Kuna ushahidi wowote wa kimazingira kuwa gharika ya Nuhu ilitokea?

Kuna ushahidi wowote wa kimazingira kuwa gharika ya Nuhu ilitokea?

Kisayansi ni ngumu kuthibitisha hilo kwa maana kwa mujibu wa maandiko ni kama dunia nzima ilijazwa na maji and if so basi lazima katika point fulani duniani kote kungekua na layer fulani ya aina moja au yenye tabia zinazofanana yenye kuonesha kwamba kweli Dunia ilikumbwa na hilo tukio katika wakati mmoja.

Now ushahidi uliopo mwingi inaonesha ukanda mmoja tu na wala sio Dunia nzima.

Ila pia kuna hoja ya kwamba baada ya tukio hilo Dunia ni kama ilijireset na kurudi ikiwa kwenye hali ya tofauti coz hata pores zilibadilika kutoka kwenye ule uumbaji wa awali, kwahiyo kinachoonekana ndicho tulichoanza nacho sisi ila hapo kabla Dunia ambavyo ilikua hatujui.

Kwa maana hiyo basi, hiyo hoja ya ushahidi wa kikanda inawezekana iko na ukweli endapo kama baada ya lile tukio dunia ilibadilika mazima, kwa maana hayo mabadiliko inawezekana yalileta nyongeza fulani ambazo mwanzo hazikuwepo, ndio maana by default utaona now kuna hatihati ya bara la Africa kugawanyika kwa maana bahari itaenda kuligawa katika pande mbili, lakini si tu mara la Africa ila kuna visiwa vingi ambavyo miaka mingi ijayo havitaendelea kuwepo, kwa maana dunia inajirudi kwenye ile hali yake ya asili kutoka kwenye ule uumbaji wa awali.

Kwahiyo ni ngumu kusema kwamba ni tukio ambalo liliwahi kutokea kweli au halikuwahi kutokea kwasababu katika upande wowote utakaousimamia katika mjadala huu ni ngumu kufikia muafaka ambao Kila mtu atatoka ameridhika nao.
 
Wanasayansi wanasema kiasi chote cha maji duniani(ndani ya ardhi, hewani na juu ya ardhi) ni kilomita za ujazo 1.38 bilioni. Biblia inasema maji ya gharika ya Nuhu yalifunika milima yote hadi mikono kumi na tano juu yake.

Kwa wastani ili maji yafunike hadi mlima Everest kutoka usawa wa bahari zinahitajika kama kilomita za ujazo za maji bilioni 4.5! Karibu kilomita za ujazo bilioni tatu za maji zinatakiwa kuongezeka duniani ili kufanikisha gharika ya Nuhu. Inawezekana dunia ina maji mengi kuliko yaliyogunduliwa na wanasayansi?
 
Back
Top Bottom