sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Katika ulimwengu huu wa sasa teknolojia imekua kubwa, baadhi ya vijana wamejiajiri katika blogging, youtube, n.k.
kwa hapa kwetu wapo a aina mbili
Aina ya kwanza - kwa upande wa bloggers wengi bado wapo google adsense lakini wengi wao wanacheza wanapokea laki 2 jadi laki 8 kwa mwezi, hali hii imefanya wengi kuhamia youtube kwenye nafuu, kuna kipindi youtube ilimpa millard ayo mkwaja mrefu miaka ya 2013 hadi 2015 alikuwa anapiga views kijiji ila saizi ushindani ni mkubwa na pia mabando yamepanda bei ni changamoto kiasi, pia kuna adsense ya kwenye apps nayo imetulia maana ushindani ni mdogo ukilenga penye uhitaji unaogelea pesa.
Aina ya pili - hawa wanatengeneza blog hata haina mpangilio inakuwa na kitufe ambacho mtu akiminya pesa imeingia, wanashare link za blog zao kwa kutegesha picha zinazoshawishi kuminya kwenye makundi ya facebook ili mtu aingie kwenye blog zao aende kuminya sehemu ambayo inawaingizia pesa, mfano kwenye group la fb unakutana na picha ambayo iliyopachikwa kitufe cha video, kwa akili yako unadhani hio ni video, utaminya hapo utapelekwa kwenye blog ambayo ina picha ile ile uliyoina, unaminya hio picha ukidhani ni video kumbe imepachikwa link ya tangazo, hapo tayari ukiminya blogger kapiga pesa.. kindi hili wanapiga hadi milioni 20 kwa mwezi, adsense walipowastukia mchezo wao wakahamia propeller ads, huko nako wakazinguliwa wakahamia adsterra, wakazinguliwa hiko kwa sasa wapo gg agency, mtu analaza laki 6 kila siku utadhani mchezo.
miaka hiyo wakiwa google adsense ikifika tarehe 22 ndio ilikuwa siku ya malipo, unakuta dogo ana miaka 19 amaenda kuchukua milioni 4 na upuuzi kwenye lile dirisha la kupokea hela kwa western union, hapo walikuwa wanapiga milioni 4.x kwa maksudi maana ilikuwa ukizidisha hapo basi western union inakua ngumu kutoa hela, sasa hao bloggers wakaja kufanya uchunguzi wa kuruka hicho kiunzi ndio wakajua kuna njia ya bank transfer inayorusu kutoa pesa zaidi na pesa zinaingia moja kwa moja benki,
Hii watu walikuwa wanapiga milioni 20 kila mwezi, benki pendwa ilikuwa ni Equity Bank ambayo waliweza kuungansha hio njia ya bank transfer, watu wa bank walikuwa wanashangaa sana. Mpaka sasa watu wanaendelea kupiga dollar ila wamehamia gg agency huko naskia wanalipa kwa bitcoins then unaziuza na kuzibadili ziwe tshs kwa watu wanaonunua bitcoins sehmu kama Remitano, Coinbase, n.k.
Huku mtu akikusikia anaweza kuona ni rahisi ila asikwambie mtu huku mambo yanabadilka sana, njia ikianz kutumika leo kupiga dollar unakuta inakaa miezi sita tu baada ya hapo ishachuja, hizi njia wanaziita "triki", ili kupata hizo triki inabidi uwe na marafiki wa vikundi tofauti vya bloggers hawa maana nao huwa wana vikundi vyao na pia uwe na pesa ya kulipia kufundishwa hizo triki, triki zinauzwa mpaka milioni huko.
Pia kuna visasi na umafia wa hali ya juu sana, unakuta kuna wale waliokuwa wananyimwa triki, wamepambana wakapata triki zao wakaanza kupiga dollar, hizo triki huwa hawawapi waliowanyima enzi hizo, kazi inakuwa ni kuposti kwenye magroup yao ya whatsapp dollar wanazopiga ila hawatoi mbinu, hii kitu huwa inakasirisha sana wale waliowanyimaga triki, kuna bloggers walikuwa wanalaza dolla za kutosha miaka ya 2015 lakini baada ya triki zao kuchujaleo hii wanatia huruma uchumi umeyumba, so huku hkunaga uhakika wa kesho.
Binafsi nilikuwa natamani huko sehemu ya pili ila ilishindikana kwasababu zangu binafsi kulingana na kazi ilivyo.
HITIMISHO:
Kundi la kwanza kuna uhakika na usalama, mambo yapo wazi ila linahitaji juhudi na uvumilivu sana maana unaweza kuanza kupiga hela ya maana kidogo baada ya msoto wa miaka mitatu., baada ya hapo inaweza kuwa kazi rasmi ya kuitegemea kukuingizia kipato kwa miaka ijayo.
kundi la pili hilo halina uhakika maana mambo yanaenda kwa triki ambazo hazipo wazi na huwa zinafungiwa sana, yaani kufumba na kufumbua triki inaweza kupigwa pini. Uzuri wake ni kwamba ukiwa na hio ramani utapiga pesa nyingi tu, ila ndio hivyo tena, trick kwa tafsiri yake ni kutoka kiingereza ni ujanja, hizo janja janja huwa hazidumu, wapo watu waliokula maisha mithiri ya peponi miaka ya juzi tu hapo 2018 lakini kwa sasa wana maisha magumu ambayo yamegeuka kuwa furaha kwa wale waliokuwa wakiwanyima hizo triki, ni umafia na visasi, na hawa ambao miaka hii wameotea mbinu si ajabu miaka ya mbele yakawakuta.