Naendelea leo wakuu...lakini kabla sijaendelea naomba nisimulie kwa kilichotokea mpaka kupata ajali ambayo nusura initoe uhai
Niliamka nikiwa bukheri wa afya tayari kwa mishe zangu, mimi naishi Pwani lakini kuna mishe zangu nyingi ziko Dar.. Hivyo sometimes hujilawa mapema asubuhi ili kufika dar mapema
Siku husika nilikuwa na miadi saa nne hivi mitaa ya kurasini hivyo nikitoka saa moja nawahi kabisa
Nimeshajiandaa nachukua funguo ya kausafiri kangu nakutana na pancha.. Logistics za kubadili tairi zingenichukua si chini ya nususaa kulingana na mazingira niliyokuwa nayo
Kwa bahati njema wakati natafakari cha kufanya akapita jirani yangu na kunipa lift mpaka magomeni
Nikafika kwa wakati Kurasini na kufanya shughuli zangu mpaka saa kumi hivi nilipopata nafasi ya kuandika hii mada niliyokwisha iandaa siku moja kabla
Nikiwa nimeshaanza kuandika nikapata simu ya dharura na kunitaka nifike Mbezi kwa haraka! Nilikatisha kuandika nikapost nilipoishia ili nikimaliza ishu yangu Mbezi niendelee
Ishu ya pale Mbezi ikala muda wangu na nikatoka pale hoi, nikasema hapa siwezi kuendelea kuandika nimechoka acha nifike home nipumzike nitaendelea kuandika usiku
Mbezi nikakamata usafiri wa jumuiya na kunifikisha salama kituo ninachoshukia.. Hapo sasa ilikuwa ni kuchukua boda kunifikisha kilingeni kwangu
Nikampigia boda wangu lakini akasema yuko mbali hivyo nikamchukua aliyepo japo kwa kusita sana sana! Hapa nilipaswa kuisikiliza roho yangu lakini nikafanya ukaidi
Nikapanda akaondoa chombo ili tuvuke barabara, nilichosikia ilikuwa ni honi moja tu ya boda aliyekuwa kibati mbaya.. Sekunde iliyofuata ilikuwa ni bonge la sauti la mgongano
Nilipaishwa juu na kutua juu ya lami kwa kuburuzika kidogo.. Kilichofuata ilikuwa ni kelele za watu na maruweruwe.. Nilibakiza kidogo mno kupoteza fahamu
Nilisaidika kwa haraka kusogezwa pembezoni mwa barabara na kupata huduma ya kwanza na kuwahishwa hospital
Simu, saa na pochi vilisalimika kuna msamaria mwema alinihifadhia (ananifahamu) vingine vilimwagika, kuharibika na kupotea eneo la ajali
Nilifikishwa hospital na kupata matibabu.. Ilihofiwa nitakuwa nimevunjika mkono wa kulia kutokana na ulivyokuwa ukionekana lakini baada ya vipimo nikaonekana sina mvunjiko wowote bali majeraha ya kawaida kwenye mguu wa kulia kiuno cha kulia mkono na bega la kulia
Sikulazwa niliruhusiwa usiku huo huo no kati ma kilingeni nikiwa na pancha za kutosha ambazo sikuwa nazo asubuhi
Kuhusu eneo la ajali ni eneo ambalo ndani ya mwezi mmoja limeshaondoka na roho zisizopungua sita na ajali yangu ilikuwa ya nne ndani ya siku kumi huku zingine zikiuwa wawili, mmoja eneo la ajali na mwingine alifia hospital. Ajali ya tatu huyo alivunjika mguu na majeraha mengine! Ajali ya nne ni mimi
Sent using
Jamii Forums mobile app