Wakuu,
Huko ulaya na hasa Marekani kuna pastors wengi na vijana wengi wanaojiunga na Kanisa Katoliki kuliko wakati wowote.
Ajabu kubwa wengi hakuna aliyewahubiri wabadilike bali ni kwa utafiti wao wa kina hasa historia ya kweli ya Kanisa na mafundisho ya mababa wa kale wa Kanisa na maandiko matakatifu
Ukitaka kujua kwamba sasa hii movement si kitu kidogo tena nenda youtube na fatilia ushangae kinachoendelea. Hata mainstream media zinatangaza kuwa kuna ongezeko la ajabu hadi kwenye mahudhurio ya misa kwenye makanisa mengi Marekani.
Moja ya sababu ambayo baadhi ya Gen Z wameitoa kuhamia Kanisa Katoliki ni makanisa mengi ya kileo kugeuka kuwa majukwaa ya maonesho, muziki, madhabahu kupambwa na mithili ya nyumba za disko na kupoteza tofauti wanayokutana nayo kwenye majukwaa ya kidunia.
Anyway, kama sio Mkatoliki ukijichanganga kufatilia debate na hizo movement za watu wanaobadilika tena wengi wakiwa ni Pastors, wainjilisti n.k utajikuta na wewe unaanza kuvutika kuchunguza kweli za imani yetu ya Kikristo.
Nafikiri huo upepo ukianza kuja huku tutashangaa prominent pastors waki Bongo wanafunga makanisa na kuwa walei wa Kikatoliki. Let us watch and pray!
Farisayo na sadukayo ndio wewe.
Ujumbe uliotaka kufikisha upo aya ya mwisho.
Kanisa linaloamini utatu, Baba , Mwana na Roho mtakatifu ndio sahihi.
Kanisa linalo ongeza sijui Mama wa Yesu ,mtakatifu sijui kitu gani , ogopa sana.
Yesu alipopaa aliwaambia mitume wasubiri roho mtakatifu na jukumu moja walilo achiwa ni kuhubiri injili, atakayekubali ataokolewa atakaye kataa amekwisha hukumiwa, jukumu la haya makanisa ya walokole, ni kuhubiri, hata mkiwa wawili kanisani lengo kuu limetimia, maana kazi yamtu kuokoka na kutokuokoka si kazi ya wachungaji , ni kazi ya Mungu , maana hata farao na watu wake walikuwa na mioyo migumu kama wewe!
Nuhu alijenga safina, wachache waliitikia huku akibezwa na wengi , njiia ya mbinguni ni nyembamba na wengi hawaioendi.
soma zaburi yote, Mungu anapenda sifa, kazi ya kumwimbia na kumuabudu ni yeye pekee, na Daudi kwenye Zaburi aljmuimbia mpaka nguo zikaanguka.
Wewe , unaleta upuuzi wa "warumi " waliotengeneza ambao haupo kwenye biblia.
Kama ukienda disko na ukumbi umependeza, unafurahia, kwanini Mungu isiwe zaidi ya Disco?
MTAZAMO Kama ukienda Tripple A , Super Dom kujirusha unafurahia disco sasa Mungu in Zaidi, So far htujamtende a haki, tunah.
SHETANI alikuwa mkuu wa sifa mbinguni, akajikuza na kutupwa jehanamu, sasa Ninyi mafarisayo mnahisi sifa ni za shetani ila. ni za Mungu.