Kuna viongozi wanahujumu miradi ya SGR wakiwaza biashara zao za mabasi na malori zisife. Muda si mrefu tutaburuzwa mahakamani kwa kukiuka mkataba

Kenya kuna SGR na Mabasi na Malori bado yanafanyakazi.
Wabongo tunapenda sana kulalamika.
 
Kitu kikubwa kinacho umiza ni fedha zilizolala au zinaoza katika miradi hiyo.
Pili ni adha ya usafiri wa basi wanayopata wasafiri kuelekea pande hizo iwe Karagwe, Kagera,Chigoma,Mara na kadhalika.
Hasa wazee na watoto Kwani kwenda maliwatoni Kwa basi mpaka dereva aamue, tatizo jingine ni kukaa Kwa muda mrefu bila kunyosha miguu , tatu ni muda wa safari ambao unatarajiwa kupungua hivyo kuongeza tija katika uzalishaji na kufanya biashara.labda waseme kwamba Hawataki au juhudi za makusudi kuhujumu maendeleo ya mikoa husika na watu wake , ili walio nacho wabaki wao Tu na sio tabaka lililo chini Yao.
 
Wanaweza kufikiria hivyo. Ila wanakosea. Tanzania inahitaji Kuunganishwa ni nchi kubwa.

Malori, Mabasi, SGR, daladala Metro, Mwendokasi, bajaji, boda, uber, taxi, mkokoteni, baiskeli vyote bado vinahitajika na vitahitajika kwa miaka zaidi 20 ijayo. Ukizingatia SGR haitakamiliki leo au kesho na kukumbuka jinsi population ya Watanzania inavyoongezeka kwa kasi.
 
Tuna uongozi nashindwa hata kueleza kipi wamatekeleza na kujisifia nacho.

Leo nilikuwepo pale one stop centre pale temeke, jengo jipya umeme umekatika hata stand by generator hamna.
 
Kuna upigaji mkubwa. Ila mabasi na malori na SGR vinaweza kwenda pamoja.

SGR itakuwa expensive kidogo lakini usafiri wa haraka. Mabasi, malori cheap kidogo ila itatuma muda zaidi.

Watu wataamua. Nchi nyingi duniani zina hizi options zote.
Muda ni mali
 
Kwani Huwa Kuna uchagizi?
Zaidi ya watu kupandikizwa
Babu bul, natamani nikuite 'We CHADEMA wewe' ila nasita, kwa sababu waweza kuwa umelishwa tu hayo maneno na Wana CHADEMA kuwa, Huwa hakuna Uchaguzi Tanzania, kitu ambacho kitakuwa sio sahihi.

Kukujibu moja kwa moja, NDIO, huwa kuna Uchaguzi Tanzania. Unadai watu wanapandikizwa....Watu wanapandikizwa kivipi?

Kama wewe ni CHADEMA utaenda kususa tena?
 
Nimekuelewa chama Mabuzi ila Kila chenye mwanzo kina mwisho
Dalili ya mvua ni mawingu
 
Inawezekana waliopewa dhamana yakisimamia hii miradi walikuwa against mwanzilishi wake. Inawezekana waliopo wizara ya fedha walikuwa siyo wafuasi wa Magufuli.

Lakini kwa gharama zilizokwisha kutolewa kwenye miradi hii ni Busara zaidi kuacha kutoa fedha kwa miradi mingine nakuelekeza fedha kwenye miradi hii ikamilike angalau huduma zianze kutolewa tupate fedha za kulipa madeni. Leo wafanyakazi wa SGR wanagoma viongozi wapo wanaingia ofisini na kutoka hakuna tamko wala maelekezo yanayotolewa.

Tutaendelea kuchezewa hadi lini?
 
nakubaliana na hoja yako kwa asilimia 100, SGR inahujumiwa sana kuanzia kwa CAG hadi Bungeni.
 
Sijataja mtu anayekwamisha mkuu, nimetoa mfano tu ambao ndio uhalisia uliopo. Kumbuka siasa ni mchezo wa maslahi binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…