Wakuu,
Huko ulaya na hasa Marekani kuna pastors wengi na vijana wengi wanaojiunga na Kanisa Katoliki kuliko wakati wowote.
Ajabu kubwa wengi hakuna aliyewahubiri wabadilike bali ni kwa utafiti wao wa kina hasa historia ya kweli ya Kanisa na mafundisho ya mababa wa kale wa Kanisa na maandiko matakatifu
Ukitaka kujua kwamba sasa hii movement si kitu kidogo tena nenda youtube na fatilia ushangae kinachoendelea. Hata mainstream media zinatangaza kuwa kuna ongezeko la ajabu hadi kwenye mahudhurio ya misa kwenye makanisa mengi Marekani.
Moja ya sababu ambayo baadhi ya Gen Z wameitoa kuhamia Kanisa Katoliki ni makanisa mengi ya kileo kugeuka kuwa majukwaa ya maonesho, muziki, madhabahu kupambwa na mithili ya nyumba za disko na kupoteza tofauti wanayokutana nayo kwenye majukwaa ya kidunia.
Anyway, kama sio Mkatoliki ukijichanganga kufatilia debate na hizo movement za watu wanaobadilika tena wengi wakiwa ni Pastors, wainjilisti n.k utajikuta na wewe unaanza kuvutika kuchunguza kweli za imani yetu ya Kikristo.
Nafikiri huo upepo ukianza kuja huku tutashangaa prominent pastors waki Bongo wanafunga makanisa na kuwa walei wa Kikatoliki. Let us watch and pray!