Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Tena mwenye matokeo mazuri kuanzia O-Level mpk GPA ya Hatari

Chai hii
Mbona wengi sana hao, na muda si mrefu tutakuwa kama Nigeria muuza mahindi ana degree zake kadhaa. Vyuo vinatoa wahitimu na soko la ajira halina uwezo wa ku absorb.
Mtoto wa jirani yangu saa hii yupo bize kujifunza kushona na cherehani, hakuwahi kufeli toka na msingi hadi gegree usdm, na hana kazi. Unaweza kutoa chozi akikuonesha vyeti vyake
 
Mkuu,
Na shida na mwalimu wa kunifundisha kiingereza naomba uniunganishe nae akute ananinoa wakati anasikilizia ajira
 
Kama unaweza msaidie mkuu.
 
Ni kweli wapo wengi sana ila kwa performance aliyoelezewa huyo na sifa za muonekano wake angeomba hata kufanya kazi kwny maofisi ya watu au kuvolunteer ila sio kuuza bar

My own observation lakini
 
Watu wanawachukulia wahudumu wa bar kama Malaya,kama watu wasiyofaa

Hii siyo kweli

Huku nyuma Kuna maumivu makali mnoo ila Mungu ndiye anayejua
Sehemu inavyowachukulia wahudumu wa bar inaonesha mengi kuhusu maadili ya sehemu hiyo. Na mengine ni matatizo ya umasikini na ujinga tu.

Habari kama hizi zinanikumbusha mtoto mmoja Italian American nilifanya naye kazi hapo Wall Street, New York, New York. Mtoto kakaa kama Julia Roberts, aki smile unaweza kusahau kazi ukawa unamuangalia tu, mtoto mcheshi, mtoto anatoka familia bora baba yake alikuwa mkurugenzi mmoja mkubwa katika benki mashuhuri.

Licha ya yote hayo, huyo Julia lookalike alikuwa mcheshi sana. Sasa kila Ijumaa ilikuwa tunaulizana mipango ya weekend imekaaje? Siku moja akaniuliza, nikamwambia mipango yangu. Nikamuuliza na yeye, atafanya nini?

Jibu alilonipa lilinishangaza sana kwa binti ambaye nilimuweka matawi ya juu kama yeye. Aliniambia atakuwa anahudumia katika bar (bartend). Nikashangaa sana, mtoto mzuri, mwenye elimu, aliyetoka familia bora kama huyu anaenda kuwa barmaid tena?

Akanifafanulia zaidi, akasema huwa anafanya hivyo mara nyingi, bar yenyewe baba yake ni kati ya wanaoimiliki, halafu watu wanaokuja ni kama wanajuana wote, na kisha, anaipenda hiyo kazi kwa sababu anapata ku interact na watu sana na kumix vinywaji, zaidi, anapiga hela ndefu sana kwenye tips (huku kila mtu anayehudumiwa analipa bakhshishi/tip kwa mhudumu). So akasema huwa anapata mpaka dola za Kimarekani 500 kwa usiku mmoja kutokana na tips hizo.

Nikapata somo kubwa sana kwamba inawezekana kwa mwanamke mwenye heshima zake, mzuri, kijana, anayefanya kazi Wall St., anayetoka familia bora, akafanya kazi ya uhudumu wa bar, bila kuonekana malaya.

Nilijifunza pia kuwa wenzetu wanaheshimu sana kazi, yani huyu dada hakuona haya kusema kuwa yeye anafanya uhudumu bar, aliona fahari kuwa anafanya kazi, anatumia ujuzi wake wa ku mix vinywaji, anafanya kazi inayompa social interaction nzuri kwa family and friends, na anapata kipato kizuri cha ziada.

Na zaidi, nilijifunza kuwa wanaume wanaweza kwenda bar na kuwaheshimu wahudumu kwa kunywa vinywaji vyao bila kuwabugudhi wahudumu, na zaidi, kwa kuwapa tips nzuri tu zitakazoonesha wanathamini kazi zao.

Je, na sisi hatuwezi kuweka jamii inayojali kama hivi?
 
Situation kama yako hii wakati nikiwa chuo nilikua naingia room alone nafumba macho halafu nasema hivi"Baba kama ndio huyu naomba iwe kama siyo muondoe kwenye maisha yangu na fikra zangu kabisa""

Aiseh nilipoteza visu vingi Kwa style hiyo,siku nilipokutana na huyu niliomba Ivo Ivo aiseh ikawa kinyume chake nikajue ni yeye Baba kamleta!!

Lakini Sasa naambiwa Kuna mwingine anakuja coz huyu nilipomfikisha panatosha anataka kujitawala !!na mimi napokea eeh Baba!!namtaka yuleee nadhani unajua!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…