Kuna ushahidi wowote wa kimazingira kuwa gharika ya Nuhu ilitokea?

Kuna ushahidi wowote wa kimazingira kuwa gharika ya Nuhu ilitokea?

Dunia ina zaidi ya miaka bilioni 4.5 so kuwa na traces kwa miaka elfu 6 iliyopita ni ngumu kwasababu hata vitu villivyotokoea mwaka 1800 hatuna labda kidogo mwaka 1900 na kuendelea.
Kisayansi, ushahidi wa magharika upo hata magharika yaliyotokea enzi za dinosaurs miaka mamilioni yaliyopita upo ila hakuna ushahidi wa kuwepo gharika lililotokana na mvua kubwa iliyonyesha dunia nzima kwa wakati mmoja. Hivyo inawezekana kuna gharika lilipiga eneo dogo tu ambalo binadamu wengi waliishi enzi hizo ndio ikazaliwa story ya Noahs ark.
 
Mwanzo 9:13-15 BHN​

BHNSUVNenoSRUV
Naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia. Kila nitakapoifunika dunia kwa mawingu, na huo upinde wa mvua utakapoonekana katika mawingu, nitalikumbuka agano langu nanyi na viumbe vyote hai. Kamwe maji hayatageuka kuwa gharika ya kuviangamiza viumbe vyote hai.

Maana yake Mungu aliahidi kutoiangamiza tena dunia kama mwanzo, mnabishanaga bila kusoma maandiko ilimradi tafrani tu!
Maandiko sio ushahidi wa kisayansi, biblia ni kwa ajili ya mambo ya kiroho sio kisayansi ndio maana kuna watu walifufuliwa ilihali kikawaida haiwezekani. Mfano mwandishi wa kitabu cha Mwanzo anasema Mungu alitenganisha maji mengine yakabaki duniani kama bahari na mengine yakawekwa angani (sio mawingu) je ni kweli?

Usichanganya bible na science
 
Sawa mtumishi
 
Kisayansi ni ngumu kuthibitisha hilo kwa maana kwa mujibu wa maandiko ni kama dunia nzima ilijazwa na maji and if so basi lazima katika point fulani duniani kote kungekua na layer fulani ya aina moja au yenye tabia zinazofanana yenye kuonesha kwamba kweli Dunia ilikumbwa na hilo tukio katika wakati mmoja.

Now ushahidi uliopo mwingi inaonesha ukanda mmoja tu na wala sio Dunia nzima.

Ila pia kuna hoja ya kwamba baada ya tukio hilo Dunia ni kama ilijireset na kurudi ikiwa kwenye hali ya tofauti coz hata pores zilibadilika kutoka kwenye ule uumbaji wa awali, kwahiyo kinachoonekana ndicho tulichoanza nacho sisi ila hapo kabla Dunia ambavyo ilikua hatujui.

Kwa maana hiyo basi, hiyo hoja ya ushahidi wa kikanda inawezekana iko na ukweli endapo kama baada ya lile tukio dunia ilibadilika mazima, kwa maana hayo mabadiliko inawezekana yalileta nyongeza fulani ambazo mwanzo hazikuwepo, ndio maana by default utaona now kuna hatihati ya bara la Africa kugawanyika kwa maana bahari itaenda kuligawa katika pande mbili, lakini si tu mara la Africa ila kuna visiwa vingi ambavyo miaka mingi ijayo havitaendelea kuwepo, kwa maana dunia inajirudi kwenye ile hali yake ya asili kutoka kwenye ule uumbaji wa awali.

Kwahiyo ni ngumu kusema kwamba ni tukio ambalo liliwahi kutokea kweli au halikuwahi kutokea kwasababu katika upande wowote utakaousimamia katika mjadala huu ni ngumu kufikia muafaka ambao Kila mtu atatoka ameridhika nao.
Gharika ya Nuhu haikuwahi kotukea kwa sababu
1. Hakuna ushahidi wowote wa Kisayansi
2. Hakuna maji ya kutosha duniani kutengeneza gharika ya kufunika hadi milima( gharika ya aina hiyo inakadiriwa ingehitaji maji mara nne ya yaliyopo duniani)
3. Isingewezekana wanyama wote wanaosemwa kuwekwa kwenye safina kutoka kote duniani
4. Samaki wote wangekufa baada ya maji baridi na maji chumvi kuchanganyikana.
5. Hoja ya ulimwengu kujiresti haiwezi kuwa na mashiko pia kwa sababu ukienda kwa historia ya Biblia binadamu Tangu Nuhu mpaka sasa ni miaka takribani elfu nane wakati wana historia wana ushahidi wa archeological na anthropological wa zaidi ya miaka laki tatu na huko kote hakuna ushahidi wa gharika ya Nuhu au gharika za myths nyingine kama epic of Gilgamesh, Sumerian au za Kihindu.
 
Gharika ya Noah haikuwahi kotokea kwa sababu
1. Hakuna ushahidi wowote wa Kisayansi
2. Hakuna maji ya kutosha duniani kutengeneza gharika ya kufunika hadi milima( gharika ya aina hiyo inakadiriwa ingehitaji maji mara nne ya yaliyopo duniani)
3. Isingewezekana wanyama wote wanaosemwa kuwekwa kwenye safina kutoka kote duniani
4. Samaki wote wangekufa baada ya maji baridi na maji chumvi kuchanganyikana.
Ni sawa ila ushahidi wa kisayansi ndio nini? Maana ushahidi wa kisayansi usipokuwepo haimaanishi kitu hakipo au hakijawahi kuwepo kwasababu sayansi yenyewe ni history iliyokataa kuwa historia.

Maji ya dunia hayatoshi inawezekana ni kweli ila hilo gharika halikuletwa na maji ya dunia isipokua hilo andiko ukilisoma linasema mvua ilinyesha usiku na mchana ndani ya siku 40 katika kiwango kile kile.

Hapo kwenye wanyama pia huwezi kusema haiwezekani moja kwa moja kwa maana kuna watu wako na zuu zenye wanyama kadha wa kadha na Mimi na wewe hatujui hiyo safina ilikua na ukubwa gani.

Hakuna kiumbe chochote ambacho kilibaki hai baada ya lile tukio kwa maana maji yalikaa juu ya ardhi siku 150, so ni kweli hata hao samaki yawezekana walikufa.
 
Unaweza kuachana na maneno ushahidi wa Kisayansi badala yake iwe hakuna ushahidi "wowote".

Utahitaji assumptions nyingi sana ili kuifanya story ya gharika ya Nuhu iwe kweli. Utahitaji kusema Nuhu alibeba mazao na mbegu zote kama Mahindi, Maharage, ngano, viazi n.k katika safina yake maana visingeweza kuvumilia gharika ya wiki tu achilia mbali siku arobaini. Utahitaji kusema maji yalioingia duniani kimiujiza yalipotelea ardhini au kutoweka nje ya dunia kimiujiza pia, Utahitaji kusema Nuhu alipeleka meli za kubeba wanyama, ndege, nyoka, mijusi, wadudu na samaki kutoka America zote mbili, Australia, Africa na Indonesia . Kiufupi utahitajika kusema kitu chochote tu ilimradi hiyo story iweze kushika.

Ili hiyo story iwe kweli inahitaji kuamini ni muujiza tu kama ule wa Muhamad wa mwezi kupasuka katikati na kujirudia.

Ukubwa wa Safina ya Nuhu unajulikana, ni square meters 8900, hata evangelicals wa huko US wamejenga kitu kama hicho kinaitwa Arc Encounter.
 
Hakuna ushahidi. Possibly hiyo gharika ilitokea eneo dogo tu uko middle east. Waandishi wa hilo andiko either walikua na ajenda zao au hawakujua kama dunia inaendelea uko nje ya makazi yao ndio wakaandika hiyo story.
 
Billion 18 kijana
Weka source yako mkuu.

Weka maji mdomoni wakati wa jua halafu yateme kwa kuyasambaza kwa kasi , huo upinde utauona je ni ahadi kuwa hayo maji uliyoyaweka mdomoni hayataleta mafuriko?
Usimtese sana, atafute Spray pump kama zile za Salon atie maji upulize hivyo kuelekea usawa wa mwanga wa jua afu aobserve mchongo wa Nuhu.
 
Back
Top Bottom