Kuna wakati maisha yanakuwa magumu hadi unaelewa kwanini baadhi ya wadada kuamua kujiuza

Kuna wakati maisha yanakuwa magumu hadi unaelewa kwanini baadhi ya wadada kuamua kujiuza

Suala la kujiuza ni jambo la udhalili na pia kimaadili halifai, lakini inafika wakati, hali ya maisha inakua ngumu hadi mtu anaona, njia pekee ya kujinasua ni kutumia mwili wake, mdada akiangalia wateja anaweza kuwapata anaona bora niingie huku.

Anaweza asifike hatua ya kujipanga barabarani lakini aajua tu apate wapi huyo mteje, wengine watakutumia meseji mfano " Haszu ninashida kweli kweli, niko tayari kwa lolote ili mradi nipate hiyo hela niweze kutatua tatizo langu".

Najua wapo tena ndio wengi ambao wamekubuhu na wanafanya haya mambo kama biashara, ila pia naamini ipo asiimia kubwa ya waliojikuta katika hali ngumu ya maisha na wakaona hana namna ila ya kujiuza.

Eeeh Mungu, Utupe siku kwa siku riziki yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].
 
Daah hatuna kiungo mkabaji hapa aisee daah na wahuni wanaosaka hii nyasi wapo kimya hatari sana..
 
Biashara ya kujiuza ilianza takribani miaka 5000 iliyo pita , hivyo wewe mtoto wa juzi hapa unapoteza mda wako hata kuizungumzia

La kuzungumzia hapa ni inakuaje mtoto wa kiume uwe na pigo za kike kike?
Hivi huyu jamaa ni team cocastic? Naona raia wengi mnampa makavu
 
Jamani jamani nyie viumbe wa JF mtaani kugumu msichulie poa wadada wengi wanaliwa sio kwa kupenda ila dhiki tu ....mwishoe anajikuta malaya kakubuhu hajali tena.

Hivi mtu analipwa afu tatu kwa siku akipewa 20k mshahara wa week nzima unafikiri hatoi mzigo huyo???? Wakipita wadau wanne watano hajawa malaya huyo ??hajaona kawaida??? Acheni kabisa mtaani pazito nimekaa kitaa miaka minne ya msoto mkali naelewa vita yake.

Haya maisha bora yamchape mtoto wa kiume atakaza ila wakike utawaonea huruma aisee mabinti wanaliwa sana kwa ahad za ajira feki noma sana.

Ukiona mambo yako yanaenda mshukuru Mungu funga bakuli hilo.
Hawatakuelewa ila hawa dada zetu kuna wakati wanapitia hali ngumu sana mpaka kujikuta ktk hali kama hiyo.
 
Back
Top Bottom