Kuna vitu vinakwaza ila ndio uhalisia wenyewe


ndugu nina miaka 10 kazini out to speak this inshu hapa hamna sehemu nimewai kusema. na hii nimeandika ni kile nime-experience na sio mimi tu wengi tu yanawakuta haya na ni mbaya sana in mental healthy.
mi sijazungumza ubaya wake tu ndo mana nimeonesha kuheshimu mchango wake pitia vizuri io thread yangu.

Na kama atamaindi ni sawa tu mana hata mimi kuna time nilimaindi pia..ila jaribu kuexperience kitu hiki
 
Mkuu mfikishie maneno yangu haya👇👇.

Mwambie hata bila yeye wewe ungelifika hapo kwa sababu Mungu ndie alipanga wewe ufike hapo kupitia yeye.

Hivyo yeye asingekuwepo basi Mungu angemtumia Mtu mwingine kukufikisha wewe hapo.

Lengo la Mu gu ni wewe ufike hapo na wala lengo halikuwa yeye akusaidie,kwa hivyo kama lengo la Mungu ni wewe ufike hapo basi Mungu hutumia njia tofauti kukufikisha,basi kwa nini hizo njia zinajisifu kwamba ndio zimekufikisha wakati zimepata bahati tu ya kutumika kuelekea kwenye lengo kuu ?

Ukiona mtu anajisifu kumsaidia mtu fulani basi ujue bado hajayaelewa maisha na hajajifunza kitu katika maisha haya.

Watu ambao wameyaelewa maisha husaidia wenye shida na kusahau kwa sababu wanafahamu kwamba hata bila wao basi hao wenye shida wangesaidiwa na wengine kufikishwa kwenye lengo la Mungu.

Kwa mantiki hiyo mtu ambaye anatoa msaada ndio ambaye anatakiwa kujiona ana bahati sana kwa kule Mungu kumchagua yeye kwani Mungu ana machaguzi mengi tukiachilia mtu huyo.
 
Ukikosa ajira unalalamika, ukipatiwa ajira unalalamika...maneno yanazuia pesa kuingia kwa akaunti yako?

Ikiwa bado unaogopa kusemwa basi una safari ndefu sana
 
Umetaja godfather nikamkumbuka vito corleone baba la ma mafia. A friendly man, a just man , a reasonable man. The deadliest lord of cosa notra.
 
Kwani akikusema uñapungukiwa nini?
Ukitaka ujue umuhimu wake,acha hiyo kazi,uje mtaani upambane kutafuta ajira mwenyewe.Ukute aliwahikuongelea mara moja au mbili,ila watu wanakufikishia habari mbaya,kwa manufaa yao,labda kuona unakereka ndo furaha yao au wanajua historia yako na huyo mzee,hivyo wanaunda maneno ambayo wewe ni rahisi kuamini.Endelea na maisha ndugu yangu.Shukuru umeunganishiwa ukapata kazi.Hizo fursa zinatafutwa sana.Mpuuze kama una uhakika kweli yeye anakusemasema.
 
Mkuu uwe unakumbuka fadhila "ngoja niishie hapo tu au basi ngoja niendele," nyie ndio mnaifanya watu wajute kusaudia watu wengine mkishapandishwa juu mnapandishaga mabega na kudharau waliowafikisha huko.
 
Jifunze kuishi na watu mkuu waswahili wanasema jifunze kula na kipofu watu tupo tofauti "nobody is perfect" hiyo hali chukulia kama udhaifu wake hapo sahivi unaongea ivo kwakuwa umekaa kwenye maokoto mambo yamenyooka unasahau ulipotoka ila sishangai kwa binadamu wasio na fadhila ni kawaida sana.

Hii kwenye saikolojia ni kawaida sana watu wakimsaidia mtu akitusua lazima ajitambe na atoe mfano kwa wengine huwa wanajisikia amani sana.

Binafsi mzee wa ivo me ningekuwa nikikutana nae tu namjaza mzee shikamoo aisee mzee umenitoa mbali bila wewe sijui ingewaje Mungu akuweke sana kama kuna staff wengine unasema kwa sauti aisee bila huyu mzee nisingekuwa hapa mpka nimejenga na kuwa biashara za hapa na pale ni jitihada za huyu mzee naweza sema amekuwa kama baba kwangu mbona simple.Unamjaza tu kwa maneno ya hapa na pale na yeye anasikia raha then unaendela na mambo yako

Ila nilichokiona wewe na wenzio mmesahau mlipotoka na kuota mapembe na kwako na wenzio huyo mzee mnamuona jau kwakuwa masikin akipata matako hulia mbwata.

Usimchukulie simple mtu aliyekutoa matopeni na kukupa maisha ndio watu kama hao hutumwa na Mungu

Me watu walinigusa wakati wa shida nawaheshimu sana au mtu atokee anipe mchongo aisee kwangu atakuwa Mungu wakitoka Mungu mwenyewe na wazazi.

All in all hapa umeandika tu kusema unathaamin mchango wake lakini deep down sio kweli unamuona mzee watu jau.
 
Hehehe....dah
 
Mkuu uwe unakumbuka fadhila "ngoja niishie hapo tu au basi ngoja niendele," nyie dio mnaifabya watu wajute kusaudua watu wengine mkishapandishwa juu mnapandisga mabega na kudharau waliowafikisha huko
Masikini akipata matako hulia mbwata washahau walipotoka hafu wapo wenzie

Hapo juu jamaa kamuuliza swali zuri sana kuna mchongo wa kazi je ukatae au ukubali ila uwe unatangazwa na hapo upo njaa kali.kakubali bora atangazwe sahiv kashashiba anasahau alipotoka

Hawa ni dizaini ya watu hawataki kuonekana wameingia kazini kwa mchongo(connection)wanaona kama staff wenzao watawachukulia poa.
 
kabisa
 
kizuri sijaficha connection yake kwangu na nimemshukuru pia mbona...
swala ni nyinyi mnaotusaidia mnatutangaza sana kama bila ninyi hamna kitatokea...Acheni io tabia
 
Mkuu uwe unakumbuka fadhila "ngoja niishie hapo tu au basi ngoja niendele," nyie ndio mnaifanya watu wajute kusaudia watu wengine mkishapandishwa juu mnapandishaga mabega na kudharau waliowafikisha huko.
na hata tunaosaidiwa inafikia hatua tunajuta kupokea misaada yenu pia...
 
kizuri sijaficha connection yake kwangu na nimemshukuru pia mbona...
swala ni nyinyi mnaotusaidia mnatutangaza sana kama bila ninyi hamna kitatokea...Acheni io tabia
Asa si ndio ukweli, bila yeye hakuna kitu kilitokea.
Au kilitokea?
 

Asa si ndio ukweli, bila yeye hakuna kitu kilitokea.
Au kilitokea?
sijakataa mkuu hata ukisoma heading yangu mbona ipo wazi lakini hahah
 
Usiyape muda ayasemayo we komaa na mambo yako ila kuna binadamu wanapenda sana Umungu mtu, waabudiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…