Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
Sote tunafahamu kwamba,
michuano ya kombe la dunia imepangwa kufanyika kuanzia mapema mwezi June 2026. Lakini kutokana na hali ya kiusalama kudorora duniani, hasa ndani ya miongoni mwa nchi waandaaji na washiriki wa michuano hiyo, upo uwezekano mkubwa sana wa kuahirishwa kwa michuano hiyo, na kupangwa kufanyika wakati mwingine mahali pengine salama.
Kwa mfano nchi mwenyeji kama vile Mexico, makundi ya kihalifu na magenge ya walanguzi na wauzaji wa mihadarati yanahatarisha usalama wa nchi hiyo na serikali yake na hivyo kuzua hofu kubwa dhidi ya usalama wa wana michezo na mashabiki wa nchi mbalimbali duniani wanaopanga kwenda kushuhudia mashindano hayo nchini humo, na hivyo hali hii inaweza kuchochea mataifa mengi kusita kuingia Mexico au kususia kabisa michuano hiyo kuhofia usalama na uhai wao dhidi ya magenge hayo hatari sana ya kihalifu.
Kwa nchi nyingine mwenyeji kama Marekani, licha ya kua na kiwango cha juu sana cha teknolojia katika usalama, lakini bado kuna hofu ya matukio ya kigaidi kutokea kwa wingi ndani au nje ya viwanja vitakavyotumika kwa michuano hiyo. Mbali na hilo, upo uwezekano mkubwa sana kwa nchi kama Iran kususia michuano hiyo, lakini pia upo uwezekano mkubwa sana kwamba Marekani inaweza kuwanyima timu ya Irani na mashabiki wa mataifa mengine vibali vya kuingia Marekani na hivyo kuvuruga ratiba ya FIFA na kupunguza mvuto wa michuano hiyo muhimu sana duniani.
Kama mshauri muhimu wa masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kitaifa na kimataifa,
Naishauri FIFA, endapo wataahirisha michuano hiyo mwaka huu kwa sababu hizo za wazi na za msingi kabisa, nadhani ni muhimu sana wailete michuano hiyo ichezwe katika ardhi ya Afrca Mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda 2028, baada ya AFCON.
una maoni gani ndugu mdau wa JF na mpenzi wa mpira wa miguu?
Mungu Ibariki Tanzania