Kuna uwezakano muumba ulimwengu aliacha kuingilia mambo ya ulimwengu aliouumba?

Mbona hushangai huyo Mungu kutokea mwenyewe tu?
Kwani Mungu katokea πŸ™„ kama katokea basi siku aliyo tokea ndiyo mwanzo ....mungu awezikuwa na mwanzo ...kwa sababu mungu na vyote ni roho(energy) vipo milele hata kisayansi ni hivyo hivyo inavyo sema kuhusu ENERGY...sasa mungu ni nini ? Mungu ni UFAHAMU WA HIYO ENERGY YOTE KWA UJUMLA WAKE huo ufahamu (nafsi)ndiyo mungu ...sisi na vitu vyote vipo ndani ya mungu hivyo ni sehemu ya mungu .
 
Ninyi watu acheni kuwa wapumbavu. Mtu maana yake ni nini?
 
Kwamba aliuumba ulimwengu kisha akaamua kukaa kando kuutazama unavyojiendesha na kujiendea wenyewe tu bila yeye kuingilia kwa namna yoyote au chochote

Hilo ndilo jibu haswaa. Km yupo hana time tena na hii Dunia. Tupambane tu na hali zetu..
 
Sasa ndo alete majanga ya mafuriko, radi, vimbunga viue watu wasiyo na hatia? Anapata faida gani watu wakifa kwa mateso ya hayo majanga? Mana Mambo km Vita utajitetea yanasababishwa na wanadamu wenyewe.
 
Adhabu Ya Kutokutii

Walawi 26:14 β€œβ€†β€˜Lakini kama hamtanisikiliza na kutimiza maagizo haya yote, 15 nanyi kama mtazikataa amri zangu na kuzichukia sheria zangu, tena mkishindwa kutimiza amri zangu na hivyo mkavunja agano langu, 16 ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kufisha, na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila mafanikio, kwa sababu adui zenu wataila. 17 Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.
18 β€œβ€†β€˜Kama baada ya haya yote hamtanisikiliza, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. 19 Nitakivunja kiburi chenu cha ukaidi na kuifanya anga iliyo juu yenu iwe kama chuma, na ardhi yenu kama shaba. 20 Nguvu zenu zitatumika bila ya mafanikio, kwa sababu ardhi yenu haitawazalia mazao yake, wala miti ya nchi yenu haitazaa matunda yake.
21 β€œβ€†β€˜Kama mtaendelea kuwa na uadui nami, na kukataa kunisikiliza, nitawazidishia mateso yenu mara saba zaidi, kama dhambi zenu zinavyostahili. 22 Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ngΚΌombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.
 
Wafia dini watakuambia Mungu kaweka huo ubaya kwa malengo yake. Yaani atese watu kwa malengo yake? Huyo ni Mungu gani? Ndio maana nimeachana na huyu Mungu wa Israel na kujikita katika jadi yangu.
 
Hakuna wazo la peke yako mkuu hata huyo Kiranga nae kuna sehem anapata mawazo yake ko hakuna copy and pest maaa kila kilichopo Duniani kilishawahi kuwepo
Hizi mada zilikuwapo kabla wote hatujazaliwa.

Pia, hata copy oaste si tatizo. Tujadili mantiki ya mada, si mada imetoka kwa nani.

Mada nzuri itakuwa nzuri tu bila kujali imetoka kwa nani, na mbaya hivyo hivyo.

Tujadili mada, si mtoa mada nani.
 
Roho inahitaji Imani,Nafsi inahitaji Maarifa, Mwili unahitaji chakula... unataka nini Tena kwa Mungu..mbona kama unakuwa mkorofi tu bila SABABU
 
Kuna maswali ukianza kujiuliza utajikuta Kichwa kinauma
 
Kila kitu kiliwekewa solution mkuu hapa duniani..Tatizo Watu wanaofikiri kwa kina wamekua wachache sana siku hizi .
 
Wewe umejuaje kuwa ana nguvu zote na anakanuni zake?
 
Yani mnafanya ujinga wenyewe hapa Duniani alafu mnamsingizia Mungu

Amekuumbeni Kisha skakuwekeeni kanuni jinsi ya kuishi hapa Duniani mmeacha kufuata hizo kanuni lazima mteseke
 
Unapochunguza dunia huwezi pinga juu ya uumbaji Bali kwa haraka haraka unaweza dhani kwamba huenda Mungu hakuimalizia kazi yake ndo sababu tunakufa nk.

Maandiko yanatanabaisha juu ya fikra hii kuwa Ni potofu. Matokeo ya maumivu kwenye maisha sio kwamba Mungu haoni, au labda ana roho mbaya sana, hasha! Bali Ni misingi au kanuni ambazo amejiwekea. Sio kwamba Hana uwezo nayo hapana isipokuwa kutokana na madhara anayoyaona yeye na si Kama tuonavyo sisi.

Mf. Kiu yetu ni Mungu ajidhihirishe ili tupate kuwa na uhakika wa yule tunayemwabudu. Lkn kwa upande wake anasema" hakuna mwanadamu alieniona akaishi" Sasa hapo wewe mwenyewe utaona afadhali Ni ipi , umuone usiishi au kuendelea kwakutokumuona.

Vilevile upande wa maumivu haya na majanga mbalimbali maishani.
Kuna Jambo ambalo Mungu aliliepuka kwa kuifungia dhambi kwenye Siri ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ili yasije kutuathiri.
Na hapa faida yake mwanadamu anaweza asiione maana haimuhusu lakini Mungu alilinda ufalme wake na enzi yake. Maana ilikuwa Ni heri kwa kifo Cha mwanadamu kutokea kuliko ufalme wake uvunjike.

Baada ya sisi kuifungulia dhambi ndipo Mungu anatafuta njia nyingine ambayo haitamuathiri yeye Wala sisi kwa kupitia yesu kristo.
Lkn pamoja na njia hiyo, bado haiondoi uwepo wa maumivu maishani. Isipokuwa usipomuamini yesu utahesabika adui wa Mungu. Na unapokuwa adui yake basi tarajia hayo majanga yote yaliyoorodheshwa na mtoa mada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…