Kuna uwezekano mkubwa Simba kuanzia hatua ya pili Champion League msimu ujao

Kuna uwezekano mkubwa Simba kuanzia hatua ya pili Champion League msimu ujao

Sio Kama ambavyo Manara alivyo wadanganya wana yanga na waandishi wa habari wasiojua chochote na walio kosa udadisi..

IKO HIVI
-Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo. Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

-Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita. Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF.

-Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF [emoji122][emoji122][emoji122]! Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili.

-Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

-Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao.

-Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO

-Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu. Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama watafika nusu fainali wanaweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi.

-Na kama itakuwa hivyo, wanaweza kuingia 10 bora na kupata moja kwa moja haki ya kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Lakini kama watatolewa na Orlando Pirates, basi watabaki katika nafasi ya 12 na kuomba zali kama la msimu huu...yaani wa juu yake wasifuzu ligi ya Mabingwa.

-Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchi mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani. Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad.

-Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA![emoji35] Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF!

Anyway, Mwenyezi Mungu ni wa wote!

Na Zaka Zakazi Msemaji Wa Azam FC
Kwani mwakani tunapeleka timu ngapi CAF?
 
H

Ii nikweli embu assume ni matokeo ya shule unapeleka report nyumbani umekuwa wa 12 sasa wewe utasema ni mwanafunzi bora kweli simba ya kawaida sana

Mbona umeishia wa kumi na mbili, hujasema idadi ya vilabu Afrika Ni ngapi. Simba Ni ya kumi na mbili Chini ya vilabu zaidi ya Mia mbili
 
Mpumbavu mama yako, alie lea toto jinga kama wewe unae amini team kufika robo finally ni kubwa hata pamba unayo cheza nayo ipo robo finally nayo ni kubwa?

Duh! Unalinganisha Azam confederation cup ya Tanzania pekee na CAF CUP la bara Zima Africa. Please tukubali ukweli Simba kajitahidi.
 
Duh! Unalinganisha Azam confederation cup ya Tanzania pekee na CAF CUP la bara Zima Africa. Please tukubali ukweli Simba kajitahidi.
Read between the lines unapo jiita mkubwa onyesha mafanikio sio unajiita mkubwa kisa upo quarter final mfano Benifica wamefika robo finally UEFA unaweza waita team kubwa au Spurs walifika final ya UEFA utawaweka kwenye team giant ulaya?
 
E
Mbona umeishia wa kumi na mbili, hujasema idadi ya vilabu Afrika Ni ngapi. Simba Ni ya kumi na mbili Chini ya vilabu zaidi ya Mia mbili
Even that nafasi ya 12 usiseme ww ni bora
 
Utopolo inawauma sana

Na mwakani kama kawaida mnatoka mapema tu kenge nyie
 
Mbona haueleweki
Nilichomaanisha ni kwamba Petro de Luanda na Setif ndio timu mbili pekee zilizochini ya Simba ambazo zimesalia kwenye michuano ya klabu bingwa.

Petro de Luanda wanashika nafasi ya 25 wakina na point 14.5 na Setif nao ni wa 27 ana point 13. Endapo Petro de Luanda akicheza fainali atajikisanyia point 25 hivyo itamfanya kufikisha jumla ya point 36. Na pia kwa nchini kwao ana uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao. Na endapo wakifuzu kucheza nusu fainali watakuwa wamejikusanyia point 20 hivyo watakuwa na jumla ya point 31

Setif hawa nao endapo wakicheza nusu fainali watakuwa na point 28 ambazo ni sawasawa na Simba endapo wakitolewa hatua hii. Setif wakifuzu kucheza fainali watakuwa na jumla ya point 33 japo hawa Setif kwenye ligi yao bado hajawa na uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao.

Hivyo ni lazima Simba iombe Petro de Luanda itolewe kesho ili Simba ndio ichukue advantage ya kutofuzu kwa Berkane. Kinyume na hapo itakuwa ni vigumu kuanzia raundi ya pili kwa Simba. Naruhusu kurekebishwa
 
Simba ina karbu 90%kuanzia hatua ya pil ,, kwa sababu wenye namba zao ambao uwakika kabisa ni berkane na pyramid ,, atika ligi yao ni ngum sana kufuzu ligi ya mabingwa ,mfano berkane yupo nafas ya nane ata kama atashinda vp ni ngum sana kumtoa wydad na raja,so vyovyote vile atashirik shirikisho, tukijaa kwa pyramid ni nafuu kwake maana hajapishana sana na zamalek japo ni ngum kwake kumtoa ukiangalia uwezekano wa hao wawil kushirik ligi ya mabingwa ni mdogo ,apo ndio unakuja urahisi kwa simba kunzia hatua ya pil
Msiwaze wa juu pekee fikiria na walio chini ya Simba(Petro de Luanda) akifuzu kucheza nusu fainali ni kwamba ile nafasi Berkane kutofuzu nchini kwao atakuwa ameibeba wao, na Simba itambidi aanze hatus ya awali
 
Kuna asilimia zaidi ya 85 Simba kuanzia raundi ya pili. Mara paap fainali ya klabu bingwa inachezwa kati ya Petro de Luanda vs Setif
Mara paap....Simba anachukua kombe la shirikisho.
 
Mara paap....Simba anachukua kombe la shirikisho.
Itakuwa ni hatua kubwa sana kwa Tanzania, na tutamfuata Mwinyi akatengue rasmi kauli yake. Simba kuchukua kombe linawezekana hilo kwasababu hakuna timu inayoingiza wachezaji zaidi ya 11 uwanjani.
 
Itakuwa ni hatua kubwa sana kwa Tanzania, na tutamfuata Mwinyi akatengue rasmi kauli yake. Simba kuchukua kombe linawezekana hilo kwasababu hakuna timu inayoingiza wachezaji zaidi ya 11 uwanjani.
Tutazunguka na kombe nchi nzima
 
Back
Top Bottom