Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nasikia Wanigeria kwa utapeli ndio wanaongoza eti
Umemalizaje hapo misonisondoo?Kuna utapeli mpya bila shaka ni wanaigeria Kuna kitu linaitwa task mtu yupo tayari akutumia hata laki bure ila ukijaa lazima uliwe🤣🤣
Kuna jamaa yangu alikuwa anapitia kipindi kigumu maisha kupewa fursa ya task akahisi ni Mungu amemshushia neema kutumiwa pesa za bure kumbe wajuba wapo kazini nao haya maisha🤣🤣
Mkuu nielekeze jins ya kupata hizo taskWakiingia 18 zangu lazima niwavue chupi..))
Naipataje hiyo mkuu,nataka nichukue hela yako kisha nasepaNdio ,kufungua hizo videos ,kulike na kusubscribe accounts za YouTube , a nonsensical task
Atakayepigwa naye zoba
Hakuna kitu kipya duniani ila mambo yanakuwa updated kila siku kufanya watu ndio mana zimekuja zile ishu za kununua saa kwa million 4 watu wamepigwa kuna deci,forex,kalyinda watu wamepigwaSasa hapo kuna upya wowote ? Hizo ni long Con mtu anawekeza hata mwaka mzima anakupanga ili mwisho wa siku akumalize...
Nilifuatilia nione wanavyopiga, kwanza wakanipa demo halafu wakanitumia afutatu baada ya hapo nikaungwa kwenye group ambalo task zinapitia na kazi ni kuweka tiki za like katika YouTube video.Ndio ,kufungua hizo videos ,kulike na kusubscribe accounts za YouTube , a nonsensical task
Atakayepigwa naye zoba
Nipo kwenye task moja hapa nimeshatumiwa kama 10k nipo kwenye hatua ya mwisho hapa natakiwa kujiunga na app yao ili nitumiwe tena elfu 40 baada ya hapo sijui Nini kinafuata 🤣🤣Nilifuatilia nione wanavyopiga, kwanza wakanipa demo halafu wakanitumia afutatu baada ya hapo nikaungwa kwenye group ambalo task zinapitia na kazi ni kuweka tiki za like katika YouTube video.
Unapewa point na kila point ina value ya 500 tshs. Kukutamanisha wanakwambia wekeza commission ili uongeze mpunga wako ndani ya masaa machache tu. Hapa ndio mtego ulipo Wanatuma screeshot za watu waliotumiwa miamala baada ya kuwekeza.
Hakuna pesa za bure watu wafanye kazi, Watanganyika wenzangu maendeleo hayaji bila kutoka jasho kweri kweri.