ngorokori
JF-Expert Member
- Sep 2, 2026
- 564
- 922
Yeah. Jana nilikutana na baba yangu mzazi sehemu fulani. Nilimkuta anamwambia fundi wake mkuu wa kujenga. Pesa haiwezi kununua Kila kitu kwahiyo inatupaswa tuwaheshimu wanaotufanyia kazi akatoa mfano Kuna jamaa yake aliwahi kumjibu mfanya kazi wake "Mimi ndy nakulisha wewe, wewe bila Mimi sio kitu huwezi kupata pesa". Mzee akasema mfanyakazi akasusa akamwambia boss chukua pesa zako ziweke hapo zikufanyie kazi yako Mimi naondoka. Boss Kwa jeuri akamwambia nenda aseeh mzee anasema walikuja watu kufanya hizo kazi walikuwa wanaharibu kazi vibaya sana, boss ilimbidi amtafute yule jamaa Tena ili akamfanyie kazi na jamaa aligoma kabisa akamwambia chukua pesa yako iweke hapo ikufanyie kazi.Mada nzuri na fikirishi ngoja nikite kambi hapa kupata shuhuda mbalimbali za wanajamii
Ila ni ukweli mtupu, Pesa si Kila kitu, Kuna vitu hata pesa haiwezi kuvinunua vikienda ni vimeenda.
Pesa ni muhimu lakini sio mbele ya Kila kitu.