Kwa lugha rahisi ni hivyo Corona Covid 19 HAKUNA Tanzania
Kwanini Hatukuweza kukaa lockdown kama ulivyo Sema Mzee mshana ??[emoji23]
Nadhani si sahihi kusema haipo.
Mimi naamini ipo.
Na pengine hata wewe ukienda kupimwa wanaweza kuikuta unayo.
Lakini waweza kuwa nayo na wala usiwe mgonjwa.
Na karibu asilimia 99 ya wanaoipata, wanapona.
Na wengi wa hao wanaoipata wala huwa hawaumwi kivile.
Na ndo maana umeona hata majuzi hapa Rais Trump alikutwa nayo na sasa keshapona na yuko fiti kabisa licha ya kuwa na umri mkubwa.
Mke wake, Melania Trump naye alikutwa nayo lakini hata spitali hakwenda.
Hata yule Rais wa Brazil, Bw. Bolsonaro naye aliipata na wala hakuwa mgonjwa.
Waziri mkuu wa Urusi naye aliipata. Hakuugua sana. Alipata vijimafua tu na vikapona vyenyewe.
Ndo maana mimi msimamo wangu kwa muda wote huu umekuwa kwamba, Corona si ugonjwa hatari kama ulivyotangazwa.
Mi mwenyewe hapa nahisi nilishaupata. Nikakohoa kwa siku mbili tatu, baadaye nikaanza kubanja, hatimaye nikapona. Hata wiki haikuchukua.