Sehemu inavyowachukulia wahudumu wa bar inaonesha mengi kuhusu maadili ya sehemu hiyo. Na mengine ni matatizo ya umasikini na ujinga tu.
Habari kama hizi zinanikumbusha mtoto mmoja Italian American nilifanya naye kazi hapo Wall Street, New York, New York. Mtoto kakaa kama Julia Roberts, aki smile unaweza kusahau kazi ukawa unamuangalia tu, mtoto mcheshi, mtoto anatoka familia bora baba yaje alikuwa mkurugenzi mmoja mkubwa katika benki mashuhuri.
Licha ya yote hayo, huyo Julia lookalike alikuwa mcheshi sana. Sasa kila Ijumaa ilikuwa tunaulizana mipango ya weekend imekaaje? Siku moja akaniuliza, nikamwambia mipango yangu. Nikamuuliza na yeye, atafanya nini?
Jibu alilonipa lilinishangaza sana kwa binti ambaye nilimuweka matawi ya juu kama yeye. Aliniambia atakuwa anahudumia katika bar (bartend). Nikashangaa sana, mtoto mzuri, mwenye elimu, aliyetoka familia bora kama huyu anaenda kuwa barmaid tena?
Akanifafanulia zaidi, akasema huwa anafanya hivyo mara nyingi, bar yenyewe baba yake ni kati ya wanaoimiliki, halafu watu wanaokuja ni kama wanajuana wote, na kisha, anaipenda hiyo kazi kwa sababu anapata ku interact na watu sana na kumix vinywaji, zaidi, anapiga hela ndefu sana kwenye tips (huku kila mtu anayehudumiwa analipa bakhshishi/tip kwa mhudumu). So akasema huwa anapata mpaka dola za Kimarekani 500 kwa usiku mmoja kutokana na tips hizo.
Nikipata somo kubwa sana kwamba inawezekana kwa mwanamke mwenye heshima zake, mzuri, kijana, anayefanya kazi Wall St., anayetoka familia bora, akafanya kazi ya uhudumu wa bar, bila kuonekana malaya.
Nilijifunza pia kuwa wenzetu wanaheshimu sana kazi, yani huyu dada hakuona haya kusema kuwa yeye anafanya uhudumu bar, aliona fahari kuwa anafanya kazi, anatumia ujuzi wake wa ku mix vinywaji, anafanya kazi inayompa social interaction nzuri kwa family and friends, na anapata kipato kizuri cha ziada.
Na zaidi, nilijifunza kuwa wanaume wanaweza kwenda bar na kuwaheshimu wahudumu kwa kunywa vinywaji vyao bila kuwabugudhi wahudumu, na zaidi, kwa kuwapa tips nzuri tu zitakazoonesha wanathamini kazi zao.
Je, na sisi hatuwezi kuweka jamii inayojali kama hivi?