Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Kila field huwa akili za wahusika zinafanana hata ukiingia na tabia zako tofauti wakongwe watakuonesha mambo yanavyoenda nawe utafanana na uliowakuta. Wanacholipwa mabaamedi ni kidogo sana... kinachowawezesha kuishi ni umalaya, kuachiwa chenchi na kubambikia bill wateja.
Endeleeni kujidanganya.
 
Mkuu, kama tyr kaingia kwenye mfumo ishi nae tu. Af ukizingatia kaletwa na mungu kabisa na ndugu yake kakuachia,. Bahati hazijirudii ila kumbuka unaweza kuwa umechezewa mchezo, hilo nalo lipo
Asante kwa ushauri mkuu, nitakuwa muangalifu sana.
 
huwa nawachukulia hivyo na wale wa salon za kiume. najua tu amevaa vibaya hapendi ila maisha yamemfikisha hapo. sijawahi kuacha kuwapatia walau alfu 5 ya soda wakimaliza kazi. zamani nilidhani ni ndogo nikaja gundua wakiniona wanagombania kabisa, wanajua tayari lunch siku hiyo wamepata. huwa naandaa kabisa bajeti nikitaka kwenda kunyoa. nafanya hivyo kwa upendo tu na mahubiri wanapata vilevile.
Ubarikiwe sana mkuu.
 
SI KILA MHUDUMU WA BAR NI MALAYA,, Kuna Bar flani kipindi npo Dom ilikua na mhudumu mzuri tu hv alikua mchangamfu sana alikua kila akiniona ananchangamkia sasa siku moja sikutaka mchezo nilimpangilia vzuri tu na nkamuahidi dau zuri tu lakn alikataa katukatu kwakua ndo walikua wanakalibia kufunga siku hyo akaniahidi nitafute siku nzuri na sehemu nyngne tupige story na anipe background ya maisha yake Aloooohh Trust me si kila mhudumu ni Malaya ni Shida tu ndo zinazowakabili na ni wachache sana wanaoshindwa kutoka kwny huo mtego..
Asante sana kwa ushuhuda huu mkuu.
 
Back
Top Bottom