Kuna uwezekano mkubwa Rais Samia akapita bila kupingwa uchaguzi wa mwakani

Ndugu zangu Watanzania,

Dalili zote zinaonyesha wazi kabisa Kuwa Mama yetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan atapita bila kupingwa uchaguzi wa Hapo Mwakani.

Hii ni kwa kuwa inaonyesha vyama vya Upinzani hususani CHADEMA kukosa mgombea Urais hapo Mwakani.Kwa sababu Lissu ambaye alikuwa anatazamiwa kugombea hapo Mwakani. Tayari viongozi mbalimbali wa CHADEMA wametamka wazi hadharani kuwa Lissu hana uwezo na hakuwa na sifa za kuwa RAIS Wa Nchi hii na kwamba walimpa nafasi Ya kugombea Urais kwa sababu tu ya Uropokaji wake kwa Magufuli.lakini ukweli ni kwamba Lissu hana uwezo wa kupanga hata mipango ya mtaa.

Na kwamba hata kama ingetokea amepita kwa bahati mbaya basi mipango yote ingesimamiwa na chama na yeye kuwa kama pambo au picha tu au RAIS kimvuli tu au Sanamu au kinyago cha kuchongwa.

Hivyo basi kwa kauli hizi zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA imepelekea wananchi mbalimbali mitaani kujuta sana na kukatishwa sana tamaa na CHADEMA kwa kuiunga mkono siku za nyuma.wengi mitaani wanasema ya kuwa wanajuta na kujutia kupoteza muda wao kupanga foleni kumpigia lissu kura na CHADEMA yake ilihali kumbe hata chama kinafahamu ya kuwa alikuwa hana uwezo wa kuongoza. bali aliteuliwa kwa Uropokaji wake kwa Magufuli uliotokana na chuki binafsi.

Wananchi wanasema kwa sasa hawawezi kamwe kuiamini tena CHADEMA na kumpigia kura mgombea Urais wake kwa sababu chama kimeonyesha ulaghai na utapeli mkubwa sana wa kisiasa kwa kuwarubuni.wanasema pengine ndio maana Mbowe hakujihangaisha kumnadi lissu kwa sababu alikuwa anajua hana uwezo wa kuwa RAIS zaidi ya Uropokaji tu na mihemuko..

Wakarejea pia kilichotokea 2015 na kufikia hitimisho kuwa CHADEMA haijawahi kuwa na mipango wala mikakati ya kuandaa mgombea Urais wake.Ndio maana huwa wanafanya kuvizia wagombea kutoka CCM na kuwapa nafasi ya kugombea nafasi nyeti na za juu. Hapa mnaweza kukumbuka namna hayati Lowassa alivyopewa hadi ujumbe wa kamati kuu.hapo bado sijazungumzia upande wa Nyarandu na Mheshimiwa Frederick Sumaye ambao nao walipewa nafasi ndani ya CHADEMA.hii ni kwa kuwa chama kina ombwe kubwa sana la uongozi na uhaba wa watu wenye uwezo wa kuongoza.

Ndio Maana nasema ya kuwa RAIS Wetu kipenzi Daktari Mama Samia ana uwezekano mkubwa sana wakupita bila kupingwa hapo Mwakani.Sasa embu niambie wana jukwaa ni nani ndani ya CHADEMA mwenye uwezo wa kugombea Urais na mwenye uwezo wa kushindana na Rais Samia katika sanduku la kura?

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Tunachotaka pesa iwepo mtaani,bajeti iwe real isiwe ya muse,na tunachotaka ni biashara ziwe imara,bei za mazao ziwe rafiki,na tunachotaka ni household income level iimarike na tunachotaka ni tukitaka kupanda ndege tusijiulize tunapata wapi pesa,na hoteli ziuze biashara na mazao yawe na bei imara,Mamishahara yapae juu na sio ulingo uwe wa maroli pekee pesa haba tafadhali poti hili lizangatiwe.Rais hata ukiwa wewe hapo as long watu wako happy not bad benga,ila kama wanafurahi wa Kizmkazi basi tutampigia magoti Allah utuwekee wepesi sababu hatujakosea hapa Tanzania ni sehemu tumezaliwa na hatuwezi kuhamia nchi za watu.
 
Rais Samia atapita na kushinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima.atazoa kura zote za ndio.
Madeni ya hovyo hatutaki na uwekezaji kama ule wa DP World ya akina Roy McLoy hatutaki na kuuza vitaru Ngorongoro hatutaki,na asilimia ya mgao wa Zanzibar ujadiliwe bungeni na upigiwe kura na hata hili la bajeti inapita halafu haitekelezwi inahama miaka na Miaka nalo sio credit,swala la kuleta wezi kuja kuiba pesa kupitia mikopo ya Benki nayo ni tatizo,We brother unajisikiaje unapoona parachichi zinauzwa kilogram 1 kwa kiasi cha Tsh 500, na korosho kuuzwa kwa bei ya Tsh 1000, na pia mafao ya wastaafu yanapo kuwa na vitu vya ajabu kama kitu ya uchawi inaitwa kikotoo,inakuwaje watu walete hii kitu kama kweli Kuna utawaka Bora,hata ILO Haina ujinga huu.
Brother urais hata wewe kuwa tuu lakini haya mambo ya kuwa Rais wakusifiwa kwa Miradi ya kujenga school ni maji ya kunywa hiyo ni kupigiana kelele,Maji na Barabara jukumi la serikali,wacha watu wawe na furaha,hayo mengine ni mhemuko.
 
Sawa, japo unafanya propaganda za kisiasa, kwani hakuna vile vyama 14 vya magumashi vikasimamisha wagombea wa mchongo ili ionekane kashinda kwa kuwashinda hao wagombea feki?
 
Havina mgombea mwenye uwezo wa kushindana na RAIS Samia na wala haviwezi kuzunguka hata mkoa mmoja tu kufanya kampeni.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Dalili zote zinaonyesha wazi kabisa Kuwa Mama yetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan atapita bila kupingwa uchaguzi wa Hapo Mwakani.

Hii ni kwa kuwa inaonyesha vyama vya Upinzani hususani CHADEMA kukosa mgombea Urais hapo Mwakani.Kwa sababu Lissu ambaye alikuwa anatazamiwa kugombea hapo Mwakani. Tayari viongozi mbalimbali wa CHADEMA wametamka wazi hadharani kuwa Lissu hana uwezo na hakuwa na sifa za kuwa RAIS Wa Nchi hii na kwamba walimpa nafasi Ya kugombea Urais kwa sababu tu ya Uropokaji wake kwa Magufuli.lakini ukweli ni kwamba Lissu hana uwezo wa kupanga hata mipango ya mtaa.

Na kwamba hata kama ingetokea amepita kwa bahati mbaya basi mipango yote ingesimamiwa na chama na yeye kuwa kama pambo au picha tu au RAIS kimvuli tu au Sanamu au kinyago cha kuchongwa.

Hivyo basi kwa kauli hizi zilizotolewa na viongozi wa CHADEMA imepelekea wananchi mbalimbali mitaani kujuta sana na kukatishwa sana tamaa na CHADEMA kwa kuiunga mkono siku za nyuma.wengi mitaani wanasema ya kuwa wanajuta na kujutia kupoteza muda wao kupanga foleni kumpigia lissu kura na CHADEMA yake ilihali kumbe hata chama kinafahamu ya kuwa alikuwa hana uwezo wa kuongoza. bali aliteuliwa kwa Uropokaji wake kwa Magufuli uliotokana na chuki binafsi.

Wananchi wanasema kwa sasa hawawezi kamwe kuiamini tena CHADEMA na kumpigia kura mgombea Urais wake kwa sababu chama kimeonyesha ulaghai na utapeli mkubwa sana wa kisiasa kwa kuwarubuni.wanasema pengine ndio maana Mbowe hakujihangaisha kumnadi lissu kwa sababu alikuwa anajua hana uwezo wa kuwa RAIS zaidi ya Uropokaji tu na mihemuko..

Wakarejea pia kilichotokea 2015 na kufikia hitimisho kuwa CHADEMA haijawahi kuwa na mipango wala mikakati ya kuandaa mgombea Urais wake.Ndio maana huwa wanafanya kuvizia wagombea kutoka CCM na kuwapa nafasi ya kugombea nafasi nyeti na za juu. Hapa mnaweza kukumbuka namna hayati Lowassa alivyopewa hadi ujumbe wa kamati kuu.hapo bado sijazungumzia upande wa Nyarandu na Mheshimiwa Frederick Sumaye ambao nao walipewa nafasi ndani ya CHADEMA.hii ni kwa kuwa chama kina ombwe kubwa sana la uongozi na uhaba wa watu wenye uwezo wa kuongoza.

Ndio Maana nasema ya kuwa RAIS Wetu kipenzi Daktari Mama Samia ana uwezekano mkubwa sana wakupita bila kupingwa hapo Mwakani.Sasa embu niambie wana jukwaa ni nani ndani ya CHADEMA mwenye uwezo wa kugombea Urais na mwenye uwezo wa kushindana na Rais Samia katika sanduku la kura?

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Samia mitano tena CCM DAIMA hii imeenda
 
Back
Top Bottom