Kuna Wabunge 37 ‘haramu’ bungeni ambao hawatambuliwi na Katiba

Uchaguzi Mkuu 2020 CCM walifanya vitendo vya aibu sana kwa nchi - Dawa yao ni KATIBA MPYA, watake wasitake.
 
Uchaguzi Mkuu 2020 CCM walifanya vitendo vya aibu sana kwa nchi - Dawa yao ni KATIBA MPYA, watake wasitake.
Ilikuwa aibu kubwa sana, ndio sababu hata uchaguzi ulipotangazwa, hakukua na shamra shamra kama zile tulizozioea miaka yote.
 
Pamoja na Katiba hii ya nchi tuliyonayo kukanyagwa na watawala, vilevile wabunge kule bungeni kupitisha miswada na kubariki sheria kandamizi bado sio rahisi kwa Watanzania kuandamana.

Hii ni kwasababu wapinzani wanaotaka kuwaingiza watanzania barabarani kupigania Katiba mpya kwa damu na jasho hawana ushawishi wowote kwa Watanzania wenye maisha ya chini.

Ukiangalia vipaumbele vyao kwenye katiba vimekaa katika upande mmoja yaani kisiasa. Utasikia, Tume huru, Kupunguza madaraka ya Rais, serikali tatu, Mbunge kuwajibishwa, uhuru wa maandamano na mikutano ya kisiasa n.k, hivyo wanapigania ili kupata ulaji wao na sio maslahi mapana ya Watanzania na kizazi kijacho kama wanavyotulaghai.

Watanzania ukitaka waingie barabarani waambie mambo yanayowahusu wao sio mambo ya kisiasa. Watanzania wanatamani kusikia maandamano ya;

1. Kuondoa kodi kandamizi
2. Kudai huduma bora na nafuu za afya
3. Ajira za uhakika kwa vijana wao
4. Mazingira wezeshi ya kujiajiri
5. Mikopo yenye riba nafuu na himilivu
6. Uhakika wa nishati ya umeme kwa gharama ndogo.
7. Uhuru wa kufanya biashara mipakani
8. Ushirikishwaji wa moja kwa moja wa wananchi kwenye mambo ya kitaifa. Kuliko wabunge wengi waliokaa kisiasa bungeni kazi kula hela ya walalahoi.

Lakini wapinzani wanatueleza mambo yao ya kisiasa ili tuwasapoti kwa kuingia barabarani. Hilo haliwezekani. Hakuna mtanzania mjinga kuwapigania ulaji wenu wakati mkipata madaraka mnatusahau na kujaza matumbo yenu.

Vijana wana hasira na chuki kali na wanasiasa, wamechoka kutumika na ahadi hewa. Vugu vugu la mabadiliko ya kweli litaletwa na vijana na sio wanasiasa wa upinzani wenye kuangalia maslahi yao.
 
Usichanganye sheria na katiba, unataka katiba izungumzie upatikanaji wa umeme? masuala ya kodi sijui biashara haya yanashughulikiwa na sheria na kanuni zake.
 
Usichanganye sheria na katiba, unataka katiba izungumzie upatikanaji wa umeme? masuala ya kodi sijui biashara haya yanashughulikiwa na sheria na kanuni zake.
Angalia vizuri bandiko langu. Nimetaja hayo mambo ambayo yanaweza kumshawishi mwananchi wa kawaida kuingia barabarani.

Suala la katiba limekaa kisiasa. Na ipo siku vijana watafanya reformation kwa sababu ya kuwachukia wanasiasa (wote).
 
Kikwete aliporuhusu kuandikwa kwa katiba mpya 2014 kuna mtu aliandamana.
 
Wabunge waliopita bila kupingwa, maana yake ni waliochaguliwa na kushinda kwa asilimia 100, na hivyo kupelekea kukwepesha gharama za uchaguzi kwa Taifa. Hawa ndiyo wabunge halali kwa iwango cha juu zaidi kuwazidi hata wale wengine walioshinda kwa asilimia pungufu ya 100%
 
UNAJUWA UKIWA UNA NJAA KALI LAZIMA UTAANZA KUFIKIRIA KWA KUTUMIA NJIA YA HAJA KUBWA TU SASA WEWE KAMA MGOMBEA AMEBAKI PEKEYAKE HAKUNA WA KUSHINDANA NAYE UTAMWITAJE SI KAPITA BILA KUPINGWA? ACHENI UNGESE WENU CHADOMO
 
Mihemko ya chama hiyoo mkuu, katiba mpya ni ya watanzania wote, ila kwa nyie mliopo kwenye system ndo mnaipinga kutetea ugali wenu.Aibu
hivi hii katiba iliyopo unaona haifai yote au ina mapungufu ambayo yanaweza kufanyiwa amendment?
 
Nani aliwapigia kura je tukisema walipata 0% kwa vile hakuna kura hata moja iliyohesabiwa utasemaje.
 
UNAJUWA UKIWA UNA NJAA KALI LAZIMA UTAANZA KUFIKIRIA KWA KUTUMIA NJIA YA HAJA KUBWA TU SASA WEWE KAMA MGOMBEA AMEBAKI PEKEYAKE HAKUNA WA KUSHINDANA NAYE UTAMWITAJE SI KAPITA BILA KUPINGWA? ACHENI UNGESE WENU CHADOMO
Alichaguliwa na nani? waliojitoa ni wagombea sio wananchi angalau wangepigiwa kura za NDIO au HAPANA.
 
Nani aliwapigia kura je tukisema walipata 0% kwa vile hakuna kura hata moja iliyohesabiwa utasemaje.
Kwani mantiki inayopelekea watu kupiga kura ni ipi? Kura inapigwa ili kuthibitisha mgawanyiko wa mawazo ya wapiga kura juu ya mgombea au wagombea wao. Kama mgawanyiko wa mawazo kwa wapiga kura haupo, kupiga kura kunakosa mantiki na kinakuwa ni kitendo cha kupoteza muda na rasilimali za wapiga kura.
kwa hiyo, waliostahili kuiga kura wanakuwa wameamua kitu fulani kifanyike na hicho ndicho kinachopelekea ushindi wa mpigiwa kura. Wapiga kura wanaamua kitu "mbadala wa kupiga kura" ambacho kinapelekea mgombea kupita. Kwa hiyo si kila mara zote mtu anapita kwa kupigiwa kura kwenye ballot box
 
Natoa siku 7 wawe wametubu. Narudia tena natoa siku 7 wawe wametubu. Narudia kw mara ya mwisho, natoa siku 7 wawe wametubu. Vinginevyo mmoja baada ya mwingine wataanza "kwenda peponi".

Una usafiri wa kuwapeleka huko au ndio upo huko una waandalia makao..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…