Kuna uwezekano mkubwa Simba kuanzia hatua ya pili Champion League msimu ujao

Kuna uwezekano mkubwa Simba kuanzia hatua ya pili Champion League msimu ujao

Nilichokisema kimetimia ni rasmi Petro De Luanda wanafikisha alama 31 hivyo inachukua rasmi nafasi ya Berkane kutofuzu. Hivyo ili Simba ianzei raundi ya pili kwenye klabu bingwa msimu ujao ni lazima ajiongezee point ili ampite Petro De Luanda. Hivyo anapaswa kesho afuzu
 
Inaonekana mashabiki wa Uto mna makaptura kabisa matako hayakaliki, maana hata sehemu ambayo Simba Sc haijatajwa ni lazima muitaje?

Sasa kwenye hiyo comment uliyo-quote, Simba Sc inahusikaje?

Yanga inacheza leo ila hamna furaha kabisa mioyoni mwenu, kwasababu ni mashindano ya mbuzi.
Matusi tena?! kisa mpira
 
Kwani coefficient ni mali ya club au shirikisho zinapo toka team?
Kuna mambo mawili mnachanganya. Kuna kitu kinaitwa association ranking halafu kuna club ranking. Kwenye association ranking hapo ndipo inachukuliwa point zote zilizokusanya na klabu zake hiyo association husika na kisha inafanya ranking ili kuweza kupata association 12 ambazo zitakuwa zinaingiza tumu mbili kwenye michuano ya kimataifa. Kisha kuna club ranking ambapo inachukuliwa timu 10 ambazo hizo hazitoanzia kwenye preliminary roundi

Nakupa mfano katika association ranking ya msimu wa 2021 Algeria inashika nafasi ya 4 bingwa wa Algeria mwaka 2021 alikuwa ni Belouizdad. Lakini angalia Belouizdad pamoja na kuwa bingwa nchini kwao lakini kaanzia preliminary round msimu huu kwasababu hakuwa kwenye top ten ya CAF
 
Nilichomaanisha ni kwamba Petro de Luanda na Setif ndio timu mbili pekee zilizochini ya Simba ambazo zimesalia kwenye michuano ya klabu bingwa.

Petro de Luanda wanashika nafasi ya 25 wakina na point 14.5 na Setif nao ni wa 27 ana point 13. Endapo Petro de Luanda akicheza fainali atajikisanyia point 25 hivyo itamfanya kufikisha jumla ya point 36. Na pia kwa nchini kwao ana uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao. Na endapo wakifuzu kucheza nusu fainali watakuwa wamejikusanyia point 20 hivyo watakuwa na jumla ya point 31

Setif hawa nao endapo wakicheza nusu fainali watakuwa na point 28 ambazo ni sawasawa na Simba endapo wakitolewa hatua hii. Setif wakifuzu kucheza fainali watakuwa na jumla ya point 33 japo hawa Setif kwenye ligi yao bado hajawa na uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao.

Hivyo ni lazima Simba iombe Petro de Luanda itolewe kesho ili Simba ndio ichukue advantage ya kutofuzu kwa Berkane. Kinyume na hapo itakuwa ni vigumu kuanzia raundi ya pili kwa Simba. Naruhusu kurekebishwa
Aisee
Luanda✅
Setif ✅
 
Coefficient ya ubora wa ligi ndo unaamua timu zipi zianzie round ya ngapi? Na ligi hiyo iingize timu ngapi katika mashindano ya CAF.

Pamoja na unazi wangu wa Yanga, Simba imechangia Sana kukuza ubora wa ligi(coefficient ya ligi ya Tanzania katika list ya CAF. Na ilitokea kweli ikafikia hatua ya ligi yetu kutoa timu ya kuanzia round ya 2 badala ya kwanza basi tambua timu itakayokuwa ya 1 kwa ligi(bingwa) ndo atafaidika. So hata kama Simba wamiiwezesha ligi yetu kufikia ubora huo na Yanga akatwaa ubingwa then Yanga ataanzia round ya pili na atakayekuwa wapili likely Simba ataanza round ya kwanza ya playoffs
Hujui chochote kuhusu soka la afrika na kanuni zake jipe muda kwanza kujifunza then uje uchangie ukiwa unajua unacho changia
 
Nilichokisema kimetimia ni rasmi Petro De Luanda wanafikisha alama 31 hivyo inachukua rasmi nafasi ya Berkane kutofuzu. Hivyo ili Simba ianzei raundi ya pili kwenye klabu bingwa msimu ujao ni lazima ajiongezee point ili ampite Petro De Luanda. Hivyo anapaswa kesho afuzu
Nafasi ya pyramids anaichukua nani?
 
Sio Kama ambavyo Manara alivyo wadanganya wana yanga na waandishi wa habari wasiojua chochote na walio kosa udadisi..

IKO HIVI
-Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo. Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

-Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita. Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF.

-Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF [emoji122][emoji122][emoji122]! Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili.

-Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

-Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao.

-Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO

-Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu. Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama watafika nusu fainali wanaweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi.

-Na kama itakuwa hivyo, wanaweza kuingia 10 bora na kupata moja kwa moja haki ya kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Lakini kama watatolewa na Orlando Pirates, basi watabaki katika nafasi ya 12 na kuomba zali kama la msimu huu...yaani wa juu yake wasifuzu ligi ya Mabingwa.

-Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchi mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani. Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad.

-Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA![emoji35] Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF!

Anyway, Mwenyezi Mungu ni wa wote!

Na Zaka Zakazi Msemaji Wa Azam FC
Ikatokea Ligi ya NBC simba akawa nafasi ya 5 msimu ujao atashiriki kombe lipi?
 
Back
Top Bottom