PreGE2025 Kuna uwezekano Askofu Gwajima anamchafua Rais Samia kuelekea Uchaguzi na akitumika na wale watu waliotaka asiwe Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
acha zako bhana sisi sio ndugu zako tungekuwa ndugu zenu mungekuwa na uchungu na tunayopitia,kuteka mteke,muue na kulawiti ninyi afu mdai c ndugu zenu kivipi?
Watanzania wote sisi ni ndugu labda wewe ni mhamiaji haramu
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ningependa Kuwaambieni na kuwakumbusheni Ya Kuwa Pamoja na Katiba yetu kuwa wazi na kunyooka kabisa juu ya nini kinapaswa kufanyika pale Rais aliyepo madarakani anapofariki Dunia, Yaani Makamu wa Rais Kuapishwa na kuchukua Madaraka ya Urais kuongoza Nchi.

Lakini ni Lazima Mfahamu ya Kuwa kuna Mambo makubwa ,Mazito ya kuogofya ,Ya Siri yalifanywa au kudhamiliwa kufanywa au kukusudiwa kufanywa na baadhi ya watu kutaka Kupindua Matakwa ya Katiba yetu ili Mama yetu aliyekuwa Ni Makamu wa Rais Asiweze Kuapishwa na kuchukua Madaraka ya Urais Baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli kama inavyoeleza Katiba yetu.

Hapa mnaweza kurejea kauli ,maneno na Mazungumzo ya Jenerali Venance Mabeyo Ambaye alikuwa ni Mkuu wa Majeshi wakati huo. Ambapo Alisema kuwa Kuna watu walisahau matakwa ya katiba na katiba inasema nini baada ya kifo cha Rais aliyepo madarakani. Ambapo anasema na alisema ya kuwa yeye ndiye alifanya kazi ya kuwakumbusha hao watu matakwa ya Katiba.

Kitu nachopenda kuwaambieni ni kuwa hii ni kauli nzito sana kutoka kwa mtu na kiongozi mzito sana ambayo aliitamka kiuongozi. Hapa kwa lugha nyingine waweza kusema kuwa kuna watu au kikundi cha watu kwa sababu zao na maslahi yao walitaka kupindua matakwa ya katiba ili waweke au kusimika mtu wao katika kiti cha Urais baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli kinyume kabisa na matakwa ya katiba yetu.

Kwa hiyo siyo kwamba walikuwa wamejisahau au walikuwa ni wajinga wa sheria na katiba au kwamba walikuwa hawajui katiba inataka nini kifanyike. Walikuwa wanajua kila kitu ila kwa uroho na uchu wa madaraka walitaka wafanye kitendo hicho cha hatari ambacho pengine kingeweza kuhatarisha usalama wa Taifa letu kwa kusababisha machafuko na mgawanyiko ndani ya Taifa letu.

Kwa sababu ni lazima kungezaliwa kambi na mgawanyiko mkubwa sana kuanzia Majeshini ,uongozini hadi uraiani ambapo wengi wangekuwa upande wa katiba yetu kutaka katiba iheshimiwe na kufuatwa kwa Mama Samia kuapishwa kuwa Rais wa NCHI yetu. Hivyo tuna kila sababu ya kumpongeza General Mabeyo kwa Ujasiri na uzalendo wake uliotukuka kabisa wa kusimama imara kulinda katiba yetu kama kiapo chake kinavyo Muelekeza.

Hivyo basi kushindwa kwa jaribio hilo la watu hao la kutaka Kupindua matakwa ya katiba yetu. Bila shaka liliwaumiza,kuwakwaza ,kuwasononesha ,kuwachukiza na kuwaacha na hasira kubwa sana vifuani pao watu au kikundi hicho kilichotaka kufanya jambo hilo la hatari kwa usalama wetu wa Taifa. Hali ambayo bila shaka iliwaacha na kitu kimoja pekee mikononi na vifuani pao. Ambalo ni Dua na Maombi mabaya kwa utawala wa Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Bila shaka waliendelea kuomba Rais wetu ashindwe kuongoza Nchi ,utawala wake uwe wa misukosuko,majanga majanga ,kuchukiwa na wananchi ,vurugu na maandamano ya hapa na pale na mambo mengine mbalimbali mabaya mabaya. Lakini kwa sababu uongozi unatoka kwa Mungu,na kwa kuwa Mungu ndiye hutoa kibali cha uongozi kwa mtu ikawa tofauti sana na matarajio ya hawa watu na hicho kikundi Chenye chuki binafsi kwa Rais wetu.

Chuki zinazoweza kuwa zilichochewa na ubaguzi kwa Misingi ya Ukabila ,Udini ,Ukanda au jinsia yake Rais wetu. Sasa kitendo cha kuona Rais wetu akiongoza Nchi vizuri kwa amani na utulivu huku kukiwa kumetamalaki umoja na mshikamano hapa Nchini bila shaka lilikuwa ni pigo baya kwa watu hao wenye chuki binafsi.

Kitendo pia cha CCM kupitia Mkutano Mkuu wake kuamua kumpitisha Mapema kabisa Rais Samia kuwa Mgombea wake katika uchaguzi Mkuu ujao nalo linaweza kuwa ilikuwa ni msumari wa moto katika kidonda kibichi . Hivyo basi kuna uwezekano Askofu Gwajima akawa anatumika na kutumiwa kama kipaza Sauti kwa niaba ya kundi na watu hao kutaka na kujaribu kumchafua Rais Samia katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi Mkuu.

Hii ni katika kusukuma kete taratibu ili kumdhoofisha ,kumvuruga ,kumpanikisha,kumhamisha kiajenda Rais wetu na kumfanya akose amani na utulivu wa kuongoza Nchi yetu, na hivyo kutimiza azima na malengo yao ya tangia 2021 ya kutotaka Rais Samia awe Rais wetu kwa sababu za kijinga na zilizojaa ubaguzi na chuki binafsi tu zenye kuchochewa na uchu na uroho wa madaraka.

Kwa hiyo Askofu GWAJIMA ni anaweza kuwa kama mtu aliyetangulizwa mbele tu na kupewa jukumu la kumchafua kwa nguvu zote Rais Samia na uongozi wake. Hasa baada ya kutambua ya kuwa RAIS Samia anapendwa, kukubalika ,kuaminika na kuungwa mkono na watanzania wote. Ndio maana unaona Askofu Gwajima alijielekeza katika kumshambulia na kuelekeza mashabulizi kwa taasisi ya Rais na Urais ,kwa sababu ndio lengo kuu la ajenda zilizo nyuma ya pazia kutaka kummaliza Kisiasa Rais wetu.

Hata hivyo Askofu Gwajima hataweza kufanikisha ajenda zake za kumchafua Rais wetu. Hataweza kumdhoofisha Mama yetu,hataweza kumshusha Jemedari wetu,hataweza kwa namna yoyote ile na kwa mbinu ya aina yoyote ile kuchafua taswira nzuri ya Rais wetu mbele ya watanzania. Najua atafanya kila mbinu na kuzungumza kila uzushi na uongo kwa lengo la kutaka kumchonganisha Rais Samia na wananchi ili achukiwe yeye binafsi na uongozi wake lakini kamwe na katu hataweza kufanikiwa. Rais Samia ataendelea kuongoza Taifa letu mpaka 2030 Panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu kwa Uweza na msaada wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe aliye mtoa njia na maarifa.

Rais Samia aliinuliwa kwa mkono wa Mungu na hawezi kamwe kushushwa kwa Mkono wa Mwanadamu mwenye chuki zake Binafsi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

Kumchfua ameongea nini ambacho sio cha kweli?
 
Gwajima amechaguliwa watu gani kumjibu? Je huko Ccm hakuna hata wenye akili timamu wakajibu hoja zake?
 
Uko sahihi wakati mwingine! Bahati nzuri ni baadhi ya Wanachama wa CCM chama chako ambao hawakutaka Taifa kuongozwa tena na Mwanamke!
 
CCM Kauli yetu ni Moja tu kuwa tunakwenda na Mama hadi 2030 . Ambaye anaona hajaridhishwa na maamuzi haya ya wengi ambayo ni kiu kubwa ya watanzania. Basi ajiondoe chamani na kuunda chama chake ili akagombee Urais aone namna tutakavyo mgaragaza kwenye sanduku la kura
 
Aje kiongozi au mtu mashuhuri/ mtaalam aitishe conference aongelee kuhusu Uchumi au mwenendo wa kibajeti,...
Hutaona mjadala waka uchambuzi wala support kwa nini ? Mfumo wetu wa ELIMU..Hauwajengi waTz kujadili ISSUES.....

njoo na issue kama hizi ndipo utagundua mental capacity za kizazi ...
Bunge hadi linaisha , vijana na watu wazima wangapi wanaibua mijadala....
Kuna kipindi mh Zitto Kabwe alikuwa anaitisha conference kujadili Madudu report ya CAG.....
Watu kimyaaaaa....si kwamba wanapenda ila waletee cheap AGENDA.....!!!

Mfumo wa elimu, mfumo wa elimu , mfumo wa elimu.....
 
1. Hii ni Awamu ya mpito ya marehemu, sawa kwa nini sasa hataki kuacha ili Agombee lakini yeye anataka kuunganisha?
2. Kwa uninja wake akabadiri awamu ya tano ya mpito kuwa awamu ya sita kama vile yeye ndiyo alichaguliwa
3. Hayo yote, lakini uliyoandika hayajibu lolote kuhusu tuhuma kutoka kwa Gwajima
Ulipompigia kura JPM ulimpigia kura Samia, wote wawili ni mtu na msaidizi wake kwenye utekelezaji wa kazi ya urais.

Ukimchagua Donald Trump umemchagua pia JD Vance, hiyo ndiyo siasa. Nyinyi ndio mlimchukia Samia kisa ameurithi urais kwa kuwa makamu wa JPM kuelekeza hasira zenu mkaanza kumshambulia Kikwete kama vile yeye ndiye aliyehusika na afya ya marehemu kubadilika ghafla kisha akaaga dunia.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ningependa Kuwaambieni na kuwakumbusheni Ya Kuwa Pamoja na Katiba yetu kuwa wazi na kunyooka kabisa juu ya nini kinapaswa kufanyika pale Rais aliyepo madarakani anapofariki Dunia, Yaani Makamu wa Rais Kuapishwa na kuchukua Madaraka ya Urais kuongoza Nchi.

Lakini ni Lazima Mfahamu ya Kuwa kuna Mambo makubwa ,Mazito ya kuogofya ,Ya Siri yalifanywa au kudhamiliwa kufanywa au kukusudiwa kufanywa na baadhi ya watu kutaka Kupindua Matakwa ya Katiba yetu ili Mama yetu aliyekuwa Ni Makamu wa Rais Asiweze Kuapishwa na kuchukua Madaraka ya Urais Baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli kama inavyoeleza Katiba yetu.

Hapa mnaweza kurejea kauli ,maneno na Mazungumzo ya Jenerali Venance Mabeyo Ambaye alikuwa ni Mkuu wa Majeshi wakati huo. Ambapo Alisema kuwa Kuna watu walisahau matakwa ya katiba na katiba inasema nini baada ya kifo cha Rais aliyepo madarakani. Ambapo anasema na alisema ya kuwa yeye ndiye alifanya kazi ya kuwakumbusha hao watu matakwa ya Katiba.

Kitu nachopenda kuwaambieni ni kuwa hii ni kauli nzito sana kutoka kwa mtu na kiongozi mzito sana ambayo aliitamka kiuongozi. Hapa kwa lugha nyingine waweza kusema kuwa kuna watu au kikundi cha watu kwa sababu zao na maslahi yao walitaka kupindua matakwa ya katiba ili waweke au kusimika mtu wao katika kiti cha Urais baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli kinyume kabisa na matakwa ya katiba yetu.

Kwa hiyo siyo kwamba walikuwa wamejisahau au walikuwa ni wajinga wa sheria na katiba au kwamba walikuwa hawajui katiba inataka nini kifanyike. Walikuwa wanajua kila kitu ila kwa uroho na uchu wa madaraka walitaka wafanye kitendo hicho cha hatari ambacho pengine kingeweza kuhatarisha usalama wa Taifa letu kwa kusababisha machafuko na mgawanyiko ndani ya Taifa letu.

Kwa sababu ni lazima kungezaliwa kambi na mgawanyiko mkubwa sana kuanzia Majeshini ,uongozini hadi uraiani ambapo wengi wangekuwa upande wa katiba yetu kutaka katiba iheshimiwe na kufuatwa kwa Mama Samia kuapishwa kuwa Rais wa NCHI yetu. Hivyo tuna kila sababu ya kumpongeza General Mabeyo kwa Ujasiri na uzalendo wake uliotukuka kabisa wa kusimama imara kulinda katiba yetu kama kiapo chake kinavyo Muelekeza.

Hivyo basi kushindwa kwa jaribio hilo la watu hao la kutaka Kupindua matakwa ya katiba yetu. Bila shaka liliwaumiza,kuwakwaza ,kuwasononesha ,kuwachukiza na kuwaacha na hasira kubwa sana vifuani pao watu au kikundi hicho kilichotaka kufanya jambo hilo la hatari kwa usalama wetu wa Taifa. Hali ambayo bila shaka iliwaacha na kitu kimoja pekee mikononi na vifuani pao. Ambalo ni Dua na Maombi mabaya kwa utawala wa Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Bila shaka waliendelea kuomba Rais wetu ashindwe kuongoza Nchi ,utawala wake uwe wa misukosuko,majanga majanga ,kuchukiwa na wananchi ,vurugu na maandamano ya hapa na pale na mambo mengine mbalimbali mabaya mabaya. Lakini kwa sababu uongozi unatoka kwa Mungu,na kwa kuwa Mungu ndiye hutoa kibali cha uongozi kwa mtu ikawa tofauti sana na matarajio ya hawa watu na hicho kikundi Chenye chuki binafsi kwa Rais wetu.

Chuki zinazoweza kuwa zilichochewa na ubaguzi kwa Misingi ya Ukabila ,Udini ,Ukanda au jinsia yake Rais wetu. Sasa kitendo cha kuona Rais wetu akiongoza Nchi vizuri kwa amani na utulivu huku kukiwa kumetamalaki umoja na mshikamano hapa Nchini bila shaka lilikuwa ni pigo baya kwa watu hao wenye chuki binafsi.

Kitendo pia cha CCM kupitia Mkutano Mkuu wake kuamua kumpitisha Mapema kabisa Rais Samia kuwa Mgombea wake katika uchaguzi Mkuu ujao nalo linaweza kuwa ilikuwa ni msumari wa moto katika kidonda kibichi . Hivyo basi kuna uwezekano Askofu Gwajima akawa anatumika na kutumiwa kama kipaza Sauti kwa niaba ya kundi na watu hao kutaka na kujaribu kumchafua Rais Samia katika wakati huu wa kuelekea uchaguzi Mkuu.

Hii ni katika kusukuma kete taratibu ili kumdhoofisha ,kumvuruga ,kumpanikisha,kumhamisha kiajenda Rais wetu na kumfanya akose amani na utulivu wa kuongoza Nchi yetu, na hivyo kutimiza azima na malengo yao ya tangia 2021 ya kutotaka Rais Samia awe Rais wetu kwa sababu za kijinga na zilizojaa ubaguzi na chuki binafsi tu zenye kuchochewa na uchu na uroho wa madaraka.

Kwa hiyo Askofu GWAJIMA ni anaweza kuwa kama mtu aliyetangulizwa mbele tu na kupewa jukumu la kumchafua kwa nguvu zote Rais Samia na uongozi wake. Hasa baada ya kutambua ya kuwa RAIS Samia anapendwa, kukubalika ,kuaminika na kuungwa mkono na watanzania wote. Ndio maana unaona Askofu Gwajima alijielekeza katika kumshambulia na kuelekeza mashabulizi kwa taasisi ya Rais na Urais ,kwa sababu ndio lengo kuu la ajenda zilizo nyuma ya pazia kutaka kummaliza Kisiasa Rais wetu.

Hata hivyo Askofu Gwajima hataweza kufanikisha ajenda zake za kumchafua Rais wetu. Hataweza kumdhoofisha Mama yetu,hataweza kumshusha Jemedari wetu,hataweza kwa namna yoyote ile na kwa mbinu ya aina yoyote ile kuchafua taswira nzuri ya Rais wetu mbele ya watanzania. Najua atafanya kila mbinu na kuzungumza kila uzushi na uongo kwa lengo la kutaka kumchonganisha Rais Samia na wananchi ili achukiwe yeye binafsi na uongozi wake lakini kamwe na katu hataweza kufanikiwa. Rais Samia ataendelea kuongoza Taifa letu mpaka 2030 Panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu kwa Uweza na msaada wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe aliye mtoa njia na maarifa.

Rais Samia aliinuliwa kwa mkono wa Mungu na hawezi kamwe kushushwa kwa Mkono wa Mwanadamu mwenye chuki zake Binafsi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wamdhibiti mapema.
 
Lucas umechanganyikiwa? Unatoa majibu mara mbilimbili au umesahau Jana umeitoa andiko lako kuchambua press ya gwajima?
 
Back
Top Bottom