Kuna Wabunge 37 ‘haramu’ bungeni ambao hawatambuliwi na Katiba

Kuna Wabunge 37 ‘haramu’ bungeni ambao hawatambuliwi na Katiba

Hivi Kasim Majaliwa Majaliwa Alipigowa kura??
Aah wapi. Huyu alimteka mgombea ubunge wa chadema akiwa mlango wa ofisi ya mkurugenzi anataka kurudisha fomu.

Akatuma watu waliojitambulisha kama maaskari na kuanza kumpiga mgombea wa chadema mbele ya mkurugenzi.

Wakamnyang'anya fomu na kumfungia chumbani next to the ofisi ya mkurugenzi. Halafu wakamwachia muda ukiwa umeisha.

Nadhani unakumbuka waliweka siku ya kurejesha fomu ilikuwa moja .

That man is an animal.

Nina pdf ya maovu yake yote huyu jamaa.
 
Aisee hadi Kigwangala na u-much know wote ule ila akaogopa kuingia kwenye sanduku la kura
Mkuu. Umesahau Yale matunguli na Lile jopo la waganga waliomgangua akiwa uchi akaganguka mpaka wapinzani fomu hawakuziona.
Yeye Ni Kati ya ma dokta wanaoamini uchawi na waganga wa kienyeji. Humkosi na hirizi inayomlinda popote anapokwenda.
 
Mihemko ya chama hiyoo mkuu, katiba mpya ni ya watanzania wote, ila kwa nyie mliopo kwenye system ndo mnaipinga kutetea ugali wenu.Aibu
Hii lugha jumuishi umemuuliza baba yako,mama ,shangazi ,mtoto, rafiki ,mke wakasema wanahitaji katiba mpya? ,acha kuwalisha watu takwa lako ukasema letu ,mbona Mimi sihitaji hiyo katiba mpya na ni mtanzania kweli kweli
 
Wabunge 19 wasio na chama na Wabunge 18 waliopita bila kupingwa.

Ibara ya 66; Kutakuwa na aina zifuatazo za wabunge,

1. Wabunge wa kuchaguliwa majimboni.
2. Wabunge wanawake wa viti maalumu.
3. Wabunge wa kuteuliwa na rais.

Hao wasio na vyama na waliopita bila kupingwa wameandikwa kwenye Ibara gani.

Hivi siku mgombea urais akibaki peke yake uchaguzi hautafanyika? yaani hatutampigia kura ya NDIO au HAPANA? na automatically NEC itamtangaza kuwa Rais?

Ndio maana sisi wengine tunapodai Katiba mpya muwe mnatuelewa ni pamoja na kuondoa utata kama huu.
===============

Wabunge waliopita bila kupingwa.

1. Ushetu - Elias Kwandikwa
2. Kongwa - Job Ndugai
3. Gairo - Ahmed Shabiby
4. Kilosa - Palamagamba Kabudi
5. Mvomero - Jonas Van Zeeland
6. Morogoro Kusini - Kalogereris Innocent
7. Morogoro Mashariki - Taletale Hamis Shabani
8. Mlele - Eng. Isaack Kamwelwe
9. Kavuu - Geofrey Pinda
10. Songwe - Philipo Mulugo
11. Bukene - Zedi Jumanne
12. Nzega Vijijini - Hamis Kigwangalla
13. Ruangwa - Kassim Majaliwa
14. Mtama - Nape Nnauye
15. Namtumbo - Vita Kawawa
16. Butiama - Sagini Abdallah
17. Misungwi - Alexander Mnyeti
18. Bumbuli - January Makamba
mbona katiba ya sasa imewakataa na hujafanya kitu?
 
Hii lugha jumuishi umemuuliza baba yako,mama ,shangazi ,mtoto, rafiki ,mke wakasema wanahitaji katiba mpya? ,acha kuwalisha watu takwa lako ukasema letu ,mbona Mimi sihitaji hiyo katiba mpya na ni mtanzania kweli kweli
Sio lazima hadi watanzania wote wakubali ndio katiba iandikwe.
 
mbona katiba ya sasa imewakataa na hujafanya kitu?
Kila mmoja ana wajibu na sehemu yake ya kuilinda katiba, rais ana sehemu yake wabunge wana sehemu yao na mwananchi wa kawaida kama mimi nina sehemu yangu, ile kuonyesha tu kuwa katiba imevunjwa nimetimiza wajibu wangu wa kuilinda.
 
Ndugai amelinajisi Bunge muda mrefu tu tangu 2015 hadi sasa hakuna Bunge ni wachumia tumbo wamejazana mule....wapitishe milele hadi iwe life sasa nashangaa kazi imerahisoshwa wao bado wapo kwa nini
 
Back
Top Bottom