Kuna wanafunzi wa shule za umma bado wanakaa chini

Kuna wanafunzi wa shule za umma bado wanakaa chini

Hassanjk

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2023
Posts
333
Reaction score
689
Nafikiri ifike mahala watu wamalize hii changamoto jamani.

Hivi unajionaje uko mjini unatembelea usafiri wa Nguvu halafu kule kijijini ulikotoka Watoto wanakalia mawe darasani? Na kuna mikoa ina misitu na inauza mbao nayo eti inamatatizo ya madawati; Ni aibu!

Naamini hili la madawati na vyoo linaweza kumalizwa kwa ushirikiano wa wazazi na Wilaya/Mkoa. Mbona kuna baadhi ya mikoa imeweza kwa kujitolea tu kwa wanachi? Nyie wengine mnaojifisia huku Mijini, kwenye vijiwe nk mmefanya nini kjijini kwenu?

Najua kizazi hiki kimegubikwa na ubinafsi mkubwa sana wa kujifikiria wao na watoto wao (BMW), ila amini tu hata ungejilimbikizia mali kama Mchwa, hutaenda navyo kaburini na pengine huku nyuma zichezewe tu.
 
Kila ninapopata uzi unaofanana na huu, [unaougusa na kushawishi umaskini wa Kiafrika] nahisi kukerwa. Siwezi kujua kwa nini. Pamoja na kuwa mleta mada anaweza kuwa ana nia nzuri, mara nyingi nyuzi kama hii huishia kutukana Jamii nzima ya mwafrika/mtanzania(hili linakera) badala ya wahusika, au wale walio na dhamana ya kufanya mabadiliko hayo.

Hatahivyo, kuna hoja zilizowasilishwa vyema, nashauri tuwe tunaangalia na kuwasilisha taarifa bila ya kubeza tamaduni za maeneo husika kwa usawa.
 
Back
Top Bottom