Kuna uwezekano 2020 tukapata viongozi wabovu sana!

huyo kiongozi mnaomataka nyie ni nan hana ubovu wake?
 
Haijalishi kabisa kuwa wewe ni mwana CCM au ni mpinzani. Jambo la mhimu hapa ni Tanzania, ambayo sote ni yetu.

Umeandika vizuri sana; na ninajua wamo ndani ya CCM walio na mawazo kama haya yako, hata kama ni wachache.

Ni jukumu lenu huko huko CCM mtafute njia ya kulinusuru taifa letu na balaa hili linalotunyemelea. Viongozi wenu, kama huyo Katibu wenu kila akipanua mdomo, harufu chafu inatoka, hata haoni umhimu wa kujisetiri na aibu ya maneno anayoyatoa mdomoni. Sijui anayasema maneno hayo kumpendeza nani, nyinyi wanachama wake?

Mwelezeni, yeye na viongozi wenzake wanaofurahishwa na hali hii wanaliweka taifa letu kwenye majaribu makubwa. Kauli zao hizi zinaweza zikatumiwa kama ushahidi endapo kama vurugu zitatokea kwa sababu ya tamaa zao za kutaka kutuongoza kwa mabavu.
 
Huyo Bashiru acha ajidanganye, sisi tumeamua hakuna uchaguzi bila tume hiyo. Ndio, sisi wananchi.

S
Napenda kukuunga mkono mkuu 'Chakaza', ila sijui maana hasa unayolenga kwa maneno haya uliyoyatumia:
"...sisi tumeamua hakuna uchaguzi bila tume hiyo"
Itapendeza sana ikiwa hivyo hasa.

Lakini kama maana yake ni kama ile iliyofanyika kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, yaani kwa vyama vya upinzani kususia uchaguzi huo, basi hapo maana inakuwa imepotea.

Hapo mwisho wa sentensi yako umewahusisha wananchi, "ndio sisi wananchi", nikitumai ni wananchi watakao uzuia uchaguzi usifanyike , na wala sio wao kususia tu kwa kutokwenda kupiga kura.

Kama maana ya wananchi kuzuia uchaguzi usifanyike, hili linahitaji maandalizi kabambe sana. Sio jambo la kukurupuka tu na kulifanya. Linahitaji uongozi makini. Yote mawili siyaoni, na wakati wake wa kuyafanya ni huu, sasa hivi, sio kuanza kesho au keshokutwa.

Labda unaweza ukaeleza maana yako uliyokusudia kwa kuyaandika maneno hayo.
 
Duuuh mbinu zile zile ndio maana Mimi sina mpango wowote wakupiga kura nahisi ntapoteza muda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kura yako ya HAPANA au kumpigia mpinzani ina thamani kubwa sana kuliko wewe kutojitokeza kutumia haki yako ya kupiga kura.

Nenda kapige kura, ya kuwakataa, mengine waachie wowote watakaokuwa na uthubutu wa kuilinda kura yako isiharibiwe. Kutokwenda kupiga kura kwako kunawanyima watu hao ushahidi wanaoweza kuutumia kuwaondoa hao wanaokulazimisha wakuongoze bila ya idhini yako.
 
huyo kiongozi mnaomataka nyie ni nan hana ubovu wake?
Mkuu, haya mambo yanatuhusu sote. Mwl. Nyerere aliwahi kusema" Kiongozi bora ni yule anayekubali kukosolewa kwenye mambo ya msingi".
 
Sisi tunaamua lakini bado tunapaswa kushinikiza vyama vyetu kutopeleka majina ya wagombea.
Tofauti na uchaguzi wa SM ambao ulikuwa ni lazima ujiandikishe kwanza, huu tayari tumejiandikisha lakini kama hakuna chama kitapeleka majina hautakuwa uchaguzi.
Na ni vema vile vyama puppet kutambua kuwa kupeleka jina LA MTU ni kumhatarishia maisha.
Ndipo uchaguzi mkuu utakao kuwa na mgombea Urais pekee, wabunge pekee na madiwani pekee wa CCM utakuwaje.
Bado sisi (wananchi) tunahitaji umahiri wa viongozi wa kisiasa kuli ongoza hili bila utani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hawa waliopo ni wabovu mno
 
Umejaribu, lakini bado hujanishawishi mkuu wangu Chakaza kwa haya uliyoweka hapa.

Maana ya hii ni kwamba CCM na vibaraka wao bado watakuwa wamefanya uchaguzi kwa niaba ya sisi wengine wote.

Ya nini kuendelea kulembalemba jambo ambalo liko wazi?

Kama hatutaki pawe na uchaguzi ni kuzuia uchaguzi wa aina yoyote ile, hata huo wa CCM wenyewe usifanyike.

Ikiwezekana kuwashawishi wananchi walikubali hilo, tutakuwa tumeukata mzizi wa fitna wote.

Kazi ngumu ni hiyo, ya kuwaelimisha wananchi wachukue madaraka yao.

Ni nani ataifanya kazi hiyo?
 
Pamoja nchi ya uganda kutajwa kuwa kiongozi wake amekaa muda mrefu madarakani lakini yeye uwa aingilii chaguzi zilizo chini yake .Yuko resilient kuruhusu chaguzi kama serikali za mitaa madiwani na wabunge wananchi wanachaguwa viongozi wao wanaowataka bila ya figisufigisu au kutumia nguvu za dola.Halafu katiba ya Uganda inaruhusu matokeo ya Raisi kupingwa Mahakamani .Je sisi Tanzania kwa nini hata mwenyekiti wa kitongoiji /mitaa tunatamani asichaguliwe kupitia debe asimikwe bila kuchaguliwa na wananchi?
 
Mkuu kosa la kutokuwa na tume huru lilipuuzwa na hao wanaotaka tume huru sasa,lakini baada ya kuonja machungu ya ubabaishaji wao kuwa hawafiki kokote bila ya mambo ya msingi.
Tulipoingia siasa vyama vingi enzi za Mzee Ruksa watu mahili kama Mchungaji Mtikila waliliona hilo kuomba vyama vya upinzani wasikubali chaguzi hadi mambo ya msingi kama mgombea binafsi,tume huru yapewe uvumbuzi.Lakini nguvu ya RUZUKU ikakumbatiwa wakasahau maana halisi ya Upinzani ni kuchukuwa Dola
Chaguzi zote 1995,2000,2005,2010,2015.tume huru haikupewa kipa umbele kisa RUZUKU!
Wakasahau kuwa CCM haikupenda vyama vingi bali lilikuwa shindikizo toka nchi za magharibi.
Dynamic ya siasa zimebadirika,China Communist ni Super Power,kwa sasa nchi za Magharibi zina matatizo yao na sio kipaumbele kuhimiza siasa ya vyama vingi kwa nchi za Afrika.
Tume huru itaongozwa na watu,nani anajua roho za wajumbe wa tume,roho zao zitakuwa hazipendelei au kuegemea upande wowote?
 
Mkuu inawezekana kabisa mawazo haya ni mazuri. Tupe the way forward.
 
Onyesheni kama mna dini nasiyo kugandamiza wenzenu wajamii ilele mnapotawala.
 
Haipo popote duniani hii kitu ni kwetu na rwanda tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…