Kuna umuhimu wa jeshi letu kuboresha sare zake ziwe za kisasa zaidi

Kuna umuhimu wa jeshi letu kuboresha sare zake ziwe za kisasa zaidi

inspectorbenja

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
597
Reaction score
651
Habari wanajamvi,

Nimekuwa nikifuatilia uniform za majeshi ya nchi zinazoendelea kama Marekani, China, Uinhereza n.k. Itagundua uniform za majeshi yao za zamani na sasa ni tofauti kabisa.

Mfano jeshi la Marekani uniform zao wakati wa vita vya Vietnam na za sasa ni tofauti kabisa. Za sasa zina muonekano mzuri na wa kuvutia. Achilia mbali buti zao zile zenye rangi ya kaki.Yaani mjeda akisimama hivi mpaka unapenda, alafu pembeni kuna baji ina rangi ya bendera.

Akienda kwenye operesheni ana miwani, helmet ya kisasa. Alaf kavaa kitu kama jaketi fulani hivi lina bullet prrof material na sehemu za kuwekaweka silaha na mabomu.

Sasa uniform za jeshi letu ni zile zile za tangu enzi za nduli, ya kijani kijani hivi. Naona kama zimepitwa na wakati. Pia mabuti yetu meusi yale yale za kizamani. Ninadhani tunahitaji uniform zenye mvuto zaidi.
 
Full gear ya Askari mmoja wa marekani hapungui milioni 20 je uchumi wetu unasapoti hiyo? ile bunduki peke yake ni milioni 13 achilia mbali radio bullet proof viatu uniform pistol na matakataka mengine kibao ambayo teknolojia yake haijatufikia bado.
 
Mkuu nisamehe ila napingana na wewe katika uniform za hovyo ni za us army, nenda kwenye picha za leo za kufunga mafunzo ya ukomandoo uone tofauti ya uniform..uniform zetu ni the best.

Kwenye gears ukitoa hizo fatigue wao wako advanced, hizo styles nyingine sisi sio ishu sana ila kwa uniform we are the best
 
Screenshot_20210911-212633.png
 
Camouflage uniforms zinategemea na eneo na mazingira, labda useme tutafute gear za kisasa ila sio uniform
 
Nchi nyingi za Kiafrika uniform za jeshi ziko vizuri tatizo labda ni bajeti tu ya kuwapa uniform mpya wanajeshi kwa wakati muafaka
 
TUKIONA ZIMEPITWA NA WAKATI TUTAREKEBISHA...

ZA WAMAREKANI ZILIPITWA NA WAKATI NDIO MAANA WAKAREKEBISHA.

Uoto wa Asili... Kijani kibichiiiii
 
..tatizo nililoliona mimi ni baadhi ya askari kuvaa uniform oversize ambazo haziwakai vizuri mwilini.

..hali hiyo inasababisha askari wetu waonekane hawako nadhifu, wakati sifa ya askari ni pamoja na unadhifu.
Over size zinavaliwa hasa kwenye sherehe za kitaifa
 
Hakuna walichoboresha kwenye uniform, bali mazingira ya eneo vita inapopiganwa uamua wavae uniform ipi? Zipo mpaka sare za kwenye Ice/ snow land
1631393965362.png

1631393994467.png


Kombat za kwenye mazingira ya snow

1631394114296.png
 
Back
Top Bottom