati kwenye bomba (codes breaker) huleta matokeo yasiyokamilika na ama kusababisha
Tafsiri potofu/kinyume
Ucheleweshaji wa tafsiri
Ndoto maruweruwe/kutisha
Uchizi/wendawazimu/upumbavu nk



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu duniani kinaongozwa na mambo matatu na huo ndio ukamilifu wake.. Kwenye karma tunaita
Cause/ chanzo
Condition/ michakato
Effect/ matokeo
Chochote kile ulimwenguni kinaongozwa na hiyo kanuni ya utatu
Cause/chanzo huu ndio ulimwengu wa roho
Condition/mchakato huu ndio kiunganishi kitendaji
Effect/matokeo huu ndio ulimwengu wa mwili

Mara nyingi kama si mara zote huwa wengi wetu hatuangalii asili ya kitu/tendo wala mchakato wake bali huangalia matokeo au matokeo kwanza .. Hakuna kinyume kwenye hii kanuni kwamba effect, condition then cause..! Hakuna.. Kama muda usivyo na rivasi basi hii kanuni nayo haina kinyumenyume!

Matendo yote yanayofanyika kwa usahihi na pengine utimilifu bila kujali matokeo tarajiwa kuwa hasi ama chanya hufuata mlolongo huo bila kuwa na kasoro kwenye mchakato mzima

Ndoto zisizoeleweka (vague dreams)
Upungufu/ukosefu wa akili
Uchizi/uwendawazimu
Kasoro za kimaumbile nknk vyote hivi vina uhusiano wa moja kwa moja na kanuni yetu ya utatu mkamilifu

Ndoto niliyoota ya kuripoti kituo cha police nisichokijua ni ulimwengu wa tafsiri zilizopotoka ama kuvuja toka kwenye chanzo kuelekea kwenye matokeo! Na ni ulimwengu wengi kama sio wote tunaouishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemaliza ila nakupa bonus


Ulimwengu wa roho ni timilifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemaliza ila nakupa bonus


Ulimwengu wa roho ni timilifu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninzuri
 
Watu mijusi au lizard people Kama kina Obama, Elion musk,au wale high illuminated people wanaijua hii concerpt
 
Inahitaji utulivu sana ili kuelewa haya mambo ya kiroho....safi kabsa mshana Jr kwa elimu nzuri.
 
Kila kitu duniani kinaongozwa na mambo matatu na huo ndio ukamilifu wake.. Kwenye karma tunaita
Cause/ chanzo
Condition/ michakato
Effect/ matokeo
Chochote kile ulimwenguni kinaongozwa na hiyo kanuni ya utatu
Cause/chanzo huu ndio ulimwengu wa roho
Condition/mchakato huu ndio kiunganishi kitendaji
Effect/matokeo huu ndio ulimwengu wa mwili

Mara nyingi kama si mara zote huwa wengi wetu hatuangalii asili ya kitu/tendo wala mchakato wake bali huangalia matokeo au matokeo kwanza .. Hakuna kinyume kwenye hii kanuni kwamba effect, condition then cause..! Hakuna.. Kama muda usivyo na rivasi basi hii kanuni nayo haina kinyumenyume!

Matendo yote yanayofanyika kwa usahihi na pengine utimilifu bila kujali matokeo tarajiwa kuwa hasi ama chanya hufuata mlolongo huo bila kuwa na kasoro kwenye mchakato mzima

Ndoto zisizoeleweka (vague dreams)
Upungufu/ukosefu wa akili
Uchizi/uwendawazimu
Kasoro za kimaumbile nknk vyote hivi vina uhusiano wa moja kwa moja na kanuni yetu ya utatu mkamilifu

Ndoto niliyoota ya kuripoti kituo cha police nisichokijua ni ulimwengu wa tafsiri zilizopotoka ama kuvuja toka kwenye chanzo kuelekea kwenye matokeo! Na ni ulimwengu wengi kama sio wote tunaouishi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku nliwahi kuota napelekwa kituo cha polisi kesho yake nikapata ajali ya gari yule aliye nisababishia ajali akaniambia tusiende polisi tumalizane ilikuwa usiku akanilipa fidia nikaenda nyoosha gari nika piga rangi maisha yaka endelea
 
Niliota kuna jamaa kaniwekea sumu kwenye beer ya seringeti, kesho yake sikwenda kijiweni, nilipofanya utafiti wa kina nikagundua kulikuwa na huo mapango. Sasa nimehama kijiwe, ndoto ni ulimwengu wa roho, unaweza kutonywa na mababu zako.
 
Back
Top Bottom