Kuna uwezekano mkubwa Simba kuanzia hatua ya pili Champion League msimu ujao

Mtapenda

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2011
Posts
1,115
Reaction score
2,063
Sio Kama ambavyo Manara alivyo wadanganya wana yanga na waandishi wa habari wasiojua chochote na walio kosa udadisi..

IKO HIVI
-Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo. Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

-Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita. Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF.

-Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF [emoji122][emoji122][emoji122]! Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili.

-Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

-Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao.

-Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO

-Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu. Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama watafika nusu fainali wanaweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi.

-Na kama itakuwa hivyo, wanaweza kuingia 10 bora na kupata moja kwa moja haki ya kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Lakini kama watatolewa na Orlando Pirates, basi watabaki katika nafasi ya 12 na kuomba zali kama la msimu huu...yaani wa juu yake wasifuzu ligi ya Mabingwa.

-Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchi mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani. Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad.

-Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA![emoji35] Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF!

Anyway, Mwenyezi Mungu ni wa wote!

Na Zaka Zakazi Msemaji Wa Azam FC
 
Simba ina karbu 90%kuanzia hatua ya pil ,, kwa sababu wenye namba zao ambao uwakika kabisa ni berkane na pyramid ,, atika ligi yao ni ngum sana kufuzu ligi ya mabingwa ,mfano berkane yupo nafas ya nane ata kama atashinda vp ni ngum sana kumtoa wydad na raja,so vyovyote vile atashirik shirikisho, tukijaa kwa pyramid ni nafuu kwake maana hajapishana sana na zamalek japo ni ngum kwake kumtoa ukiangalia uwezekano wa hao wawil kushirik ligi ya mabingwa ni mdogo ,apo ndio unakuja urahisi kwa simba kunzia hatua ya pil
 
Jamaa na wewe ukikopi maoni ya watu acknowledge basi!!!
 
Mkuu some mpaka mwisho yaani mwisho kabisaaa halafu rudi kucomment
 
Sasa hapo umesahihisha nini au una mhaho
 
wewe utakuwa umedandia mada. soma vizuri halafu elewa maana ya "kuna uwezekano"
Yanga mnatupa taabu sana kuwaelewesha vitu kwa sababu mnakurupuka
 
kama simba akitolewa hatua hii ya robo na kuwa wa 12 basi ataanzia raundi ya pili kwakuwa moroco na misry wana timu tatu tatu zilizowepo juu ya simba. na ligi ya mabingwa zitaenda mbili mbili. sasa hapo simba atakuwa wa kumi miongoni mwa wale waliofuzu cafcc.
 
... Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; ...
Kwa kuongezea, ni kwamba hapo ttunahesabu RS Berkane tu, maana hata Pyramids akichukua nafasi mbili za juu, maana yake atamshusha Zamalek au Al Ahly kucheza Shirikisho, ambao hao wote wapo juu yetu 😁
 
Kwa kuongezea, ni kwamba hapo ttunahesabu RS Berkane tu, maana hata Pyramids akichukua nafasi mbili za juu, maana yake atamshusha Zamalek au Al Ahly kucheza Shirikisho, ambao hao wote wapo juu yetu [emoji16]
Mkuu. Legeza kichwa

Hapo Misri champions league zinaenda timu Mbili tu , so timu ya tatu iliyo ndan ya top 10 ambayo itaenda shirikisho hiyo nafasi itachukuliwa na Simba , timu yeyote ile itakayoshindwa fuzu champions league , iwe al ahly iwe zemalek iwe pyramid , nafasi yake itakuchukuliwa na walio nafasi ya 11, 12 .. sio lazima awe pyramid , au sio lazima awe Berkane, yeyote yule tu pale Morocco,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…