Uchaguzi 2020 Kuna umuhimu wa kupiga kura 2020 wakati tume iko mfukoni kwa Rais?

Uchaguzi 2020 Kuna umuhimu wa kupiga kura 2020 wakati tume iko mfukoni kwa Rais?

siasa hizi 😂: kwan si tunamuongezea awamu baada ya awamu ya pili, nyie endeleeni kutafuta tume:
 
Bora kususa wenzetu mle, kuliko tushiriki na bado tusile. Kimsingi sasa hivi hamna uwezo tena wa ushindani maana kizazi hiki hakiko na chama cha zamani, hivyo namna pekee ni nyie kunajisi chaguzi kwa msaada wa vyombo vya dola.
Siku hizi wanashinda bila kupingwa new strategy
 
Let me be very blunt here. Siasa zetu sasa hivi zinahitaji "reset button". Mtu ukipiga hesabu za haraka haraka, ukaangalia kule tulikoanzia, kule tulikopitia, na pale tulipo sasa, utagundua kwamba safari yetu tuliianza vizuri, tukakwama, tukajinasua, halafu tukaendelea vizuri kwa yard kadhaa, na sasa hivi tumekwama tena. Tunahitaji kujinasua ili safari iendelee.

Tatizo mkwamo wetu wa mara hii ni mbaya zaidi ya mikwamo yote tuliyowahi kuipitia. Wengi hatujaliangalia hili kwa jicho la ndani lakini Tanzania ya sasa inapita katika kitu ambacho kwa lugha rahisi ninaweza nikakielezea tu kama "uncharted waters". Sheria zinakanyagwa ovyo, watu wanatekwa ovyo, wabunge wanatishwa kwa bastola na kushambuliwa kwa risasi, na itifaki za chaguzi za serikali za mitaa zinavunjwa ovyo. Haya ni mazingira ambayo, kama nchi, hatujawahi kuyapitia; ni mazingira yenye utata sana, na ni mazingira ambayo, kwa sababu yamegubikwa na wingu la "unusualness", kisaikolojia yametuvuruga sana.

Na ndiyo maana ninasema "tumekwama", lakini muhimu zaidi, mkwamo wetu wa mara hii si wa kawaida kama mikwamo tuliyokuwa tumeizoea katika enzi zile za Baba wa Taifa, mzee Alhaji Hassan Mwinyi, na nyinginezo. Kuna tembo mkubwa amejaa sebuleni mwetu lakini ingawa tunamwona kabisa huku tukiwa tumemzunguka, woga wa kisichojulikana (fear of the unknown), unaochagizwa na utamaduni wetu wa kukumbatia mazoea, unafanya tumpuuze tembo huyu.

Mtihani unaotukabili sasa, na ambao mpaka sasa umetushinda, uko katika ari yetu ya uthubutu katika kumkabili tembo. Mpaka pale tutakapopata uthubutu wa kukabiliana na kile kinachotuangamiza kisiasa, kijamii, na kiutamaduni, nchi yetu itazidi kutopea katika mkwamo wa tope tuliomo sasa.

Kisiasa, huwezi kuongelea kuhusu nani atashinda au kushindwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu bila kuwa na tume huru, kwa mfano. Kijamii, iko haja ya kudeal na mentality ya jamii yetu hususan kuhusu siasa za mazoea na umuhimu wa itifaki, maana viongozi wetu wanatoka miongoni mwetu. Na kiutamaduni, kama alivyosema mzee Nelson Mandela na hata mzee Lowassa, "elimu, elimu, elimu". Ni muhimu sana Tanzania ii-invest kwenye elimu. Piga garagaza, hakuna kitu kingine kitakachokuja kuiokoa Tanzania bali elimu.

Kama nilivyosema hapo juu, siasa zetu zinahitaji reset button. It is clear that something somewhere has gone very wrong and, as a result, everything is now all muddled up. Uwongo umezidi, ukatili umezidi, alimradi shida tu. I think that we all need to step back, take a good look at ourselves, take stock of our mess, then start again.
 
Hii ni January 01/01/2020. Tuanze kufikiria tutafikaje October na kuanza kufanya implement ions. Tusitegemee kudra.
JPM hawezi kuruhusu Tume huru iundwe kwa sababu anaamini juu ya Tanzania ya Magufuli! Hivyo ni kuwa na Akili isiyoku na Akili, kwenda kupiga kura hali ukijua kuwa Kura yako haitaheshimiwa.
Kwa upande mwingine wanachama wa CCM wanabariki uovu huu kwa misifa ya kutawala milele bila kujali kuwa hali hii itatuletea vita hivi karibuni na kuivuruga nchi yetu vibaya sana.
 
Ndiyo lakini tunahitaji vyama vinavyosaidia watz siyo wala ruzuku tu kama Chadema wanashindwa hata kujenga ofisi wakati wanapewa ruzuku ya almost 350million per month lakini zinaishia kwenye matumbo ya kina Mbowe na genge lake.
Propaganda ya Ruzuku dhidi ya CHADEMA inatukera sana ambao tuna Akili yenye Akili.
 
Ukisusa wenzio wala !
Kama Akili yako inafanya kazi ,ungekuwa umeelewa siku nyingi kuwa Uchaguzi wa Serekali za Mitaa 2019,
Uliporwa kwa nguvu za dora hukususiwa na Upinzani.
Lakini kwa kuwa umekaririshwa kuwa CCM itatawala milele si rahisi kujua hatari ya CCM kuamua kuanza kutawala kimabavu.
 
Juzi nilikuwa masasi nimeshangaa gari na tume ya uchaguzi NEC linapga matangazo watu wakajiandikishe, ukiangalia muitukio wa wananchi kila mtu hana hata habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye uchaguzi wa 2010 Magufuli alifanya hila na mizengwe kibao kwa mpinzani wake kule Chato hadi akapita ubunge bila kupingwa na hii iko kwenye records.

Inaonekana Magufuli hapendi kabisa siasa za ushindani na hii iko kwenye damu yake. Tumeona namna chaguzi ndogo mbali mbali hata na ule uchaguzi wa S/M zilivyovurugwa ili kuhakikisha matakwa yake yanatimia.

Kuna kila dalili kuwa uchaguzi mkuu pia yale yale yatajirudia kwani wakurugenzi wataingia mitini na wagombea wa upinzani watabaki wameduaa na fomu zao mikononi.

Baada ya hapo, wagombea wa ccm watapata tena "Fake Walkover" na kwenda bungeni na kwenye mabaraza ya halmashauri ila yatakayofuata ndio bado hatuwezi kubashiri kwa ufasaha.

Hali kama hiyo iliikumba Ethiopia kwenye uchaguzi wao wa 2015 uliosusiwa na wapinzani na hivyo kulifanya bunge lao kuwa na waunge wa chama tawala tu kasoro moja (1).

Yaliyofuata hadi kupelekea waziri mkuu wao kujiuzulu kufuatia kukaripiwa na Obama hadi kupelekea PM wao wa sasa kuomba 'Poo' kwa wapinzani hadi kuwekwa mpinzani kuwa Speaker wa bunge, is nobody's guess.

All in all, huko mbele tuendako, Tanzania haitabaki kama ilivyo leo na kwa bahati mbaya hakuna nchi ambayo iko 100% self reliant. Ccm huko mbele itabidi waingie kwenye 'National Dialogue' na wapinzani, wapende, wasipende.
 
Ngoja na mm mwaka huu nikachukue jimbo kiulainiiii kupitia CCM.CCM ndiyo baba lao kwa sasa.
 
Haina maana ya Kwenda Kupiga kura ikiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za msingi wa kibinadamu zinaendelea. Kila Mtu ana haki ya kuchagua ama kuchaguliwa, haina maana ya Kwenda kuchagua ikiwa haki yangu ya kuchaguliwa imeminywa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama tungeweza tungefanya kama Oman.
Ukisoma historia na pia kuitembea Oman utaona Sultan Qaboos ameingia madarakani 1970.

Tokea hapo Oman ilikuwa kwa haraka sana kibiashara, kujenga miundombinu kama bandari, barabara, airports za vivutio vya kibiashara kama hotels na vitu kama hivyo.

Kama tungeweza; tungefanya amendment huyu mzee apige kama 20years.

Kagame toka akae Rwanda 1995 Rwanda is stable na wana-thrive.

South Korea alitawala General Park Chung-hee kati ya 1963-79;
Pace aliyoweka kwa mkono wa Chuma ndo ilikuwa turning point ya kukua kiuchumi Korea ya kusini.

Tz lolongolongo na hiena hiena nyingi sana. Kwa rasilimali kama hizi under good leadership TANZANIA inatakiwa iwe mbali sana.

Ila kwa matakwa ya katiba na kuiga Demokrasia zilizoanzishwa na wagiriki; sawa twendeni kwenye uchaguzi huku tukijua JPM anashinda. Na yet tunajua hulo bado tutajipanga foleni kuchagua na kuna wengine washa-declare hawatakwenda kupuga kura.

Kwanini tusifikiri tofauti na kuamua mzee alisongeshe ili Fedha za campaign zifanye shughuli ungine ya kutatua kero za Watanzania



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupiga kura bila tume huru hasa kipindi hiki ambacho dictator anagombea ni uwebdawazimu uliopitiliza.
Hiki ndo kipindi cha kushiriki mchakato wa uchaguzi na kupiga kelele zaidi kuhusu umuhimu wa tume huru! Tutafanya kelele itakayowaamsha majirani wa karibu na mbali na this there’s no giving up!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Leo ni 01/01/2020 hongera kwa kuona mwaka mpya.

Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu. Kwa hali ilivyo kama mihimili yote imeshikiliwa na ule mhimili ulijikita chini zaidi kuna haja gani ya kupiga kura?

Wengi wanadai tume huru ya uchaguzi. Muda tulionao utatosha kuiandaa tume huru na iwe tayari kufanya kazi October 2020? Kama wazo lenyewe la tume huru halijawasilishwa wala kupokelewa?
Sky Eclat mimi nawashauri sio tu wasipige kura, hata kugombea wasigombee. Wafanye kama Serikali za Mitaa. Mbona itakuwa poa tu!!!
 
Back
Top Bottom