Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Kuna wadada wema tu ila wanauza Baa, shida hizi

Jana nilipita Baa Moja hivi usiku mkali kula, nikakuta ndio Bar inakaribia kufungwa. Ghafla nikasikia malumbano kati ya Meneja wa Baa na kabinti kamoja hivi (waitress). Kumcheki yule waitress sikuamini. Mrefu, ana rangi ya udhurungi, shape ya kwenda, pua ya kisomali halafu nywele mpaka mgongoni! Baada ya malumbano yule binti mhudumu akawa analia.

Malezi niliyopewa na wazazi wangu ni kusababisha tabasamu kwa wengine, ingawa sababu ya ziada ni uzuri wake pia, nikamuita yule waitress, nikamuuliza kulikoni mbona malumbano? Akaniambia, "kaka angu, tangu nianze kazi hapa nina siku ya 9, kila mhudumu wa kike ananichukia wanadhani nitawachukulia mabwana zao, kumbe mimi natafuta maisha".

Nikapatwa na simanzi sana. Nikamwambia basi usilie, agiza kinywaji. Akasema na kazi anaacha. Eeh! Nikashtuka, akamuuliza kaunta anamdai sh ngapi ya vinjwaji, akamlipa hela yote, akaniambia kaka angu kama unataka kuninunulia bia twende ukaninunulie kwengine ila silali na wewe, nikamwambia poa. Kumbe ananipeleka sehemu ambayo atakutana na mwenyeji wake.

Tukahama joint, tukafika kwenye night club Moja hivi, akawa anakunywa bia kwa hasira kama mtu mwenye msongo hadi nikawa namzuia, wakati tuko pale akaja dada mmoja ambaye nilimuacha primary madarasa mawili, anamuita yule waitress dada, nikamuuliza vipi mnafahamiana? Akasema huyu ni mtoto wa marehemu mama mkubwa na mimi ndio nimempokea hapa mjini anaishi kwangu, ana matatizo makubwa, na yeye ndio kanitumia msg yuko hapa ndio nimekuja, yule waitress akafurahi kuona nafahamiana na ndugu yake.

Tamaa zikanijaa, nikamuomba sana niondoke naye kwasababu mimi sio stranger kwake tena kwasababu nafahamiana na ndugu yake, akaanza kumuuliza ndugu yake mara mbilimbili kwamba unamuamini huyu kaka? Ndugu yake akamjibu ndio, namfahamu sana tangu tukiwa Primary. Ikabidi ndugu yake aniapize kwamba sitafanya ufirauni [emoji2]

Tukaondoka, nikam-drop mdg mtu kwake, nikasepa na manzi. Tumefika kwangu aisee story aliyonipa inahuzunisha sana. Aliolewa miaka 2 iliyopita na mwanaume ambaye alikuwa na familia mkoani. Yeye akiwa amaemaliza Shahada yake ya kwanza ya BAF (Bachelor of Accounts and Finance) na kazi nzuri, mwanaume akamshauri aache kazi, kwa mapenzi binti akaacha kazi. Mwaka mmoja baadaye mwanaume akaanza kumnyanyasa, na ndio akagundua kwamba mwamba alikuwa ana mke na watoto 4 mkoa X!!! Kumbe binti ni yatima na alizaliwa kwao peke yake. Anachoshukuru ni hakuzaa na yule mwanaume kwasababu mwanaume hakutaka kuzaa nae kwa wakati ule.

Nikamuuliza kwanini auze bar na taaluma yake? Akasema ilibidi akimbie ule mkoa alipoolewa aje mkoa huu kuficha aibu na kuwasahaulisha watu, na akaona hawezi kukaa tu kwa ndugu yake bila kujishughulisha na chochote wakati anatafuta ajira. Kikubwa zaidi kwenye ile bar aliyoacha kazi hakuna mtu aliyekuwa anajua binti ni msomi, alijishusha afanane nao, nikamuuliza kazi umeacha kweli? akanijibu nimeacha kaka.

Baada ya zile story usiku wa jana nikamwambia haya lala mama. Asubuhi wakati naamka nakuta kavaa pensi na t-shirt yangu vyombo vyote kaosha, nguo chafu kafua, kuna sufuria nilitakaga kuzitupa ila kaziosha zimekuwa nyeupe kama theluji. Nikamuomba anioshe vyeti soft copy, aisee ni kichwa hasa, O na A level ni vijiti tu, Sekondari zote kasoma za kike. Chuo GPA KUBWA!

Mchana nikampa maelekezo asipike nitamuagizia Chakula ikabidi sasa nimtafute yule ndugu yake akaanza ku-verify zile taarifa alizonieleza Binti. Wakuu Mimi sijaoa, il Kuna Binti ambaye nilikuwa namfikiria fikiria kumuoa ila hili ni jaribu kwakweli. Yani huu ni wakati mgumu sana napitia, sielewi kwakweli. Sijamfanya kitu tangu Jana. Sasa hivi ndio nimeingia kwangu na msosi wake namuangalia tu hapa namna alivyotulia kwenye kochi anatazama tamthilia.
Acha Wenge,

Analysisi ya siku 1 au 2 au wiki haitoshi kujustify kuwa flani ni Mke mwema

Aliyokuambia yote umeyaamini? Kama ana mtoto alimuacha kwao utajuaje?

Amewaambia Washkaji wangapi? Mbona hawajamchukua?

Btw, nitumie namba yake nithibitishe uyasemayo

Dunia hadaa
 
Wewe ni mgeni na wahudumu wa bar.... Utakuja kupigwa na kitu kizito!!! Yaani we umeopoa siku ya kwanza tu unajiona mjanja? Jiulize kabla yako wameopoa wangapi ndugu, na wote mmepewa story hio hio, hata kama maisha magumu kiasi Gani mwanamke anayejua thamani yake hawezi kufanya kazi bar, period!!!
Tena mwenye matokeo mazuri kuanzia O-Level mpk GPA ya Hatari

Chai hii
 
H
Wewe ni mgeni na wahudumu wa bar.... Utakuja kupigwa na kitu kizito!!! Yaani we umeopoa siku ya kwanza tu unajiona mjanja? Jiulize kabla yako wameopoa wangapi ndugu, na wote mmepewa story hio hio, hata kama maisha magumu kiasi Gani mwanamke anayejua thamani yake hawezi kufanya kazi bar, period!!!
Hauko sahihi na hujui shida. Kuna msemo mwenye shida ni hanithi hata kama rijali.

Ikiwa na shida kazi ya baa utafanya na sio hiyo tu hata zingine zisizofaa kama kazi za ndani ( house girl). Huyo binti kufanya kazi baa haimaanishi hafai anaweza kufaa muhimu endelea kumchunguza.

Na nikuambie kitu kama ingekuwa sio shida za kiuchumi au tamaa za vitu wanawake ingekuwa nguma sana kuwapata.
 
U
Mkuu huu ni utetezi kama utetezi mwingine wowote!

Kijana 'fresh' hajaoa, aanze ndoa yake ya kwanza kwa kuoa nungayembe?

Tuchukulie hili swala ni la kwako, mdogo'ako wa tumbo anataka kuoa, waweza mshauri aanze maisha yake ya kwanza ya ndoa na mwanamke aliyeachika?

Emb tuweni serious kwa ushauri bas!
Una utibitisho kuwa huyo dada ni Nungaembe?? Wanaume wengi ni women abusers , sishangai kuona single and divorced mothers , ata wewe inaonekana unaweza kukontrol ndugu/mtoto wako aoe nani😭upo una taka dunia yote ifuate unavyotaka wewe! Kuuza bar sio Umalaya na wala sio kuwa kila muza bar yupo anajiuza. Mimi ni kaka na mzazi sijawia ingilia mausiano ya ndugu wala mtoto wangu na sintopoteza muda katika hilo wapo free kuoa au kuolewa na wamatakae. Na iwapo wataachana na wenziwao nawapa ushauri na kuwatuliza.kuna watu nawajua mama zao walikuwa wauza bar wakaolewa wakazaliwa na sasa ni watu mashuhuli na wema kabisa hapa Tanzania. One of the biggest person na maharufu na ameliletea taifa la TZ sifa kubwa kwa utendaji wake wa kazi hapa TZ ameo former bar maid na wapo mpaka leo. Kama mke na mume na wana wajukuu. Wewe ishi kwa kukariri
 
Kuna watu wana mahose girls majumbani mwao na wanawachia nyumba zao na vitu vya thamani na pia wanaamini 90% kama walezi wa watoto wao na pia wanaamini chakula wanachopikiwa na hawa madada lakini wanawadharua.Wajinga sana na wanajifanya smart mbele ya wengine wakati ni wapumbavu tu kama wapumbavu wengine.... chakula kapika yeye wakati wa kula mnamtenga ale peke ake🤣🤣
 
Mimi sio bro ni mwanadada. Nina umri wa kutosha sakafu ya tatu sasa.

Wewe kama ulisikiliza moyo wako na hata hukutaka kujua unaenda kuoa mtu wa aina gani mambo yakatick basi ni jambo la kushukuru Mungu lkn vipi kama mambo yangeenda tofauti? Usingeandika hiyo comment yako . Maana yangu ni kwamba angalau kabla ya kuingia kwenye mahusiano hasa ya ndoa ni better kuchukua time kujuana angalau kidogo. Neno langu sio sheria ila tusikurupuke. ahsante!
Kujuana labda kwa majina.

Lakini rangi halisi ya mtu huonekana baada ya kufunga ndoa.

Haya ya kujuana hayana uhalisia wenye manufaa.

Ndiyo maana vijana wengi wanaofeli kwenye ndoa, walikaririshwa hili.

Maana kujuana wengine wanachukulia kama kuishi na msichana ili kumuelewa background zake, ama 'kuonja mapishi' nk nk.

Kumbe hayo yote hupelekea saazingine kufubaza muhu wa kijana kuendeleza mchakato wake wa kufunga ndoa na msichana huyo na kuendelea kuangalia pengine.

Na 'kujuana' huko unakokusema kumebeba mambo mengi sana ambayo mengine hata wewe uliyelisema hili neno huyajui.

Kuna mila moja ya kwetu ambayo ikitumiwa kama shamba darasa itawavusha vijana wengi.

Ni kwamba: ukishamtamani msichana, ukamtongoza kwa nia ya kumuoa, akakukubalia na kisha ukaenda kwao kueleza nia yako kwa wazazi wake.

Wazazi watafanya utafiti kuhusu nasaba yako, kisha wakiridhia utaenda kupata jibu la go ahead na kutoa kishika uchumba.

Baada ya hapo ni mshenga pekee atakayewasiliana juu ya mahari na mipango ya ndoa na tarehe ya harusi.

Ni mwiko kijana kumzoea ama kulala na mchumba'ake kabla ya ndoa.

Haya yote yakizingatiwa yanalinda sana hadhi za wasichana.

Ndiyo maana nimetoa hoja kwamba kufahamiana ama kujuana saana kabla ya ndoa hakuleti afya.
 
Wewe ni mgeni na wahudumu wa bar.... Utakuja kupigwa na kitu kizito!!! Yaani we umeopoa siku ya kwanza tu unajiona mjanja? Jiulize kabla yako wameopoa wangapi ndugu, na wote mmepewa story hio hio, hata kama maisha magumu kiasi Gani mwanamke anayejua thamani yake hawezi kufanya kazi bar, period!!!
Mkuu samahani wewe ni msabato?
 
Mk
U

Una utibitisho kuwa huyo dada ni Nungaembe?? Wanaume wengi ni women abusers , sishangai kuona single and divorced mothers , ata wewe inaonekana unaweza kukontrol ndugu/mtoto wako aoe nani😭upo una taka dunia yote ifuate unavyotaka wewe! Kuuza bar sio Umalaya na wala sio kuwa kila muza bar yupo anajiuza. Mimi ni kaka na mzazi sijawia ingilia mausiano ya ndugu wala mtoto wangu na sintopoteza muda katika hilo wapo free kuoa au kuolewa na wamatakae. Na iwapo wataachana na wenziwao nawapa ushauri na kuwatuliza.kuna watu nawajua mama zao walikuwa wauza bar wakaolewa wakazaliwa na sasa ni watu mashuhuli na wema kabisa hapa Tanzania. One of the biggest person na maharufu na ameliletea taifa la TZ sifa kubwa kwa utendaji wake wa kazi hapa TZ ameo former bar maid na wapo mpaka leo. Kama mke na mume na wana wajukuu. Wewe ishi kwa kukariri
Mkuu umetetea kwa nguvu kubwa sana kulikoni?

Swali langu lipo pale pale.

Ukiwa kama mzazi na kaka wa kijana anayetaka kuingia kwenye ndoa utashauri nini?

Je utashauri kama uliyoyaandika hapa kwamba wewe upo free kufuata mawazo ayatakayo yeye?

Mi ninachojua, kushauri ni kutoa hints juu ya uzoefu wa jambo unalolishauri.

Naomba na mimi sasa nibakie na msimamo huu nilioshauri linapokuja swala la kushauri vijana wanaotaka kuingia kwenye ndoa.
 
Atutakiwi kuhukumu yeyote yule. Maana Mungu aliyemuumba anaweza mbadilisha either kuwa mtu mwema au kuja kuwa mtu mbaya. Mimi na wewe ni nani ata tuhukumu kuwa huyu dada awezi badilika??Matayo 7:1
 
nikamuuliza kazi umeacha kweli? akanijibu nimeacha kaka.

Baada ya zile story usiku wa jana nikamwambia haya lala mama.
Asubuhi wakati naamka nakuta kavaa pensi na t-shirt yangu vyombo vyote kaosha, nguo chafu kafua, kuna sufuria nilitakaga kuzitupa ila kaziosha zimekuwa nyeupe kama theluji.
Mliendelea kuitana KAKA na MAMA baada ya sufuria kuwa nyeupe kama theluji?
 
Kujuana labda kwa majina.

Lakini rangi halisi ya mtu huonekana baada ya kufunga ndoa.

Haya ya kujuana hayana uhalisia wenye manufaa.

Ndiyo maana vijana wengi wanaofeli kwenye ndoa, walikaririshwa hili.

Maana kujuana wengine wanachukulia kama kuishi na msichana ili kumuelewa background zake, ama 'kuonja mapishi' nk nk.

Kumbe hayo yote hupelekea saazingine kufubaza muhu wa kijana kuendeleza mchakato wake wa kufunga ndoa na msichana huyo na kuendelea kuangalia pengine.

Na 'kujuana' huko unakokusema kumebeba mambo mengi sana ambayo mengine hata wewe uliyelisema hili neno huyajui.

Kuna mila moja ya kwetu ambayo ikitumiwa kama shamba darasa itawavusha vijana wengi.

Ni kwamba: ukishamtamani msichana, ukamtongoza kwa nia ya kumuoa, akakukubalia na kisha ukaenda kwao kueleza nia yako kwa wazazi wake.

Wazazi watafanya utafiti kuhusu nasaba yako, kisha wakiridhia utaenda kupata jibu la go ahead na kutoa kishika uchumba.

Baada ya hapo ni mshenga pekee atakayewasiliana juu ya mahari na mipango ya ndoa na tarehe ya harusi.

Ni mwiko kijana kumzoea ama kulala na mchumba'ake kabla ya ndoa.

Haya yote yakizingatiwa yanalinda sana hadhi za wasichana.

Ndiyo maana nimetoa hoja kwamba kufahamiana ama kujuana saana kabla ya ndoa hakuleti afya.
Haya
 
Mkuu huu ni utetezi kama utetezi mwingine wowote!

Kijana 'fresh' hajaoa, aanze ndoa yake ya kwanza kwa kuoa nungayembe?

Tuchukulie hili swala ni la kwako, mdogo'ako wa tumbo anataka kuoa, waweza mshauri aanze maisha yake ya kwanza ya ndoa na mwanamke aliyeachika?

Emb tuweni serious kwa ushauri bas!
Ukweli ni kwamba wanawake wengi wanaolewa wakiwa wana mahusiano mengi Sana yaliyopita, Kwa wanawake mahusiano yaliyopita huwa wanapona ngumu sana kuelezea maana inakuwa ni aibu kwao.
Mdau ni muhanga wa kuongea ukweli, kitu ambacho wengi wetu hatupendi na tunapenda kufunika..
 
Mimi sio bro ni mwanadada. Nina umri wa kutosha sakafu ya tatu sasa.

Wewe kama ulisikiliza moyo wako na hata hukutaka kujua unaenda kuoa mtu wa aina gani mambo yakatick basi ni jambo la kushukuru Mungu lkn vipi kama mambo yangeenda tofauti? Usingeandika hiyo comment yako . Maana yangu ni kwamba angalau kabla ya kuingia kwenye mahusiano hasa ya ndoa ni better kuchukua time kujuana angalau kidogo. Neno langu sio sheria ila tusikurupuke. ahsante!
Ndoa zote ni game of chance, hakuna tofauti kabisa na betting.
Mambo kwenda kombo au kunyooka ni swala la bahati sana halina uhodari!! Ninachojaribu kuelezea hapa ni kwamba Kuna nafasi zinakuja mara moja tu katika maisha usipotumia akili yako haiji tena hiyo nafasi.
Kujuana kwenye mahusiano haina guarantee yoyote kama mtadumu.
 
Back
Top Bottom