Kuna uwezekano 2020 tukapata viongozi wabovu sana!

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
4,418
Reaction score
4,031
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita umetoa funzo. Kuna viongozi wamepita bila kupingwa ila baadae kidogo wananchi wamewakataa na wengine wamejiuzulu kwa kukosa support ya wananchi.

Dosari za uchaguzi huo, zilibainishwa na Mh. Jafo ambaye ni Waziri wa TAMISEMI na mwenye dhamana.

Aidha, Uchaguzi huu Mkuu wa 2020, Wakurugenzi walewale ndo wanatarajiwa kusimamia chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hadi naandika thread hii, niko tiyari kusahihishwa,sijasikia Mkurugenzi au Kiongozi aliyewajibishwa au kujiuzulu kwa uzembe ule uliofanyika.

Mimi ni Mtanzania na mpenda amani. Kwa interest ya wasomaji,mimi ni mwanachama hai wa CCM.

Leo wakati napitia habari mbalimbali ktk mitandao yetu nimekutana na uzi unaomnukuu Katibu Mkuu wangu wa Chama ukisema "Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020".

Kiujumla hii statement imenifikirisha kiasi fulani,ukizingatia kauli hii inakinzana na ile ya Mh. Jafo kuwa dosari zilikuwa ni nyingi hadi akafuta teuzi na kuamua kila aliyejaza fomu apigiwe kura.

Hofu yangu ni pale Katibu wangu Mkuu anapotamka mbinu bila kuweka bayana ni mbinu zipi! Huku akijua wazi 99% ya ushindi tuliopata ulitokana na wenzetu kujitoa na siyo mapenzi halisi ya wapiga kura! Na je, hizo mbinu zitafanana na zile zilizoendana na ushindani usio sawa?

Je, Katibu wangu hajui kabisa ni nini kilipelekea tukapata ushindi wa kishindo? Endapo anajua,haoni kuna uwezekano tukapata Wabunge goigoi kwa vile wengi watapita bila Sanduku la kura?
 
Hakuna Uchaguzi bila Tume huru ya uchaguzi. Tunataka hata CCM wakishinda washinde chini ya tume huru kwa uchaguzi huru na haki kabisa.
Huyo Bashiru acha ajidanganye, sisi tumeamua hakuna uchaguzi bila tume hiyo. Ndio, sisi wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisusa hakikisha hauna njaa bila hivyo utatamani kula makombo ya wenzako wakati chakula kimeisha.
 
Yajayo hayafurahishi
IMG_20200113_222112.jpeg

Sent using iPhone
 
Mfa maji haishi kutapatapa, kweli ccm imeshakufa ikaacha bunduki juu ya kaburi lake. Misukule ya ccm inatumia bunduki hiyo kuwatisha watz.
 
Kididimo,
Bashiru hajui uchaguzi wa 2020 utakuwa chini ya microscopic observation ya EU na US.

this time the western world hawawezi kurudia makosa waliyoyafanya kwa Mugabe - ya kuacha Udikteta utamalaki kwa zaidi ya 5 yrs.

kuna uwezekano mtu akanyofolewa kiotani na CIA!
 
Inaonesha unafaham CCM inafanya dhulma naww unajipambanua kuwa mwenzao bila kuona aibu... wewe na wenzio kama wewe ndiyo mnaanzisha,mnachochea na kuiunga Dhulma inayoendelea bora utulie kimya. Kama huelewi baba wa dhulma ni shetani so nijuu yako kumfanyia kazi ama la.
 
Jiwe ajiandae kwenda chattels kulima pamba hata kama MWENYEKITI wa tume atakua mamaake
 
Hakuna Uchaguzi bila Tume huru ya Uchaguzi. Tunataka hata CCM wakishinda washinde chini ya tume huru kwa uchaguzi huru na haki kabisa.

Huyo Bashiru acha ajidanganye, sisi tumeamua hakuna uchaguzi bila tume hiyo. Ndio, sisi wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
MUNGU wangu hapo ndo mtakuwa mmejipalia mkaa wenyewe unajua kisheria unapokataa uchaguzi kinachofuata nn

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh mbinu zile zile ndio maana Mimi sina mpango wowote wakupiga kura nahisi ntapoteza muda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana. Ni vizuri kutumia haki yako ya msingi.
Inaonesha unafaham CCM inafanya dhulma naww unajipambanua kuwa mwenzao bila kuona aibu... wewe na wenzio kama wewe ndiyo mnaanzisha,mnachochea na kuiunga Dhulma inayoendelea bora utulie kimya. Kama huelewi baba wa dhulma ni shetani so nijuu yako kumfanyia kazi ama la.
 
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita umetoa funzo. Kuna viongozi wamepita bila kupingwa ila baadae kidogo wananchi wamewakataa na wengine wamejiuzulu kwa kukosa support ya wananchi.

Dosari za uchaguzi huo, zilibainishwa na Mh. Jafo ambaye ni Waziri wa TAMISEMI na mwenye dhamana.

Aidha, Uchaguzi huu Mkuu wa 2020, Wakurugenzi walewale ndo wanatarajiwa kusimamia chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hadi naandika thread hii, niko tiyari kusahihishwa,sijasikia Mkurugenzi au Kiongozi aliyewajibishwa au kujiuzulu kwa uzembe ule uliofanyika.

Mimi ni Mtanzania na mpenda amani. Kwa interest ya wasomaji,mimi ni mwanachama hai wa CCM.

Leo wakati napitia habari mbalimbali ktk mitandao yetu nimekutana na uzi unaomnukuu Katibu Mkuu wangu wa Chama ukisema "Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020".

Kiujumla hii statement imenifikirisha kiasi fulani,ukizingatia kauli hii inakinzana na ile ya Mh. Jafo kuwa dosari zilikuwa ni nyingi hadi akafuta teuzi na kuamua kila aliyejaza fomu apigiwe kura.

Hofu yangu ni pale Katibu wangu Mkuu anapotamka mbinu bila kuweka bayana ni mbinu zipi! Huku akijua wazi 99% ya ushindi tuliopata ulitokana na wenzetu kujitoa na siyo mapenzi halisi ya wapiga kura! Na je, hizo mbinu zitafanana na zile zilizoendana na ushindani usio sawa?

Je, Katibu wangu hajui kabisa ni nini kilipelekea tukapata ushindi wa kishindo? Endapo anajua,haoni kuna uwezekano tukapata Wabunge goigoi kwa vile wengi watapita bila Sanduku la kura?
Hata waliopo madarakani kwa sasa ni wabovu kupindukia.Hata hadhi ya kuitwa "waheshimiwa" hawana! Ni matikiti maji tupu.
 
Sio uwezekano 2020 kupata viongozi wabovu, nchi hii hatujawahi kupata viongozi wasio wabovu. Ni tamaduni yetu kupata viongozi wasiojiweza kiakili na kifikra.
Kule shinyanga Kuna mwenyekiti wamtaa wa ajabu sana
 
"Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020".
Dokta amekuwa muwazi, mikakati ya ushindi wa CCM sio uwepo wa, Bombadia, SGR, Mahakama Chattle, Ujenzi wa Mabwa ya Umeme, Viwanda 40000 na vitu vingine, bali ni CCM kuwa chama Dola.
 
Boss Kididimo Mimi binafsi .. hii kitu ya ... Kupita bila kupingwa ... sikipendi aka sikiafiki. Maana haileti ushindani bora. Sijui kwa nini CCM na Watawala wanaogopa ushindani bora. Ushindani bora siku zote huleta Maendeleo bora.

Bila Upinzania madhubuti na bora, tusahau kitu Maendeleo. Na maendeleo yataletwa na Wananchi na Watanzania.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopita umetoa funzo. Kuna viongozi wamepita bila kupingwa ila baadae kidogo wananchi wamewakataa na wengine wamejiuzulu kwa kukosa support ya wananchi.

Dosari za uchaguzi huo, zilibainishwa na Mh. Jafo ambaye ni Waziri wa TAMISEMI na mwenye dhamana.

Aidha, Uchaguzi huu Mkuu wa 2020, Wakurugenzi walewale ndo wanatarajiwa kusimamia chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hadi naandika thread hii, niko tiyari kusahihishwa,sijasikia Mkurugenzi au Kiongozi aliyewajibishwa au kujiuzulu kwa uzembe ule uliofanyika.

Mimi ni Mtanzania na mpenda amani. Kwa interest ya wasomaji,mimi ni mwanachama hai wa CCM.

Leo wakati napitia habari mbalimbali ktk mitandao yetu nimekutana na uzi unaomnukuu Katibu Mkuu wangu wa Chama ukisema "Dr. Bashiru: Mbinu na mikakati tuliyotumia kupata ushindi wa 99% kwenye Serikali za mitaa ndizo tutakazotumia uchaguzi mkuu 2020".

Kiujumla hii statement imenifikirisha kiasi fulani,ukizingatia kauli hii inakinzana na ile ya Mh. Jafo kuwa dosari zilikuwa ni nyingi hadi akafuta teuzi na kuamua kila aliyejaza fomu apigiwe kura.

Hofu yangu ni pale Katibu wangu Mkuu anapotamka mbinu bila kuweka bayana ni mbinu zipi! Huku akijua wazi 99% ya ushindi tuliopata ulitokana na wenzetu kujitoa na siyo mapenzi halisi ya wapiga kura! Na je, hizo mbinu zitafanana na zile zilizoendana na ushindani usio sawa?

Je, Katibu wangu hajui kabisa ni nini kilipelekea tukapata ushindi wa kishindo? Endapo anajua,haoni kuna uwezekano tukapata Wabunge goigoi kwa vile wengi watapita bila Sanduku la kura?
 
Boss Kididimo Mimi binafsi .. hii kitu ya ... Kupita bila kupingwa ... sikipendi aka sikiafiki. Maana haileti ushindani bora. Sijui kwa nini CCM na Watawala wanaogopa ushindani bora. Ushindani bora siku zote huleta Maendeleo bora.

Bila Upinzania madhubuti na bora, tusahau kitu Maendeleo. Na maendeleo yataletwa na Wananchi na Watanzania.
Kuna mahali tutafika, tukajikuta tuna viongozi wa kuteuliwa tuu! Chama chetu cha CCM hakikuhitaji viongozi " academicians" wanaozunguka nchini bila mbinu ya kuunganisha watu!!! Unapomchagulia mwananchi kiongozi asiyemtaka unaleta utengano!!! Hata zamani enzi za Mwl. Nyerere, kulikuwa na kura za NDIYO au HAPANA pale ilipotokea kuwa na mgombea mmoja. Kuna waliopata kura nyingi za HAPANA! na wananchi wakaridhika.
 
Back
Top Bottom