Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Niliwahi kutana na barmaid kalaza one ya o level, three ya pcb na bachelor ya environmental science!!

Sikumlaaaaa! Tulikuwa marafiki Hadi akapotea.

Bamed wa digrii za ualimu, Sheria nk ni wengi mmno.
Duh environment science ya SUA iyo ni ngumu balaa.me cjawai kukutana na wasomi.

Sema ni Hali ya maisha tu.
 
Mbona wengi sana hao, na muda si mrefu tutakuwa kama Nigeria muuza mahindi ana degree zake kadhaa. Vyuo vinatoa wahitimu na soko la ajira halina uwezo wa ku absorb.
Mtoto wa jirani yangu saa hii yupo bize kujifunza kushona na cherehani, hakuwahi kufeli toka na msingi hadi gegree usdm, na hana kazi. Unaweza kutoa chozi akikuonesha vyeti vyake
Hali mbaya alisoma kozi gan?
 
Jana nilipita Baa Moja hivi usiku mkali kula, nikakuta ndio Bar inakaribia kufungwa. Ghafla nikasikia malumbano kati ya Meneja wa Baa na kabinti kamoja hivi (waitress). Kumcheki yule waitress sikuamini. Mrefu, ana rangi ya udhurungi, shape ya kwenda, pua ya kisomali halafu nywele mpaka mgongoni! Baada ya malumbano yule binti mhudumu akawa analia.

Malezi niliyopewa na wazazi wangu ni kusababisha tabasamu kwa wengine, ingawa sababu ya ziada ni uzuri wake pia, nikamuita yule waitress, nikamuuliza kulikoni mbona malumbano? Akaniambia, "kaka angu, tangu nianze kazi hapa nina siku ya 9, kila mhudumu wa kike ananichukia wanadhani nitawachukulia mabwana zao, kumbe mimi natafuta maisha".

Nikapatwa na simanzi sana. Nikamwambia basi usilie, agiza kinywaji. Akasema na kazi anaacha. Eeh! Nikashtuka, akamuuliza kaunta anamdai sh ngapi ya vinjwaji, akamlipa hela yote, akaniambia kaka angu kama unataka kuninunulia bia twende ukaninunulie kwengine ila silali na wewe, nikamwambia poa. Kumbe ananipeleka sehemu ambayo atakutana na mwenyeji wake.

Tukahama joint, tukafika kwenye night club Moja hivi, akawa anakunywa bia kwa hasira kama mtu mwenye msongo hadi nikawa namzuia, wakati tuko pale akaja dada mmoja ambaye nilimuacha primary madarasa mawili, anamuita yule waitress dada, nikamuuliza vipi mnafahamiana? Akasema huyu ni mtoto wa marehemu mama mkubwa na mimi ndio nimempokea hapa mjini anaishi kwangu, ana matatizo makubwa, na yeye ndio kanitumia msg yuko hapa ndio nimekuja, yule waitress akafurahi kuona nafahamiana na ndugu yake.

Tamaa zikanijaa, nikamuomba sana niondoke naye kwasababu mimi sio stranger kwake tena kwasababu nafahamiana na ndugu yake, akaanza kumuuliza ndugu yake mara mbilimbili kwamba unamuamini huyu kaka? Ndugu yake akamjibu ndio, namfahamu sana tangu tukiwa Primary. Ikabidi ndugu yake aniapize kwamba sitafanya ufirauni [emoji2]

Tukaondoka, nikam-drop mdg mtu kwake, nikasepa na manzi. Tumefika kwangu aisee story aliyonipa inahuzunisha sana. Aliolewa miaka 2 iliyopita na mwanaume ambaye alikuwa na familia mkoani. Yeye akiwa amaemaliza Shahada yake ya kwanza ya BAF (Bachelor of Accounts and Finance) na kazi nzuri, mwanaume akamshauri aache kazi, kwa mapenzi binti akaacha kazi. Mwaka mmoja baadaye mwanaume akaanza kumnyanyasa, na ndio akagundua kwamba mwamba alikuwa ana mke na watoto 4 mkoa X!!! Kumbe binti ni yatima na alizaliwa kwao peke yake. Anachoshukuru ni hakuzaa na yule mwanaume kwasababu mwanaume hakutaka kuzaa nae kwa wakati ule.

Nikamuuliza kwanini auze bar na taaluma yake? Akasema ilibidi akimbie ule mkoa alipoolewa aje mkoa huu kuficha aibu na kuwasahaulisha watu, na akaona hawezi kukaa tu kwa ndugu yake bila kujishughulisha na chochote wakati anatafuta ajira. Kikubwa zaidi kwenye ile bar aliyoacha kazi hakuna mtu aliyekuwa anajua binti ni msomi, alijishusha afanane nao, nikamuuliza kazi umeacha kweli? akanijibu nimeacha kaka.

Baada ya zile story usiku wa jana nikamwambia haya lala mama. Asubuhi wakati naamka nakuta kavaa pensi na t-shirt yangu vyombo vyote kaosha, nguo chafu kafua, kuna sufuria nilitakaga kuzitupa ila kaziosha zimekuwa nyeupe kama theluji. Nikamuomba anioshe vyeti soft copy, aisee ni kichwa hasa, O na A level ni vijiti tu, Sekondari zote kasoma za kike. Chuo GPA KUBWA!

Mchana nikampa maelekezo asipike nitamuagizia Chakula ikabidi sasa nimtafute yule ndugu yake akaanza ku-verify zile taarifa alizonieleza Binti. Wakuu Mimi sijaoa, il Kuna Binti ambaye nilikuwa namfikiria fikiria kumuoa ila hili ni jaribu kwakweli. Yani huu ni wakati mgumu sana napitia, sielewi kwakweli. Sijamfanya kitu tangu Jana. Sasa hivi ndio nimeingia kwangu na msosi wake namuangalia tu hapa namna alivyotulia kwenye kochi anatazama tamthilia.
Kawaida sana aseee.... Kuna mshkaji .. nafikiri nilishahadithiaga humu...kipindi tunamaliza chuo SAUT 2008/9... Kuna mshkaji tulikuwa tunasoma naye ila yeye alikuwa tayari kazini alikuwa mwanajeshi.... Alipata demu mkali kinyama RUMORS CLUB.... Tukaenda naye mpaka magetoni ..Sasa mitungi mingi na tumekesha tukapitia Royal Pub piga mamtori ndio tukaenda magetoni .... Jamaa mchanamchana hivi watu wimbi ndio linakata flani akatushtua Wana oya njooni ...bar flani IPO bondeni ndio akaanza kutupa story za yule manzi.... Jamaa alioa kabisa yani.... Na yupo naye mpaka wa Leo na demu ni mtulivu kinyama yani huwezi dhani kama alimpatia mazingira yale. Kifupi demu ndio alikuwa ameanza kazi ya pale club ya uhudumu... Mchana anatembeza uji soko la langolango usiku anauza hapo Rumors club... Baba yake alipata ajali akavunjika miguu .... Noma sana. Walikuwa wanakaa maeneo ya mto. Mirongo upande wa makaburi ya waislamu. Tulienda na mshkaji mpaka kwao aseeee..... Jamaa alichukua jumlajumla.
 
Back
Top Bottom