Kuna uwezekano mkubwa Simba kuanzia hatua ya pili Champion League msimu ujao

Mm nadhani hamkumwelewa manara. Ni hivi akili yake ipo yanga tatizo mawazo yake yapo Simba, Sasa kinacho vuruga anashindwa kuwa eneo moja kwa wakati sahihi. Simba v/s yanga.
 
Sio Kama ambavyo Manara alivyo wadanganya wana yanga na waandishi wa habari wasiojua chochote na walio kosa udadisi..

IKO HIVI
-Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo. Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

-Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita. Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF.

-Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF [emoji122][emoji122][emoji122]! Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili.

-Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

-Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao.

-Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO

-Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu. Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama watafika nusu fainali wanaweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi.

-Na kama itakuwa hivyo, wanaweza kuingia 10 bora na kupata moja kwa moja haki ya kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Lakini kama watatolewa na Orlando Pirates, basi watabaki katika nafasi ya 12 na kuomba zali kama la msimu huu...yaani wa juu yake wasifuzu ligi ya Mabingwa.

-Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchi mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani. Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad.

-Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA![emoji35] Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF!

Anyway, Mwenyezi Mungu ni wa wote!

Na Zaka Zakazi Msemaji Wa Azam FC
Tulichokuwa na uhakika ni Simba sio bingwa wa ligi kuu, hayo mengine ni kama kubeti....
Usiumize kichwa Time Will tell.
 
Nilichomaanisha ni kwamba Petro de Luanda na Setif ndio timu mbili pekee zilizochini ya Simba ambazo zimesalia kwenye michuano ya klabu bingwa.

Petro de Luanda wanashika nafasi ya 25 wakina na point 14.5 na Setif nao ni wa 27 ana point 13. Endapo Petro de Luanda akicheza fainali atajikisanyia point 25 hivyo itamfanya kufikisha jumla ya point 36. Na pia kwa nchini kwao ana uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao. Na endapo wakifuzu kucheza nusu fainali watakuwa wamejikusanyia point 20 hivyo watakuwa na jumla ya point 31

Setif hawa nao endapo wakicheza nusu fainali watakuwa na point 28 ambazo ni sawasawa na Simba endapo wakitolewa hatua hii. Setif wakifuzu kucheza fainali watakuwa na jumla ya point 33 japo hawa Setif kwenye ligi yao bado hajawa na uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao.

Hivyo ni lazima Simba iombe Petro de Luanda itolewe kesho ili Simba ndio ichukue advantage ya kutofuzu kwa Berkane. Kinyume na hapo itakuwa ni vigumu kuanzia raundi ya pili kwa Simba. Naruhusu kurekebishwa
Setif wamefuzu nusu faina kwaiyo wamefikisha pwenti ngapi
 
Mpaka sasa wana point 28 ambazo ni sawa sawa na alizonazo Simba kwasasa. Sema hawa Setif kwenye ligi ya kwao anakazi ya kufanya ili aweze kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao. Wana point 37 huku wakiwa na vipolo mechi mbili. Anayeshika nafasi ya pili kwenye msimamo wao anapoint 46. Petro de Luanda ndio timu yenye athari ya moja kwa moja kwa Simba endapo tu wakimtoa Mamelod leo.
 
Nilichomaanisha ni kwamba Petro de Luanda na Setif ndio timu mbili pekee zilizochini ya Simba ambazo zimesalia kwenye michuano ya klabu bingwa.

Petro de Luanda wanashika nafasi ya 25 wakina na point 14.5 na Setif nao ni wa 27 ana point 13. Endapo Petro de Luanda akicheza fainali atajikisanyia point 25 hivyo itamfanya kufikisha jumla ya point 36. Na pia kwa nchini kwao ana uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao. Na endapo wakifuzu kucheza nusu fainali watakuwa wamejikusanyia point 20 hivyo watakuwa na jumla ya point 31

Setif hawa nao endapo wakicheza nusu fainali watakuwa na point 28 ambazo ni sawasawa na Simba endapo wakitolewa hatua hii. Setif wakifuzu kucheza fainali watakuwa na jumla ya point 33 japo hawa Setif kwenye ligi yao bado hajawa na uhakika wa kufuzu kucheza klabu bingwa msimu ujao.

Hivyo ni lazima Simba iombe Petro de Luanda itolewe kesho ili Simba ndio ichukue advantage ya kutofuzu kwa Berkane. Kinyume na hapo itakuwa ni vigumu kuanzia raundi ya pili kwa Simba. Naruhusu kurekebishwa
Kumbe maombi ya wana Msimbazi yanabidi yaanze leo, kwa kuomba Petro de Luanda watolewe
 
Ila Simba atamtoa Pirates kwake si ndio?
Inaonekana mashabiki wa Uto mna makaptura kabisa matako hayakaliki, maana hata sehemu ambayo Simba Sc haijatajwa ni lazima muitaje?

Sasa kwenye hiyo comment uliyo-quote, Simba Sc inahusikaje?

Yanga inacheza leo ila hamna furaha kabisa mioyoni mwenu, kwasababu ni mashindano ya mbuzi.
 
Mkuu mpira huu unaweza shangaa ngoma ikaisha kwa sare
Mmh labda, lakini kwa jinsi matokeo yalivyo mwenye faida ni Mamelod (goli la ugenini).

Yeye hata akifunga moja tu bila kurusu goli, anakuwa amepita.
 
Mkuu kipindi cha kwanza kimeisha ngoma bado ni ngumu. Jamaa first half wamefanikiwa mpango wao wa kutofungwa. Ngoja tuone kipindi cha pili Mamelod watakujaje
 
Ni hatari mkuu, ila hawa Petro nimeangalia line up yao inaonekana wapo vizuri.

Kikosi chao kimajaa wabrazil na wareno, Mamelod akizubaa anatoka leo maana petro wataingia kipindi cha pili wakiwa na molari sana.

Mambo yakiwa hivi, naiona penalty wakipewa mamelod.
 
Coefficient ya ubora wa ligi ndo unaamua timu zipi zianzie round ya ngapi? Na ligi hiyo iingize timu ngapi katika mashindano ya CAF.

Pamoja na unazi wangu wa Yanga, Simba imechangia Sana kukuza ubora wa ligi(coefficient ya ligi ya Tanzania katika list ya CAF. Na ilitokea kweli ikafikia hatua ya ligi yetu kutoa timu ya kuanzia round ya 2 badala ya kwanza basi tambua timu itakayokuwa ya 1 kwa ligi(bingwa) ndo atafaidika. So hata kama Simba wamiiwezesha ligi yetu kufikia ubora huo na Yanga akatwaa ubingwa then Yanga ataanzia round ya pili na atakayekuwa wapili likely Simba ataanza round ya kwanza ya playoffs
 
Sio kweli mkuu anayeanzia raundi ya pili ni timu zilizo kwenye top ten kwenye rank za CAF
 
Coefficient ya ubora wa ligi ndo unaamua timu zipi zianzie round ya ngapi? Na ligi hiyo iingize timu ngapi katika mashindano ya CAF.

Pamoja na unazi wangu wa Yanga, Simba imechangia Sana kukuza ubora wa ligi(coefficient ya ligi ya Tanzania katika list ya CAF. Na ilitokea kweli ikafikia hatua ya ligi yetu kutoa timu ya kuanzia round ya 2 badala ya kwanza basi tambua timu itakayokuwa ya 1 kwa ligi(bingwa) ndo atafaidika. So hata kama Simba wamiiwezesha ligi yetu kufikia ubora huo na Yanga akatwaa ubingwa then Yanga ataanzia round ya pili na atakayekuwa wapili likely Simba ataanza round ya kwanza ya playoffs
Kwahiyo Manara alikuwa sawa?
 
Ni hatari mkuu, ila hawa Petro nimeangalia line up yao inaonekana wapo vizuri.

Kikosi chao kimajaa wabrazil na wareno, Mamelod akizubaa anatoka leo maana petro wataingia kipindi cha pili wakiwa na molari sana.

Mambo yakiwa hivi, naiona penalty wakipewa mamelod.
Moja moja huku Africa kusini
 
Je kwa Mkuu
Coefficient ya ubora wa ligi ndo unaamua timu zipi zianzie round ya ngapi? Na ligi hiyo iingize timu ngapi katika mashindano ya CAF.

Pamoja na unazi wangu wa Yanga, Simba imechangia Sana kukuza ubora wa ligi(coefficient ya ligi ya Tanzania katika list ya CAF. Na ilitokea kweli ikafikia hatua ya ligi yetu kutoa timu ya kuanzia round ya 2 badala ya kwanza basi tambua timu itakayokuwa ya 1 kwa ligi(bingwa) ndo atafaidika. So hata kama Simba wamiiwezesha ligi yetu kufikia ubora huo na Yanga akatwaa ubingwa then Yanga ataanzia round ya pili na atakayekuwa wapili likely Simba ataanza round ya kwanza ya playof
😂😂haha kwaio hata kama una 0.5 points unaanzia wa pili ausio kama hujui kitu bora unyamaze au uulize
 
Kwaio Mkuu kwa mfano Rs Berkane akachukua kombe la shirikisho si atafuzu Cafcl …
Halafu ikatokea hajamaliza nafasi ya 2 kwenye ligi kisheria atafuzu moja kwa moja ..Je Morroco atapeleka timu 3 au Mmoja anabidi apishe ?
 
Back
Top Bottom