Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kila siku hapa duniani kuna habari mbaya za kuteseka kwa binadamu fulani kwa magonjwa, vita, njaa, dhuluma, umaskini n.k kwa viwango tofauti, kuanzia viwango vidogo hadi vikubwa kabisa vya kutisha na kufadhaisha sana
Ni vigumu sana kuelewa kwa nini anayesemwa ana nguvu zote;
Asizue mtoto albino kutekwa, kuuwawa na kukatwa viungo vyake, Asizue watoto kufa vitani Congo, Gaza, Ukraine na kwingine kwingi
Asizue cancer,
Asizuie ubakaji na ulawiti
Asizuie dhuluma za kila aina
Asizue umasikini
Asizue ajali
Asizuie utumwa
Asizuie utapeli wa kidini
Asizuie majanga ya asili
Sasa kwa kuwa ni vigumu sana kuamini ulimwengu ulitokeza au umekuwepo tu bila muumbaji, Je inawezekana muumbaji aliyeuumba ulimwengu aliamua kuuacha ujiendeshe wenyewe tu kwa nguvu na kanuni za asili?
Kwamba aliuumba ulimwengu kisha akaamua kukaa kando kuutazama unavyojiendesha na kujiendea wenyewe tu bila yeye kuingilia kwa namna yoyote au chochote