Ja Mara
Member
- Aug 19, 2021
- 50
- 51
KUNA WATU HAWAJUI KUWA WANAWEZA KUPATA MFUMO WA KUSIMAMIA BIASHARA BURE KABISA! 😳
Rafiki yangu mmoja siku moja aliniambia anatafuta mfumo wa kusimamia biashara yake, lakini mifumo aliyokuwa anaiona ilikuwa ya kulipia na bei zake zilikuwa ghali sana kwake.Nikamuuliza, “Kaka, unafanya biashara gani?”
Akanijibu, “Mimi nakopesha watu fedha.”
Nikamuambia, “Ooh, sawa kaka. Nipe siku kadhaa nione namna ya kukusaidia. Nitatafuta njia ya kukutengenezea mfumo ambao unaweza kuutumia bila kununua software ya gharama kubwa.”
Nikamuuliza tena, “Kwa sasa unasimamia mikopo yako kwa kutumia nini? Excel?”
Akasema ndiyo.
Nikajiambia, hapa lazima nifanye kitu.
HAPA NDIPO SAFARI YA KUJENGA MFUMO ILIPOANZA! 😂
Nikaanza kufikiria namna ya kumtengenezea mfumo ambao angeweza kutumia bila mimi kuanza kutumia pesa nyingi kununua server na kulipia miundombinu.Ghafla nikakumbuka kwamba nilikuwa na blog yangu ya Blogger!
Nikajiambia, “Ngoja kwanza! Blogger si kuna sehemu ya Pages inayokubali kuweka HTML? Hapa ngoja nifanye mambo!” 😂
Nikaingia kwenye Blogger yangu, nikafungua sehemu ya Pages, nikaanza kuifanyia kazi.
Wazo langu lilikuwa kutumia Blogger kuendesha mfumo, kisha niunganishe na Google Drive pamoja na Google Sheets ili kurahisisha uhifadhi na usimamizi wa taarifa za mikopo.
Lakini nikakutana na swali muhimu.
Je, nitahifadhi taarifa za rafiki yangu kwenye Google Drive yangu?
Nikajiambia, “Hapana! Kwa nini nitumie Drive yangu wakati yeye ana akaunti yake ya Google?”
Hapo nikaanza kushughulikia Google Authentication ili kila mtumiaji aweze kuunganisha akaunti yake ya Google na kutumia Google Sheets yake kwa taarifa za biashara yake, badala ya kutegemea Google Drive yangu kama hifadhi ya taarifa za kila mtu.
Yaani kila nilipokutana na changamoto, nilitafuta njia ya kuitatua mpaka nipate suluhisho.
Hizi ni zile mbinu za panya kuchimba shimo mpaka afike kwenye ghala la chakula! 😂😂
LAKINI KABLA SIJAUACHIA MFUMO MTANDAONI, NILIONGEZA MAMBO MENGINE!
Nikajiuliza, kama ninajenga mfumo ambao unaweza kutumiwa na watu duniani kote, kwa nini niuwekee mipaka ya nchi moja au lugha moja?Ndipo nikaongeza lugha 12 na sarafu zaidi ya 150 za duniani ili mfumo uweze kuwafaa watumiaji kutoka masoko na nchi mbalimbali.
Na sikuishia hapo. Niliongeza vipengele vingine muhimu, vikiwemo:
🌍 Lugha 12 — ili watumiaji kutoka maeneo mbalimbali waweze kutumia interface ya mfumo kwa lugha wanayoielewa.
💱 Sarafu zaidi ya 150 — kusaidia matumizi katika masoko mbalimbali ya dunia.
☁️ Muunganisho wa Google Drive na Google Sheets — mfumo umeundwa kuunganishwa na akaunti ya Google ya mtumiaji, na kurahisisha kusawazisha na kuhifadhi taarifa zake.
📊 Loan Amortization — kufuatilia marejesho ya mkopo, sehemu ya mtaji, riba na athari za malipo ya ziada kwenye gharama za riba.
📄 Ripoti zinazoweza kupakuliwa — kutoa ripoti katika PDF na CSV au kuzichapisha kwa matumizi ya kumbukumbu na usimamizi wa biashara.
🧾 Nyaraka za kifedha — kuandaa ripoti za mikopo katika muundo unaofaa kwa kumbukumbu na nyaraka za biashara.
💸 Hakuna ada ya subscription — mfumo umewekwa ili watu waweze kuutumia bure kabisa, bila kulazimika kuanza kwa kulipia kifurushi cha kila mwezi bali utakapo wiwa unaweza kuninunulia kahawa!.
Nilitaka kutengeneza kitu ambacho si cha kumsaidia rafiki yangu tu, bali ambacho kinaweza kuwa na manufaa kwa wakopeshaji wengine pia.
NDIPO NIKAJIULIZA SWALI MOJA…
Kama nimeweza kutengeneza mfumo huu, kwa nini niufungie kwa mtu mmoja wakati kuna watu wengine wengi wenye changamoto hiyo hiyo?Nikaamua kuuachia mtandaoni ili watu wengine waweze kuutembelea na kuujaribu.
Mfumo huo unaitwa SmartLoan Global, na unaweza kuutembelea hapa:
👉 https://smartloanengine.blogspot.com/
Lengo lake ni kusaidia wakopeshaji na watu wanaosimamia mikopo kufuatilia taarifa za wateja, mikopo, riba na marejesho kwa njia iliyo rahisi zaidi.
Kitu kilichoanza kama jaribio la kumsaidia rafiki yangu kikawa mfumo ambao nimeupanua ili uweze kuwafaa watu wengi zaidi.
SASA HAPA NDIPO NINAPOWAHITAJI WANA JF!
Nimejiuliza, kama kuna watu wengi ambao bado wanasimamia biashara zao kwa kutumia madaftari, Excel au WhatsApp kwa sababu mifumo ya kulipia ni ghali, kwa nini tusijaribu kutafuta suluhisho linalowezekana?Ndiyo maana nimeamua kutoa nafasi hii kwa wana JF.
Natayari mimemaliza ujenzi wa "Personal finance manager" Na itakua online soon na itawafaa sana.
Unahitaji mfumo wa kusimamia biashara yako lakini huna uwezo wa kulipia mfumo wa gharama kubwa?
Labda unahitaji mfumo wa:
- 🏪 Kusimamia duka, mauzo na stock.
- 🏫 Kusimamia shule, wanafunzi na ada.
- 💇 Kusimamia salon na miadi ya wateja.
- 🍽️ Kusimamia restaurant, oda na bidhaa.
- 💰 Kusimamia mikopo, madeni na marejesho.
- 👥 Kusimamia wateja au wafanyakazi.
- 📅 Kusimamia bookings au shughuli nyingine za biashara.
🎁 OFA YANGU KWA WANA JF
Niambie mfumo unaohitaji!Kama ni mfumo ninaoweza kuutengeneza, nitajitahidi kukutengenezea na kukupa nafasi ya kuutumia kabisa.
Lengo langu ni kutumia ujuzi nilionao kutatua changamoto halisi ambazo watu wanakutana nazo kwenye biashara na shughuli zao za kila siku.
Siwezi kuahidi kwamba nitaweza kutengeneza kila wazo, lakini niko tayari kusikiliza mawazo yenu na kufanya kazi kwenye yale ninayoweza kuyatekeleza.
Huhitaji kuwa na kampuni kubwa. Hata kama una biashara ndogo au ndiyo unaanza, unaweza kushiriki.
WANA JF, NINA SWALI MOJA TU:
👇 NI MFUMO GANI UNAHITAJI LAKINI HUJAUPATA KWA SABABU YA GHARAMA ?
Andika biashara unayofanya na mfumo ungependa ukusaidie kufanya nini.
Huenda wazo lako likawa mwanzo wa mfumo mwingine utakaorahisisha maisha ya watu wengi. 🚀