Let me be very blunt here. Siasa zetu sasa hivi zinahitaji "reset button". Mtu ukipiga hesabu za haraka haraka, ukaangalia kule tulikoanzia, kule tulikopitia, na pale tulipo sasa, utagundua kwamba safari yetu tuliianza vizuri, tukakwama, tukajinasua, halafu tukaendelea vizuri kwa yard kadhaa, na sasa hivi tumekwama tena. Tunahitaji kujinasua ili safari iendelee.
Tatizo mkwamo wetu wa mara hii ni mbaya zaidi ya mikwamo yote tuliyowahi kuipitia. Wengi hatujaliangalia hili kwa jicho la ndani lakini Tanzania ya sasa inapita katika kitu ambacho kwa lugha rahisi ninaweza nikakielezea tu kama "uncharted waters". Sheria zinakanyagwa ovyo, watu wanatekwa ovyo, wabunge wanatishwa kwa bastola na kushambuliwa kwa risasi, na itifaki za chaguzi za serikali za mitaa zinavunjwa ovyo. Haya ni mazingira ambayo, kama nchi, hatujawahi kuyapitia; ni mazingira yenye utata sana, na ni mazingira ambayo, kwa sababu yamegubikwa na wingu la "unusualness", kisaikolojia yametuvuruga sana.
Na ndiyo maana ninasema "tumekwama", lakini muhimu zaidi, mkwamo wetu wa mara hii si wa kawaida kama mikwamo tuliyokuwa tumeizoea katika enzi zile za Baba wa Taifa, mzee Alhaji Hassan Mwinyi, na nyinginezo. Kuna tembo mkubwa amejaa sebuleni mwetu lakini ingawa tunamwona kabisa huku tukiwa tumemzunguka, woga wa kisichojulikana (fear of the unknown), unaochagizwa na utamaduni wetu wa kukumbatia mazoea, unafanya tumpuuze tembo huyu.
Mtihani unaotukabili sasa, na ambao mpaka sasa umetushinda, uko katika ari yetu ya uthubutu katika kumkabili tembo. Mpaka pale tutakapopata uthubutu wa kukabiliana na kile kinachotuangamiza kisiasa, kijamii, na kiutamaduni, nchi yetu itazidi kutopea katika mkwamo wa tope tuliomo sasa.
Kisiasa, huwezi kuongelea kuhusu nani atashinda au kushindwa katika uchaguzi mkuu mwaka huu bila kuwa na tume huru, kwa mfano. Kijamii, iko haja ya kudeal na mentality ya jamii yetu hususan kuhusu siasa za mazoea na umuhimu wa itifaki, maana viongozi wetu wanatoka miongoni mwetu. Na kiutamaduni, kama alivyosema mzee Nelson Mandela na hata mzee Lowassa, "elimu, elimu, elimu". Ni muhimu sana Tanzania ii-invest kwenye elimu. Piga garagaza, hakuna kitu kingine kitakachokuja kuiokoa Tanzania bali elimu.
Kama nilivyosema hapo juu, siasa zetu zinahitaji reset button. It is clear that something somewhere has gone very wrong and, as a result, everything is now all muddled up. Uwongo umezidi, ukatili umezidi, alimradi shida tu. I think that we all need to step back, take a good look at ourselves, take stock of our mess, then start again.