PreGE2025 Kuna uwezekano Askofu Gwajima anamchafua Rais Samia kuelekea Uchaguzi na akitumika na wale watu waliotaka asiwe Rais

PreGE2025 Kuna uwezekano Askofu Gwajima anamchafua Rais Samia kuelekea Uchaguzi na akitumika na wale watu waliotaka asiwe Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Afadhali safari hii umekuwa na akili 1%, ukasema kuna uwezekano, ikionyesha kwa asilimia kubwa zaidi unakiri kwamba alichosema Gwajima ni kweli, ila kwa asilimia fulani ndogo kuna uwezekano anamchafua Raisi.

Lakini hebu tulieni mjiulize swali hili; mbona sijasikia Gwajima akimtaja Raisi? Kwa nini CCM wote mmekata kauli kwamba Gwajima anamsema Raisi?
Kwani wewe ukitumia akili yako kidogo tu unashindwa vipi kuelewa kuwa alimlenga Rais na taasisi ya Urais? Kwani ni nani aliyekuwa anatengua uteuzi wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama zaidi ya Rais Mwenyewe?
 
Gwajima ni mpango mkakati wa ccm kujikosha kimataifa na katumwa na mama mwenyewe afanye hivyo ili ccm waonekane hawapendi vitendo haramu ni mbinu ya kuwahadaa Dunia, hata wabunge wanaompinga Gwajima ni Gelesha tu hawana lolote
Hakuna kitu kama hicho hata kidogo
 
Kuna watu wanamtumia kumhujumu na kumchafua Rais Samia.
Wewe ndo unamchafua zaidi, kadri unavyokazana kumsifia hata kwa maovu yanayofanyika nchini, uuaji, utekaji, ufisadi, uuzwaji wa rasilimali za nchi, yote hayo kwako unaona ni sawa so long as aendelee kuwepo madarakani. Tafsiri yake ni kwamba wananchi hawajawahi kuwa priority yenu isipokua mafanikio yenu Binafsi.
Kwa nini mmefungia mtandao wa X? Kwa nn mmeomba zile documents zote zilizovuja ziondolewe Instagram? Nani amejitokeza kuzitolea maelezo, kama ni za kweli ama la? Ile statement ya benk ya IGP wambura nayo vipi, ya kweli au ya uongo?
Hivi una familia kweli wewe? Na ukirudi nyumbani jioni wanakupa pole kabisa kua umetoka kazini? Na wanajua kazi unayoifanya, na ukilala unapata kabisa usingizi, naomba siku moja ukiwa umelala ujipe hata dk 3 utafakari wale 83+, waliouwawa na kupotezwa walikosea nn, kwa nn wao walitakiwa wafe na wewe uendelee kuishi.
 
Lucas mnatuchanganya sana, sasa kama tayari ccm imempitisha kugombea uchaguzi kuna nini cha kumkwamisha? kilichobaki ni kufanya kampeni na uchaguzi ambao ni dhahiri atashinda. Huyo gwajima ni mwanachama wa ccm na anajua taratibu za chama tayari kimempitisha agombee, kina nani tena wanamtumia gwajima amchafue samia, kwa manafaa gani?
Ungesoma andiko langu upate majibu ya swali lako.
 
Lucas mnatuchanganya sana, sasa kama tayari ccm imempitisha kugombea uchaguzi kuna nini cha kumkwamisha? kilichobaki ni kufanya kampeni na uchaguzi ambao ni dhahiri atashinda. Huyo gwajima ni mwanachama wa ccm na anajua taratibu za chama tayari kimempitisha agombee, kina nani tena wanamtumia gwajima amchafue samia, kwa manafaa gani?
akikujibu unifahamishe..ifike wakati uchama pembeni uzalendo kwanza.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ningependa Kuwaambieni na kuwakumbusheni Ya Kuwa Pamoja na Katiba yetu kuwa wazi na kunyooka kabisa juu ya nini kinapaswa kufanyika pale Rais aliyepo madarakani anapofariki Dunia, Yaani Makamu wa Rais Kuapishwa na kuchukua Madaraka ya Urais kuongoza Nchi.

Lakini ni Lazima Mfahamu ya Kuwa kuna Mambo makubwa ,Mazito ya kuogofya ,Ya Siri yalifanywa au kudhamiliwa kufanywa au kukusudiwa kufanywa na baadhi ya watu kutaka Kupindua Matakwa ya Katiba yetu ili Mama yetu aliyekuwa Ni Makamu wa Rais Asiweze Kuapishwa na kuchukua Madaraka ya Urais Baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli kama inavyoeleza Katiba yetu.

Hapa mnaweza kurejea kauli ,maneno na Mazungumzo ya Jenerali Venance Mabeyo Ambaye alikuwa ni Mkuu wa Majeshi wakati huo. Ambapo Alisema kuwa Kuna watu walisahau matakwa ya katiba na katiba inasema nini baada ya kifo cha Rais aliyepo madarakani. Ambapo anasema na alisema ya kuwa yeye ndiye alifanya kazi ya kuwakumbusha hao watu matakwa ya Katiba.

Kitu nachopenda kuwaambieni ni kuwa hii ni kauli nzito sana kutoka kwa mtu na kiongozi mzito sana ambayo aliitamka kiuongozi. Hapa kwa lugha nyingine waweza kusema kuwa kuna watu au kikundi cha watu kwa sababu zao na maslahi yao walitaka kupindua matakwa ya katiba ili waweke au kusimika mtu wao katika kiti cha Urais baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli kinyume kabisa na matakwa ya katiba yetu.

Kwa hiyo siyo kwamba walikuwa wamejisahau au walikuwa ni wapinga wa sheria na katiba au kwamba walikuwa hawajui katiba inataka nini kifanyike. Walikuwa wanajua kila kitu ila kwa uroho na uchu wa madaraka walitaka wafanye kitendo hicho cha hatari ambacho pengine kingeweza kuhatarisha usalama wa Taifa letu kwa kusababisha machafuko na mgawanyiko ndani ya Taifa letu.

Kwa sababu ni lazima kungezaliwa kambi na mgawanyiko mkubwa sana kuanzia Majeshini ,uongozini hadi uraiani ambapo wengi wangekuwa upande wa katiba yetu kutaka katiba iheshimiwe na kufuatwa kwa Mama Samia kuapishwa kuwa Rais wa NCHI yetu. Hivyo tuna kila sababu ya kumpongeza General Mabeyo kwa Ujasiri na uzalendo wake uliotukuka kabisa wa kusimama imara kulinda katiba yetu kama kiapo chake kinavyo Muelekeza.

Hivyo basi kushindwa kwa jaribio hilo la watu hao la kutaka Kupindua matakwa ya katiba yetu. Bila shaka liliwaumiza,kuwakwaza ,kuwasononesha na kuwachukiza sana watu au kikundi hicho kilichotajwa kufanya jambo hilo la hatari kwa usalama wetu wa Taifa. Hali ambayo bila shaka iliwaacha na kitu kimoja pekee mikononi na vifuani pao. Ambalo ni Dua na Maombi mabaya kwa utawala wa Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Bila shaka waliendelea kuomba Rais wetu ashindwe kuongoza Nchi ,utawala wake uwe wa misukosuko,majanga majanga ,kuchukiwa na wananchi ,vurugu na maandamano ya hapa na pale na mambo mengine mbalimbali mabaya mabaya. Lakini kwa sababu uongozi unatoka kwa Mungu,na kwa kuwa Mungu ndiye hutoa kibali cha uongozi kwa mtu ikawa tofauti sana na matarajio ya hawa watu na hicho kikundi Chenye chuki binafsi kwa Rais wetu.

Chuki zinazoweza kuwa zilichochewa na ubaguzi kwa Misingi ya Ukabila ,Udini ,Ukanda au jinsia yake Rais wetu. Sasa kitendo cha kuona RAIS wetu akiongoza Nchi vizuri kwa amani na utulivu huku kukiwa kumetamalaki umoja na mshikamano hapa Nchini bila shaka lilikuwa ni pigo baya kwa watu hao wenye chuki binafsi.

Kitendo pia cha CCM kupitia Mkutano Mkuu wake kuamua kumpitisha Mapema kabisa Rais Samia kuwa Mgombea wake katika uchaguzi Mkuu ujao nalo linaweza kuwa ilikuwa ni msumari wa moto katika kidonda kibichi . Hivyo basi kuna uwezekano Askofu Gwajima akawa anatumika na kutumiwa kama kipaza Sauti kwa niaba ya kundi na watu hao kutaka na kujaribu kumchafua Rais Samia katika wakati huu wakuelekea uchaguzi Mkuu.

Hii ni katika kusukuma kete taratibu ili kumdhoofisha ,kumvuruga ,kumpanikisha,kumhamisha kiajenda Rais wetu na kumfanya akose amani na utulivu wa kuongoza Nchi yetu na hivyo kutimiza azima na malengo yao ya tangia 2021 ya kutotaka Rais Samia awe Rais wetu kwa sasa za kijinga na zilizojaa ubaguzi na chuki binafsi tu zenye kuchochea na uchu na uroho wa madaraka.

Kwa hiyo Askofu GWAJIMA ni anaweza kuwa kama mtu aliyetagulizwa mbele tu na kupewa jukumu la kumchafua kwa nguvu zote Rais Samia na uongozi wake. Hasa baada ya kutambua ya kuwa RAIS Samia anapendwa kukubalika ,kuaminika na kuungwa mkono na watanzania wote. Ndio maana unaona Askofu Gwajima alijielekeza katika kumshambulia na kuelekeza mashabulizi kwa taasisi ya Rais na Urais ,kwa sababu ndio lengo kuu la ajenda zilizo nyuma ya pazia kutaka kummaliza Kisiasa Rais wetu.

Hata hivyo Askofu Gwajima hataweza kufanikisha ajenda zake za kumchafua Rais wetu. Hataweza kumdhoofisha Mama yetu,hataweza kumshusha Jemedari wetu,hataweza kwa namna yoyote ile na kwa mbinu ya aina yoyote ile kuchafua taswira nzuri ya Rais wetu mbele ya watanzania. Najua atafanya kila mbinu na kuzungumza kila uzushi na uongo kwa lengo la kutaka kinachoanganisha Rais Samia na wananchi ili achukiwe yeye binafsi na uongozi wake lakini kamwe na katu hataweza kufanikiwa. Rais Samia ataendelea kuongoza Taifa letu mpaka 2030 Panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu kwa Uweza na msaada wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe aliye mtoa njia na maarifa.

Rais Samia aliinuliwa kwa mkono wa Mungu na hawezi kamwe kushushwa kwa Mkono wa Mwanadamu mwenye chuki zake Binafsi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kilichokukwaza kwenye maneno ya Gwajima ni kipi? Ameuliza swali Rais atajisikiaje mwanawe Abdul atekwe halafu akutwe hana macho, Na hakuishia hapo kajitolea mfano hata yeye mwenyewe vipi ikitokea mtoto wake Jordan atekwe kesho aokotwe hana macho.
Hivi familia ya Mzee Kibao ilijisikiaje kwa kitendo alichofanyiwa Mzee wao!!
Nini kimefanyika kukomesha hali hiyo!!
Kama unamsikia mbunge anaropoka eti Martha Karua asingeachwa hivi hivi,wangemtesa ili akome kuja Tanzania, hii kauli ya kishenzi unaona Ni Sawa,maana mnakiri mna kipindi cha kigaidi kinachofadhiliwa na Ccm!!
Hivi angekuwa ni raia wa Marekani mngejaribu hata kumgusa!!
Brother CCM imepoteza dira imebakiza tu bungeni. Hoja ya Gwajima haina uhusiano Na kuingilia/kutweza Madaraka ya Rais.
Mmeshupaza shingo zenu na hoja za kijinga mmeacha kujadili ufisadi mkubwa unaendelea.
Ripoti ya Cag kama vile hamuioni.
 
Back
Top Bottom